Membe: Tunasubiri talaka Jumuiya Afrika Mashariki

Membe: Tunasubiri talaka Jumuiya Afrika Mashariki

Kuna watu hapa wanaipinga kauli ya Mh. Membe lakini hawatoi political, economic and social alternative.

Waziri Membe yuko sawa na uamuzi wa serikali unapaswa kupongezwa. Serikali "dhaifu" imesimama kidede kutetea maslahi ya Taifa. Tanzania haiathiriki chochote katika mikutano ya hawa Marais na ndiyo maana serikali inawaangalia tu ikisubiri watoe maamuzi mazito na siyo haya mepesi ya kujificha ficha.

Kwanza hili shirikisho kwa kiwango kikubwa liko based na matakwa ya marais badala ya wananchi kupitia taasisi zake kama bunge au direct representative (referendum).

Think about EAC after Pres. Museveni and Pres. Kagame ikichukuliwa kuwa hata misingi ya kidemokrasia katika nchi zao haiko imara achilia mbali kuwepo kwa makundi based on tribe and political debarment.

Siwezi hata kuongea juu ya Pres. Kenyatta kwa sababu anasumbuliwa na naively.

The entire episode is a talking shop.

Point!
 
Ni sawa kabisa..sisi ndoa yetu ipo sadc, eac wauza sura wengi..
 
Wananchi wa Tz hatutaki huu muungano wa this shit called EAC, period.
 
wewe na membe ni vipofu.
mtajutia sana haya maneno ya kanga yanayotumiwa na membe badala ya kutumia namna ya kidiplomasia kutatua matatizo ya kimahusiano.

CCM mnaakili kweli?

Nani atajutia wewe acha uoga...yani nyie Chadema kila kitu mnaleta siasa zenu za kishabiki.
 
Kijana jenga hoja badala ya kauli hizi za kitoto!

Hakuna utoto hapo, mbona unatoka povu la njano babu!!?. Kwa hili nipo upande wa Waziri Membe. Kama wewe ni Mtanzania halisi na nimfuatiliaji wa hili bundi EAC, basi utakuwa umeona au kusikia mauzauza mengi yaliyotokea dhidi yetu(TZ), sasa kwa kwa taarifa yako watanzania halisi tumekaa chonjo, wengine nyinyi wakuja tu. Au wewe unataka mpaka KKK watuchukuwe msukule nini!?... Uwenda hata wewe pia ni mpasua nazi wa Sezibera katika njia panda za Tanzania. USHINDWE.
 
Huyu jamaa wa ajabu sana badala ya kuwaambia hao jamaa wa Kenya, Uganda na Rwanda hizi issue anaenda zungumzia Clouds!! watasikia kweli? au ni yaleyale ya kusemea chumbani ukitoka nje kimya..

Aliongelea Clouds sababu walimuuliza akajibu,,sasa ulitaka asemeje?
 
Msimamo wangu bado ni ule ule kwamba tanzania hatuna mwamko wa dhati na huu mradi wa EAC integration na kwa kiasi kikubwa sana, nchi yetu ndio sababu kwanini mchakato wa integration umekuwa unasua sua; Huu ndio ukweli wenyewe, hata kama ni mchungu namna gani; Ni muhimu tufanye maamuzi magumu sasa kwamba je, are we in or out, instead of sitting on the fence;

Mimi naamini Diplomasia inayotumiwa na wahusika katika serikali yetu ina hekima, kuepusha mtafaruku kwa viongozi wa "shirikisho fake" wasiojulika kwa dhamira yao. Hawa watu sio kuwa hawajui wanachokifanya na wanachokita. Wanaweka shinikizo kwa matarajio kuwa tutafanya makosa kwenye maamuzi. Ni kipindi kizuri kuwatia moyo akina Membe kwa tahadhari wanayoichukua kwa kuwa ina tija SUBIRA YAVUTA HERI


1. Mwezi februari mwaka jana (2012), Tanzania ilifunga mpaka wake na kenye (maeneo ya Taveta) ghafla tu, baada ya madereva wa malori kugoma kupinga uamuzi wa Tanzania kutoza $200 kwa magari kutoka Kenya; Uamuzi wa Tanzania ulikuwa ni kinyume na common market protocol ambayo lengo lake ni kupunguza vikwazo vya biashara within the EAC block; Je, nani aliwajibishwa kwa violation hii ya CMP pamoja na hasara zilizojitokeza? Je, bunge au serikali zilishughulikia suala hili rationally? Majibu ya wengi yatakuwa ni ya kisiasa Zaidi;

Jibu langu ni kuwa hakuna aliye kurupuka kuufunga mpaka huo. Na kama kuna aliyeathirika basi angechukua hatua za kisheria zilizopo kudai haki yake. Singependa kuuliza kwa nini hawajachukua hatua; naamini pamoja na hatua za kidiplomasia kuna maridhiano fulani na waya forward.
Siamini kama ni mawazo yako haya ila naheshumu sana

