Dr Adam Francis
JF-Expert Member
- Aug 12, 2011
- 773
- 1,301
Ninawaza kwa sauti, hivi ni kweli kabisa Rais Samia atakuwa hajamnunia Rais Ruto kwa kuchepusha uwekezaji wa refinery kutoka Tanga kwenda Lamu?
Nasema hivi kwakuwa mazingira ya namna mradi huu ulipotangazwa kwa mara ya kwanza kuwa utatekelezwa Tanga, ni kama kulikuwa na consensus baina ya Tanzania, Kenya na Uganda.
Mabadiliko yaliyofanywa na mwekezaji, Dangote pamoja na Rais Ruto kupeleka mradi Lamu, yameibua mgawanyiko wa dhahiri; Uganda wamesema wao wataendelea na mradi wao wa refinery yao wakati huo watashirikiana na Tanzania kwenye mradi wa Tanga. Wanachama wengine wa EAC kama Rwanda wao wameshathibitisha kushiriki uwekezaji wa Dangote.
Swali linabaki, kama sisi tu watanzania wakawaida tumenuna kwa Rais Ruto kutupiga chenga ya mwili kuchepusha mradi huu kutoka Tanga kwenda Lamu, vipi kwa Rais wetu? Ingawa kidoplomasia tunapeana mikono, kwa jambo kubwa kama hili lenye maslahi makubwa ya nchi, ni wazi litaleta hisia hasi haswa katika ustawi wa mashirikiano yetu katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.