Mimi nadhani huyu jamaa ni tishio la Lowasa, RA, Mudhihiri, na mafisadi wengine wanoona kwamba ana nafasi ya kuukwaa ukuu wa nchi na hiyo ikitotekea wamekwisha!! Kama sio tishio lao wala hasingekuwa anajadiliwa, na kadri tunavyomjadili ndivyo tunavyompandisha!!
Uongo, fitina, na uzushi zote ni kete za good politicians. Leteni hoja mzito against this man, if any.
I think JK ana kila sababu za kujivunia kwa Membe; unfortunately JK hasikii ushauri na ni mwoga wa kivuli chake. So far Membe ni miongoni mwa mawaziri wachache sana ambao sio waoga wa kuongea na wandishi wa habari na kuwapa msimamo wa serikali na kuacha wananchi wamchambue kadri wapendavyo. Mwenyewe JK hili limemshinda, matokeo yake Membe anakazi ngumu ya kuongelea hata mambo ambayo hayako kwenye wizara yake na kujaribu kuu cover uozo na mapungufu ya JK.
Nimemsikia Membe akiongea radioni several times, the guy can speak what he thinks is right na sio mwoga kutoa msimamo wa serikali, hata kama wananchi wataukataa. To the contrary nikamsikia Pinda akilialia bila kutoa msimamo wa serikali, nimemsikia Pinda akiwa kama analyst badala ya kutoa msimamo wa serikali. Nikamsikia JK, yeye hana flow ya thoughts na wakati mwingine nilitamani nimwekee maneno kinywani mwake mana anakigugumizi cha mawazo.