2. Mwezi May mwaka juzi (2011), serikali ya Tanzania ilipiga marufuku usafirishaji wa mazao ya nafaka kwenda nje ya nchi (ikiwa ni pamoja mipakani na fellows EAC members) kwa hoja kwamba such trade was unregulated, ambayo ilipelekea uhaba wa chakula na mfumuko wa bei; Uamuzi huu ulitokea katika kipindi ambacho wakulima wa mazao ya nafaka walikuwa hawana soko la uhakika (kwa kawaida, tani nyingi za mahindi mikoa ya nyanda za juu kusini huwa zinaozea tu kwenye maghala kutokana aidha kwa kukosekana kwa soko au ulafi wa wafanyabiashara wa kihindi kubania mahindi so as to create artificial shortages ili wapate faida kubwa baadae); pia uamuzi huu wa serikali ulikuja katika kipindi ambacho wenzetu wa kenya walikuwa katika food crisis & famine kwenye maeneo kadhaa ya nchi yao; Uamuzi wa serikali yetu haukutuma a positive vibe kwa wanachama wengine wa EAC; Je, bunge lilishughulikia suala hili? Was it done rationally? Hata katika hili, majibu ya wengi yatakuwa ni ya kisiasa Zaidi;

Mimi ni mkulima niliathiriwa na uamuzi huo; nakiri ulichukuliwa bila matayarisho ya kutosha; lakini pamoja na uamuzi kutokuwa wazi kabisa hoja ya kuepusha uwezekano wa kuuza mazao na kusasababisha njaa ina mashiko. Tatizo ni udhaifu wetu au viongozi wetu kufanya maamuzi wakati muafaka. Pili ni kweli kama kungekuwa na utaratibu wa wazi na si wakiholela haya yote yasingetokea. Nakuhakikishia wenzetu wanataka hali hii yakufanya mambo kiholela. Ndiyo iliyovunja EAC ya mwanzo. Mimi kama mkulima nitafurahi kama soko litakuwa la wazi linalosimamiwa na utratibu wa wazi.

3. Mwaka huo huo wa 2011, mahakama kuu ya Tanzania iliingilia kati kesi iliyofunguliwa na East African Development Bank dhidi ya kampuni ya kifisadi ya Tanzania (Blueline) ambayo ilifiadi Zaidi ya $130 million na kutishia kuifilisi EADB; kwanini Tanzania tuliamua kuwa obstructionist wa haki hii ya EADB? Kwa faida ya nani? Je, bunge lilichukua hatua gani kunusuru benki hii pamoja na kulinda interest za Tanzania na za nchi wanachama? Majibu mengi pia katika hili yatakuwa ni ya kishabiki na kisiasa Zaidi kuliko mantiki;

Mkuu hapo unagusa mshipa wa fahamu wa watawala wetu UFISADI, nitasikitika sana bunge au taasisi yo yote inapohusishwa na kutetea ufisadi; lakini inatupasa kutenganisha maslahi ya nchi na ya watu binafsi. Kwa bahati mbaya hakuna mstari wa kutenganisha maslahi binafsi na ya kitaifa katika utawala wa sasa MAJANGA.

4. Mwezi November 2011, kwenye Bujumbura summit, Tanzania ilikataa kutia sahihi makubaliano juu ya establishment of the EAC political federation & mutual defense pact; hoja ya Tanzania dhidi ya political federation ilikuwa kwamba suala la ardhi lisihusishwe; Pia, tulikataa kutia sahihi makubaliano juu ya mutual defensive pact kwa hoja kwamba tungeweza kujikuta tukiingia katika vita kutokana tu na irresponsible leaders katika nchi wanachama; Hoja dhidi ya mutual defensive pact ina mashiko, lakini suala la ardhi kidogo kuna mashaka – hivi tunafahamu jinsi gani wageni kutoka nje (wazungu na waarabu na wachina) wanavyozidi kukamata maelfu ya heka za ardhi ya watanzania? Kwanini tunatetea wananchi wa Tanzania kinafiki? Kwanini hatuoni tatizo la wageni (wazungu, waarabu, wahindi) kuhodhi maelfu ya hekari za ardhi tena bila kushirikisha wananchi lakini suala la raia wa wenzetu wa EAC ndio tunaona ni tatizo? Kwanini hatuogopi raia wa nje ya afrika kuchukua ardhi lakini tunaogopa raia wanachama wa EAC? Je ina maana hatukuliona hili tatizo huko nyuma na tulikosa fursa za kuwaandaa wananchi kupitia effective policies za kuangalia maslahi ya watanzania juu ya suala la ardhi ili waingie katika federation wakiwa wamejiandaa? Katika hili, pia majibu ya wengi katika hili yatajaa siasa na ushabiki kuliko mantiki;

