Msimamo wangu bado ni ule ule kwamba tanzania hatuna mwamko wa dhati na huu mradi wa EAC integration na kwa kiasi kikubwa sana, nchi yetu ndio sababu kwanini mchakato wa integration umekuwa unasua sua; Huu ndio ukweli wenyewe, hata kama ni mchungu namna gani; Ni muhimu tufanye maamuzi magumu sasa kwamba je, are we in or out, instead of sitting on the fence;
Kauli na vitendo vyetu vimetawaliwa Zaidi na woga and defensiveness kuliko engagement katika mchakato husika kwa hali ya kujiamini; Kuna mifano kadhaa ya kuthibitisha haya, na inashangaza sana kwanini bunge letu ambalo sasa linatajwa kuwa na mamlaka ya kufanya maamuzi muhimu juu ya suala husika, bunge hili limekuwa kimya kujadili au kufanyia maamuzi kama haya:
1. Mwezi februari mwaka jana (2012), Tanzania ilifunga mpaka wake na kenye (maeneo ya Taveta) ghafla tu, baada ya madereva wa malori kugoma kupinga uamuzi wa Tanzania kutoza $200 kwa magari kutoka Kenya; Uamuzi wa Tanzania ulikuwa ni kinyume na common market protocol ambayo lengo lake ni kupunguza vikwazo vya biashara within the EAC block; Je, nani aliwajibishwa kwa violation hii ya CMP pamoja na hasara zilizojitokeza? Je, bunge au serikali zilishughulikia suala hili rationally? Majibu ya wengi yatakuwa ni ya kisiasa Zaidi;
2. Mwezi May mwaka juzi (2011), serikali ya Tanzania ilipiga marufuku usafirishaji wa mazao ya nafaka kwenda nje ya nchi (ikiwa ni pamoja mipakani na fellows EAC members) kwa hoja kwamba such trade was unregulated, ambayo ilipelekea uhaba wa chakula na mfumuko wa bei; Uamuzi huu ulitokea katika kipindi ambacho wakulima wa mazao ya nafaka walikuwa hawana soko la uhakika (kwa kawaida, tani nyingi za mahindi mikoa ya nyanda za juu kusini huwa zinaozea tu kwenye maghala kutokana aidha kwa kukosekana kwa soko au ulafi wa wafanyabiashara wa kihindi kubania mahindi so as to create artificial shortages ili wapate faida kubwa baadae); pia uamuzi huu wa serikali ulikuja katika kipindi ambacho wenzetu wa kenya walikuwa katika food crisis & famine kwenye maeneo kadhaa ya nchi yao; Uamuzi wa serikali yetu haukutuma a positive vibe kwa wanachama wengine wa EAC; Je, bunge lilishughulikia suala hili? Was it done rationally? Hata katika hili, majibu ya wengi yatakuwa ni ya kisiasa Zaidi;
3. Mwaka huo huo wa 2011, mahakama kuu ya Tanzania iliingilia kati kesi iliyofunguliwa na East African Development Bank dhidi ya kampuni ya kifisadi ya Tanzania (Blueline) ambayo ilifiadi Zaidi ya $130 million na kutishia kuifilisi EADB; kwanini Tanzania tuliamua kuwa obstructionist wa haki hii ya EADB? Kwa faida ya nani? Je, bunge lilichukua hatua gani kunusuru benki hii pamoja na kulinda interest za Tanzania na za nchi wanachama? Majibu mengi pia katika hili yatakuwa ni ya kishabiki na kisiasa Zaidi kuliko mantiki;
4. Mwezi November 2011, kwenye Bujumbura summit, Tanzania ilikataa kutia sahihi makubaliano juu ya establishment of the EAC political federation & mutual defense pact; hoja ya Tanzania dhidi ya political federation ilikuwa kwamba suala la ardhi lisihusishwe; Pia, tulikataa kutia sahihi makubaliano juu ya mutual defensive pact kwa hoja kwamba tungeweza kujikuta tukiingia katika vita kutokana tu na irresponsible leaders katika nchi wanachama; Hoja dhidi ya mutual defensive pact ina mashiko, lakini suala la ardhi kidogo kuna mashaka – hivi tunafahamu jinsi gani wageni kutoka nje (wazungu na waarabu na wachina) wanavyozidi kukamata maelfu ya heka za ardhi ya watanzania? Kwanini tunatetea wananchi wa Tanzania kinafiki? Kwanini hatuoni tatizo la wageni (wazungu, waarabu, wahindi) kuhodhi maelfu ya hekari za ardhi tena bila kushirikisha wananchi lakini suala la raia wa wenzetu wa EAC ndio tunaona ni tatizo? Kwanini hatuogopi raia wa nje ya afrika kuchukua ardhi lakini tunaogopa raia wanachama wa EAC? Je ina maana hatukuliona hili tatizo huko nyuma na tulikosa fursa za kuwaandaa wananchi kupitia effective policies za kuangalia maslahi ya watanzania juu ya suala la ardhi ili waingie katika federation wakiwa wamejiandaa? Katika hili, pia majibu ya wengi katika hili yatajaa siasa na ushabiki kuliko mantiki;
cc
Mimibaba
candid Scope
timbilimu