Mimi nakubaliana na hoja yako ingawaje sikubaliani na hitimisho lako. Suala la ardhi ni mwiba kwa sababu wanaofaidika nalo ni walioko madarakani ambao ndio wanawapa hao wahindi na hao warabu mapande ya ardhi; waathirika ni wale ambao hawana maamuzi wala hawana wakuwasemea au kuwatetea. Mbaya zaidi hili suala lina miziz kwenye katiba mbovu. Chakufanya ni kupigia upatu ipatikane katiba inakidhi mahitaji ya mwananchi wa kawaida

Natanguliza shukrani kwa fursa ya kuchangia
 
Tanzania is a sleeping Economic Giant of Africa. Hatuna cha kupoteza. Hawa wanaoungana bila ya sisi wasingekuwepo. Wao ni kuuana kila kukicha. Sasa muungano wa wauaji si wa kututisha. Watakapochokana wataanza tena kuuana na ndipo watatuita tena tuwasaidie. Bravo Tanzania - We don't need EAC.
 
Hongera Mh.JK , Membe na Sitta kwahili yuko pamoja na itikadi za vyama pembeni ni utaifa kwanza.

Ni heri tukaachana nao maana ukifuatilia historia za nchi zao ni kuuwana wenyewe kwa wenyewe kwa kupenda ukabila wa hali ya juu sasa jifikirie ikiwa wao tu hawapendani atakuja kukupenda Mtanzania wewe ambae ni Mgogo sijui. Ardhi ni rasilimali watu.
 
Kiongozi ukiwa unaongozwa na Wananchi wako ni hatari.Kuwa Kiongozi inamaanisha kuongoza njia.Kuna baadhi ya mambo mazito Wananchi hawana uelewa nayo wa kutosha maana tungetumia busara hiyo hiyo ya kuheshimu MAONI ya Wananchi nahisi leo hii tungekuwa bado tupo katika mfumo wa Chama kimoja.Watanzania hii mentality yetu ya kubadilika pole pole mno wakati sehemu nyingine za Dunia zinabadilika kwa kasi.Binafsi nafurahishwa na hatua za mageuzi ya kiuchumi zinazochukuliwa na Rwanda na hasa ile mipango yao ya kujenga jiji jipya na la kisasa kabisa la Kigari pamoja na kuanzishwa kwa matumizi ya IT bure ambayo inalenga kutengeneza mazingira mazuri ya kibiashara na uewekezaji Nchini Rwanda.Hizi ndio faida tungeweza kuzipata ktk EAC kupitia kubadilishana uzoefu na Nchi nyingine.

Hauna point ya msingi bob,,labda it utuambia dadako kaolewa Kenya tukusogeze ukweni tutakuelewa...maana iyo Rwanda unayoiongelea we umeisoma kwenye karatasi sisi tumeiona hamna kitu uko cha maana,,labda hotuba nzuri za Kagame...
 
Mchango mzuri mkuu,na hii itafanya tuendelee kutawaliwa na wageni milele tena kwa manyanyaso makubwa,serikali kuwafukuza watz na kuwapa wageni ni sawa ila akichukuwa mwafrka mwenzio ni haramu,bado tunahitaji ukombozi wa fikra.

we ndio unaitaji ukombozi wa kifikra..Kwaio tuwape ardhi yetu hao waafrica wenzetu??bas tutakuwa cha wote!!
 
Pangua hoja kwa hoja badala ya kutambia uzalendo uchwara! Siwezi tetea udhaifu wa watala eti nionekana ni mzalendo wa kweli wa Tanzania. Kama unataka kuishi dunia ya aina hiyo omba uraia wa Korea Kaskazini na Zimbabwe ambako watawala wanajiona ni viumbe tofauti na wananchi wengine!

Kama wewe na ndugu zako Membe toka Mtama,Lindi na Jakaya Kikwete toka Msoga mnaona EAC ni takataka hayo ni mawazo yenu binafsi,tofauti na mimi Mhaya toka Bkb,Kagera.ambayd nchi zote za EAC zinapakana na mkoa wangu! Heri mmalize utawala wenu salama badala ya kutuachia maadui kila sehemu baada ya kuivuruga nchi kwa.udini!

Wewe sio muhaya,,,wewe ni mnyarwanda na mtajitaja tu leo..
 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amesema nchi za Rwanda, Kenya, Burundi na Uganda hazina haja ya kuanzisha shirikisho lao la siri kwani Tanzania itakapofikia hatua ya kutaka kujiondoa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), suala hilo litapelekwa Bungeni ili lijadiliwe na wabunge wataliridhia.

Akihojiwa jana asubuhi na Cloud Radio, Membe alisema kuwa nchi hizo hazina sababu ya kufanya mambo kwa siri kwani kama wameshindwa na ni vema kuieleza Tanzania. “Kama ni talaka moja watupe tu. Sisi tunasubiri kupewa talaka.”

Afafanua msimamo wa Tanzania baada ya nchi hizo kuonekana zikifanya jitihada za kuanzisha shirikisho lao na kuitenga Tanzania, Membe alisema nchi hizo ziwe wazi na wakweli kama zinaona kuna jambo ambalo hazilidhiki nalo ambalo Tanzania inalifanya na busara itumike kulizungumza kwenye mikutano badala ya hivi sasa zinapoamua kuanzisha muungano wao wa siri.

“Tutakapoamua ku-suspend relationship (kusimamisha uhusiano) na Afrika Mashariki, tutakapoamua kujiondoa kwenye utaratibu huu wa shirikisho la haraka haraka, tutapeleka suala hili bungeni. Bunge litajadili na nina uhakika wabunge wataangalia busara ya kutokuharakisha wala kudhulumiwa wala kuburuzwa, tutawaacha waendelee kwa raha mustarehe, ila sisi tunachoomba tu wawe wakweli, wawe wawazi si kutengeneza muungano wa siri siri,” alisema.

Alipoulizwa kama hali hii inachangiwa na nini hasa, kama ni kutokana na msuguano baina ya Rais Jakaya Kikwete na Rais wa Rwanda Paul Kageme, wa hivi karibuni au ni msukumu wa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, kutaka kutimiza azma yake ya kuwa rais wa kwanza wa Shrikisho hilo, Membe alisema yanawezekana.

Hata hivyo, alifafanua kuwa kuna mambo kadhaa yanachangia, moja, ni msimamo wa Tanzania kukataa suala la ardhi kuingizwa katika mambo ya Jumuiya na kwamba ni jambo ambalo serikali haiwezi kukubali hasa ikizingatia kuwa ardhi ndiyo dhahabu ya nchi.

Alisema jambo
la pili linalolalamikiwa na nchi hizo ni hatua ya Tanzania kuwa mwanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc) na Katibu Mkuu wa Sadc kuwa ni Mtanzania. “Hivyo wanaona Tanzania damu yao ipo Sadc, kitu ambacho ni kweli, lakini hata hivyo, nao wasilalamike kwa sababu wapo IGAD na Comesa.”

A
liongeza kuwa jambo jingine linalolalamikiwa ni hatua ya Tanzania kupeleka majeshi yake Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na kuwapa kipigo kizuri kikundi cha waasi cha M23 kati ya Agosti 26 na 28 mwaka huu hatua ambayo nchi hizo zinakiona ni kama kudhoofisha Muungano wa Afrika Mashariki.

Kuhusu jinsi gani kitendo cha kuwapiga M23 kinavyodhoofisha muungano alisema: “Kwa sababu wale M23 Tanzania inakwenda kwa principle (misingi) inayosema tunapoona nchi ya Afrika Mashariki au ya Sadc inakwenda kinyume cha matakwa ya wananchi au haifuati kanuni za uongozi bora, sisi huwa tunaingilia, siyo maana kwamba tunavunja Jumuiya Afrika Mashariki.”

Membe alisema nchi za Rwanda, Uganda, Kenya na Burundi baada ya kuona Tanzania haitaki suala la ardhi kuingiza EAC, na bado ni wanachama wa Sadc na kwamba haitaki kuanzisha Shirikisho la Afrika Mashariki haraka haraka na baadhi ya viongozi wa dunia kufanya ziara Tanzania, waliamua kuanzisha shirikisho lao la siri.

Viongozi wakuu duniani waliotembelea Tanzania mwaka huu pekee ni Rais wa China, Xi Jinping, na Rais wa Marekani Barack Obama..

Alisema nchi hizo zilipaswa kutumia utaratibu kama kuna mambo yanawakera ambayo Tanzania inayafanya ukiwamo.

Hatua hizo ni pamoja na kuiita Tanzania kuzungumza kwani msimamo wa serikali ni kwamba haiwezi kuburuzwa kuingia katika Shirikisho la Afrika Mashariki.

“Msimamo wetu hatuwezi kugawa ardhi yetu, hatuwezi kuwa waangaliaji, hivyo vingezo vyote wanataka tuvitake,’ alisema na kuongeza:

“Wala wasingepata shida yote hii, tungekutana kwenye kikao tukatoa kibali wakaendelea na utaratibu na sisi tukarudi tukaendelee na utaratibu wetu wa mwendo wa pole.”

Membe alisema katika kufikiwa kwa Shirikisho la Afrika Mashariki kuna hatua kadhaa za kufuata, moja ni soko la pamoja, ushuru wa forodha, sarafu moja na mwisho shirikisho la kisiasa.

“Hadi sasa bado tunahangaika na hatua hizi za awali, hatujaweza hata kufikia sarafu moja, sasa wenzetu wanataka shirikisho la kisiasa,” alisema Membe na kuongeza:
“Mimi sioni hata hiyo monitory union (sarafu moja) ikifikiwa sasa hivi. Sisi bado tunaikataa.”

Alifafanua kuwa hata Waingereza wakati Umoja wa Ulaya wanakiunga kwenye sarafu ya Euro wao walibaki na sarafu yao, na mpaka sasa wanaendelea nayo. Hivi karibuni Tanzania imeonekana kuwekwa kando na nchi nyingine nne kati ya tano zinazounda EAC.

Tayari marais wa nchi hizo, Kagame, Museveni, Uhuru Kenyatta wa Kenya na Pierre Nkurunzinza wa Burundi wamekwisha kufikia makubaliano ya kuanzisha mchakato wa kuandikwa kwa Rasimu ya Katiba ya Shirikisho la Kisiasa la nchi wanachama wa EAC, bila kuishirikisha Tanzania.

Waziri wa Serikali za Mitaa wa Rwanda, James Musoni, amekaririwa na vyombo vya habari vya nchi hiyo akieleza kuwa makubaliano ya kuanzishwa kwa mchakato wa kuandikwa kwa Rasimu ya Katiba ya Shirikisho la Afrika Mashariki, yalifikiwa Septemba 12 mwaka huu, mjini Kampala na marais wa Rwanda, Kenya na Uganda na hivi karibuni Rais wa Burundi ambaye alialikwa katika mkutano huo na kushindwa kuhudhuria, naye sasa amethibitisha ushirika wake katika shirikisho hilo jipya.

Tayari nchi za Kenya, Uganda na Rwanda zimeshaanzisha mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Kenya hadi Rwanda.


Vile vile Bandari ya Mombasa nchini Kenya imeshafanyiwa upanuzi kuruhusu nchi za Uganda na Rwanda kupitisha mizigo yao.

Kufuatia hali hiyo ,Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, hivi karibuni alisema licha ya hatua zinazochukuliwa na nchi wanachama wa EAC za kuitenga Tanzania katika baadhi ya mambo, itabakia na msimamo wake na haitakubaliana kuingia kwenye Shirikisho la Kisiasa huku masuala ya ushuru wa forodha, soko la pamoja na sarafu moja, hayajatengamaa.

Waziri Sitta pia alieleza kuwa Tanzania imeiandikia barua sekretarieti ya baraza la mawaziri wa nchi wanachama wa EAC, ikilalamikia baadhi ya mambo yanayoendeshwa kwa usiri na baadhi ya nchi wanachama.

Kikao kingine cha viongozi wa nchi hizo kinatarajia kufanyika mwishoni mwa mwezi huu jijini Kigali, Rwanda bila kuishirikisha Tanzania.

Tanzania,Tanzania nchi yangu nakupenda kwa moyo wote na nitakupenda daima,hongera sana waziri kwa msimamo mkali katika mambo yaliyowekewa rangi nyekundu na mimi naongeza mengine kama ifuatavyo:-
  • Tanganyika na Zanzibar zimeungana toka mwaka 1964 lakini swala la ardhi na maliasili za Zanzibar ni haki ya wazanzibari iweje leo tuungane na Afrika mashariki ardhi iwe suala la muungano?
  • Kabla ya mwaka 1977 tulikuwa na shirikisho lenye nguvu na kabla ya hapo miaka ya 1968 tulikuwa tunatumia sarafu moja yaani ya Kenya na uganda ziliweza kutumika Tanzania na ya Tanzania katika nchi hizo,Jumuiya ilipovunjika kwa sababu za wakenya nakumbuka nilikuwa shule ya msingi ilituumiza sana hasa sisi tuliokuwa karibu na mipaka ya Kenya(namkumbuka yule waziri wa mambo ya nchi za nje wa Kenya wakati huo alikuwa anaitwa Charles Njonjo alitunyanyapaa kabisa) sisi tulipata hasara kubwa sana kiasi hata masurufu ya wastaafu wa hilo shirika tulishindwa kulipa hadi hii leo,na kufukuzwa watanzania kama mbwa katika hizo nchi hivi haya ni ya kusahau?
  • Vita na Uganda ilituacha hoi bin taaban kila kitu kilikuwa cha kulangua hata sabuni haikuwa inauzwa dukani hata sigara zilililanguliwa hakuna msaada wowote tulioupata kwa hawa majirani zetu sasa eti wanataka tuungane tena kisiasa, kwa lipi jema walilotufanyia?.
  • Wakati wa vita vya ukombozi kusini mwa Afrika hawa walikuwa wanatubeza sana na kutuwekea vikwazo katika maendeleo yetu vya kila aina leo Tanzania tumeungana na wale tuliowapigania(SADC) wanatubeza tulipokuwa tunaangamia kwa vita walikuwa wapi?(Bravo Hashim Mbita)
  • Watanzania tulitengwa kidiplomasia kiasi cha kuvunja uhusiano na mataifa ya magharibi wakati huo Marekani,ujerumani ya magharibi uingereza na nyinginezo hawa alikuwa wanachekelea,hivi sasa uhusiano umerudi baada ya kutuelewa msimamo wetu thabiti hadi kututembelea na kuahidi uwekezaji mkubwa kwao imekuwa kero na gubu mioyoni kwao jiulize kwa kawaida ukiwa na marafiki kama hawa utafanyaje?.
  • Huyu Museveni aliingia Uganda kwa msaada mkubwa sana wa Tanzania tena baada ya kuishi hapa nchini miaka kibao hata huyo Kabila wa DRC aliishi na kusomea hapa kasoro huyo Kagame hata huyo Kagame kuingia jumuiya haizidi miaka 2 leo amekuwa ndiyo kinara wa kuhujumu wenzake Tanzania tukitaka kusaidia DRC nao watulie kama wao wanatoa vitisho vya kila aina, jiulize ukiwa na marafiki wa aina hii we utafanyaje?.
  • Ukisafiri katika hizi nchi ukasikia jinsi wanavyotubeza huwezi kuvumilia hata kidogo,tena kwa hivi sasa tumepata gesi na mafuta ndiyo kabisaa hawajafurahi hivi mbona wao wanayo mafuta na wameanza kuchimba watanzania hatuwaonei wivu kama wanavyoonesha wivu wa wazi ketu?
  • Kenya wamefaidika na madini ya Tanzania hasa Tanzanite hadi kununua ndege kubwa ya abiria na kuiita Tanzanite hiyo Tanzanite inapatikana Kenya?.
  • Wamepora rasilimali za Tanzania kutokana na awali kuwa hoi kabisa,hadi kusema Kilimanjaro,serengeti,Ngorongoro na vivutio vingi vyetu viko kwao hao watalii sasa wamejua ukweli kuwa viko Tanzania na wameanza kuja mojakwa moja TZ bila kupitia Kenya inawauma sasa wanataka kuja kwa staili nyingine ya kutaka ushirikiano uhusishe Ardhi yetu hee tumeshajua janja ya nyani haiwezekani kabisaaa bora kuachana nao tuendelee na wenzetu wa moyoni Zambia Msumbiji na Afrika kusini.
 
Hivi ni CCM au serikali imeifanyia nini ardhi kuwainua watanzania au wewe mtanzania umefanyia nini ardhi iliyoko bwerere Tanzania kukuinua.Ulishasikia serikali au CCM inalimia watu ardhi na kuwagawia mazao?.Ardhi iko bwerere ni kazi yako sasa wewe kuamua uitumiaje.Hata CHADEMA ikija haitakulimia shamba kuinua maisha yako. Utaendelea kuimba wimbo wa magamba hadi uende kaburini lofa wa kutupwa.

Hatima ya maisha yako haiko mikononi mwa CCM wala CHADEMA iko mikononi mwako utajijua.Wewe endelea kuimba nyimbo za chama hapo utakufa lofa shauri yako.

Big like bob...
 
Kwani muungano wa tanzania una ridhaa ya wananchi wake?huwa nawashangaa watanganyika wametolewa eac wanalalamika mbona z'br ikitaka kujitoa kwenye muungao inakuwa nongwa?kama tanganyika mmetolewa kwenye eac basi iachieni zanzbr huru ijiunge.

Inakuwa nongwa kwa sababu kama watanzania tumeshawekeza sana katika utanzania wetu. Hivyo, wanzazibar wakitaka kujitenga ina maanisha utaifa wetu umegwe kidogo. Kwa upande wa EAC bado hatujaingia huko sana na ndiyo maana siyo nongwa ki hivyo. sasa wewe fikiria kama wangetufanyia haya wakati tumeshaingia katika sarafu moja, rais mmoja, ushuru wa forodha mmoja, jeshi moja na labda bunge moja si ingekuwa ni patashika??
 
Msimamo wangu bado ni ule ule kwamba tanzania hatuna mwamko wa dhati na huu mradi wa EAC integration na kwa kiasi kikubwa sana, nchi yetu ndio sababu kwanini mchakato wa integration umekuwa unasua sua; Huu ndio ukweli wenyewe, hata kama ni mchungu namna gani; Ni muhimu tufanye maamuzi magumu sasa kwamba je, are we in or out, instead of sitting on the fence;


Kauli na vitendo vyetu vimetawaliwa Zaidi na woga and defensiveness kuliko engagement katika mchakato husika kwa hali ya kujiamini; Kuna mifano kadhaa ya kuthibitisha haya, na inashangaza sana kwanini bunge letu ambalo sasa linatajwa kuwa na mamlaka ya kufanya maamuzi muhimu juu ya suala husika, bunge hili limekuwa kimya kujadili au kufanyia maamuzi kama haya:

1. Mwezi februari mwaka jana (2012), Tanzania ilifunga mpaka wake na kenye (maeneo ya Taveta) ghafla tu, baada ya madereva wa malori kugoma kupinga uamuzi wa Tanzania kutoza $200 kwa magari kutoka Kenya; Uamuzi wa Tanzania ulikuwa ni kinyume na common market protocol ambayo lengo lake ni kupunguza vikwazo vya biashara within the EAC block; Je, nani aliwajibishwa kwa violation hii ya CMP pamoja na hasara zilizojitokeza? Je, bunge au serikali zilishughulikia suala hili rationally? Majibu ya wengi yatakuwa ni ya kisiasa Zaidi;

2. Mwezi May mwaka juzi (2011), serikali ya Tanzania ilipiga marufuku usafirishaji wa mazao ya nafaka kwenda nje ya nchi (ikiwa ni pamoja mipakani na fellows EAC members) kwa hoja kwamba such trade was unregulated, ambayo ilipelekea uhaba wa chakula na mfumuko wa bei; Uamuzi huu ulitokea katika kipindi ambacho wakulima wa mazao ya nafaka walikuwa hawana soko la uhakika (kwa kawaida, tani nyingi za mahindi mikoa ya nyanda za juu kusini huwa zinaozea tu kwenye maghala kutokana aidha kwa kukosekana kwa soko au ulafi wa wafanyabiashara wa kihindi kubania mahindi so as to create artificial shortages ili wapate faida kubwa baadae); pia uamuzi huu wa serikali ulikuja katika kipindi ambacho wenzetu wa kenya walikuwa katika food crisis & famine kwenye maeneo kadhaa ya nchi yao; Uamuzi wa serikali yetu haukutuma a positive vibe kwa wanachama wengine wa EAC; Je, bunge lilishughulikia suala hili? Was it done rationally? Hata katika hili, majibu ya wengi yatakuwa ni ya kisiasa Zaidi;

3. Mwaka huo huo wa 2011, mahakama kuu ya Tanzania iliingilia kati kesi iliyofunguliwa na East African Development Bank dhidi ya kampuni ya kifisadi ya Tanzania (Blueline) ambayo ilifiadi Zaidi ya $130 million na kutishia kuifilisi EADB; kwanini Tanzania tuliamua kuwa obstructionist wa haki hii ya EADB? Kwa faida ya nani? Je, bunge lilichukua hatua gani kunusuru benki hii pamoja na kulinda interest za Tanzania na za nchi wanachama? Majibu mengi pia katika hili yatakuwa ni ya kishabiki na kisiasa Zaidi kuliko mantiki;

4. Mwezi November 2011, kwenye Bujumbura summit, Tanzania ilikataa kutia sahihi makubaliano juu ya establishment of the EAC political federation & mutual defense pact; hoja ya Tanzania dhidi ya political federation ilikuwa kwamba suala la ardhi lisihusishwe; Pia, tulikataa kutia sahihi makubaliano juu ya mutual defensive pact kwa hoja kwamba tungeweza kujikuta tukiingia katika vita kutokana tu na irresponsible leaders katika nchi wanachama; Hoja dhidi ya mutual defensive pact ina mashiko, lakini suala la ardhi kidogo kuna mashaka – hivi tunafahamu jinsi gani wageni kutoka nje (wazungu na waarabu na wachina) wanavyozidi kukamata maelfu ya heka za ardhi ya watanzania? Kwanini tunatetea wananchi wa Tanzania kinafiki? Kwanini hatuoni tatizo la wageni (wazungu, waarabu, wahindi) kuhodhi maelfu ya hekari za ardhi tena bila kushirikisha wananchi lakini suala la raia wa wenzetu wa EAC ndio tunaona ni tatizo? Kwanini hatuogopi raia wa nje ya afrika kuchukua ardhi lakini tunaogopa raia wanachama wa EAC? Je ina maana hatukuliona hili tatizo huko nyuma na tulikosa fursa za kuwaandaa wananchi kupitia effective policies za kuangalia maslahi ya watanzania juu ya suala la ardhi ili waingie katika federation wakiwa wamejiandaa? Katika hili, pia majibu ya wengi katika hili yatajaa siasa na ushabiki kuliko mantiki;

cc Mimibaba candid Scope timbilimu
Mchambuzi,

..naomba nichangie kidogo kuhusu hoja zako hapa.

..kwanza suala hili lilishaletwa kwa wananchi kupitia Tume ya Prof.Wangwe. wa-Tz walizungumza kwa uhuru kabisa kwamba hawataki masuala ya ARDHI pamoja na FEDERATION.

..zaidi, badala ya watu kushughulika na chanzo cha concerns za wa-Tanzania kuhusu ardhi yao, wengi wameishia kuwatukana au kuwabeza. lazima tujiulize kwanini wananchi wa kawaida huku Tanzania hawataki ardhi iwe ya shirikisho? zaidi, ardhi kuwa ya shirikisho kutakuwa na maslahi gani kwa wa-Tanzania?

..tukija kwenye suala la federation, lets be honest here kwamba hawa majirani zetu hawavutii kuwa nao ktk shirikisho. hatuwezi kuunda political federation wakati kuna sentiments za nationalism. sidhani kama majirani zetu wako tayari kuachana na utaifa wao na kutengeneza mazingira ya wana-EAC kuishi kama taifa moja, au shirikisho. zaidi, hatuwezi kuwa na shirikisho wakati majirani ambao wameonyesha waziwazi kwamba wanawabagua na kuwadharau wa-Tanzania. kama huamini hilo fuatilia media za Kenya, Uganda, na Rwanda.

..Jambo lingine linalokwamisha hiyo integration nadhani ni kukosa uaminifu baina ya nchi wanachama. Kuna baadhi ya nchi wanachama zimetanguliza competition badala ya cooperation. Binafsi nadhani competition haitakiwa kuwa kati ya nchi wanachama, au kati ya wananchi wa nchi moja dhidi ya nyingine, badala yake competition inatakiwa iwe kati ya east africans na outside world. Kwasababu tumetanguliza competition matokeo yake ndiyo haya ya malumbano, mifarakano, na mistrust, baina ya wananchi wa kawaida wa nchi wanachama wa EAC.

..Jumuiya hii imefika mahali inaendeshwa kwa mtindo wa "sandakalawe amina, mwenye kupata apate, mwenye kukosa akose." Kwa mfano kumekuwepo malalamiko kwamba huku Tanzania, ajira zinachukuliwa na wa-Kenya. Je, malalamiko hayo yameshughulikiwa vipi at EAC secretariat level, and at government level. Je, hatua zilizochukuliwa so far, zinafanana na hatua ambazo mataifa mengine yamechukua/huchukua kushughulika matatizo ya namna hiyo ktk jamii zao?

..Mwisho na mimi naomba nikupe mifano ya mambo ambayo wa-Tanzania wamefanyiwa lakini hayaendani na spirit ya integration.

1. Kenya iliwahi kuzuai maua ya Tanzania yasisafirishwe kupitia Nairobi.

2.Rwanda kupandisha ghafla ushuru wa barabara huku waki-target wasafirishaji wa-Tanzania.

3.Wanachama wenzetu kuendelea kulazimisha masuala ya ardhi wakati mjadala wa suala hilo ulishafungwa. wa-Tanzania wanapinga ugawaji holela wa ardhi yao kwa wageni toka ndani na nje ya Jumuiya. Watu wa nje wanaweza kupata ardhi huku Tanzania kupitia sheria zetu za uwekezaji, na kwa msaada wa Tanzania Investment Center. Je, kwanini majirani zetu wanakwazwa na utaratibu huo?

4.Kenya kupinga application ya Tanzania kuuza shehena yake ya pembe za ndovu. Wakati huohuo wanatarajia tuwasaidie ktk mgogoro wao wa kujitakia na ICC.

5. Matukio ya mamlaka za Kenya kuwapora mifugo wafanyabiashara wa Tanzania waopelekea mifugo yao ktk minada ya Kenya.

6. Uganda na Kenya kuweka vikwazo katika majadiliano ya kuanzishwa kwa monetary union. pamoja na ukweli huo hatukuona media ya Tanzania ikizishambulia nchi hizo.

7. Kulazimishwa kwa EAC mutual defense pact bila kuzingatia kwamba Tanzania ina mkataba wa aina hiyo kupitia SADC, na Uganda na Rwanda, kwa nyakati mbalimbali zimeivamia DRC ambayo ni mwanachama mwenza wa Tanzania ktk SADC.

NB:

..Kwa mtizamo wangu, kwa kuzingatia mazingira yetu, model ya ushirikiano inayotufaa ni ile ya NAFTA. Hii model ya EU tunayojaribu kuifuata sidhani kama inatufaa na inaeleke kukwama.

cc Candid Scope, Geza Ulole
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom