Akiwa Rais 2015, mie nitakuwa Waziri wa Mambo ya Nje..
Hana huo ubavu kwa kuwa tutakutana Dodoma wakati huo!
Hizo kwake ni ndoto za mchana, hafai, kwa maana kalba hata ya kugomea ameanza majungu!
Akiwa Rais 2015, mie nitakuwa Waziri wa Mambo ya Nje..
Unamaanisha nini unaposema Membe hamuwezi Mudhihiri? Binafsi sijasikia Membe akitangaza kutaka kugombea urais 2015 lakini kwavile watu wanahisi ana uwezo huo ndio maana wanaamua ku-conclude!! Hivi ndivyo mwanadamu alivyo!!! Mtu akiwa na cha kuringia basi hata asiporinga, waungwana watasema anaringa kwavile wanajua anacho cha kuringia!!lol !!! Mimi natoka Jimbo la Mudhihiri, na ni jirani na Jimbo la Membe!! Jimbo la Membe lina maendeleo makubwa kuliko la Mudhihiri na mengi aliyafanya wakati akiwa mbunge tu, sasa unaposema Membe hamuwezi Mudhihiri ni kwa lipi wakati wanatakiwa kupimwa kazi zao majimboni kwao kwavile wote ni wabunge?! Jambo moja ndilo ambalo Mudhihiri anamzidi Membe, nalo ni USWAHILI, wakati Membe sio mtu wa kuchonga kama alivyo Mudhihiri!!Ndio Mudhihiri kawa Mbunge miaka 14!! Ndio justification ya kuonesha ubora wake? Unaonaje ukitaja mafanikio aliyowapatia wapiga kura wake katika kipindi chote hicho? Mbona KImbau alikaa Mafia kwa zaidi ya miaka 20? Ni bora? Kawaulize watu wa mafia wenyewe watakuambia na ndio maana hata alipotokea Buji (Abdulkarim Shah Mafia), akachukua jimbo kiulaini. Kinachombeba Mudhihiri ni kwamba hamna competitive politician jimboni mwake na ndio maana alivyotokea mama wa watondoa akaanza kutapata!! na ndio maana hata uncle wangu alipojaribu kuwasaidia wanakijiji wenzake akazani anataka ubunge wakati yeye na siasa tofauti!!
Mambo mengine unachekesha!! Hivi tangu lini Mbunge akapimwa na shouting za bungeni? Ingekuwa kuongea bungeni ni kigezo basi Mafia ya Kimbau na Newala ya Nandonde zingekuwa kama Newyork!! Usitaje maswali aliyouliza bungeni, taja mambo aliyofanya jimboni!
MgonjwaUkimwi,
Mkuu, habari ya Mwikalo kushindwa maisha Canada sii kweli, alikuwa na kazi nzuri tu..Jamaa alihamia US kwa sababu alipata ajira yenye cheo na fedha zaidi..... mabo kwneda juu mkuu wangu..
Kilchotangulia, Mwikalo ndiye aliyepeleka Idea ya kwanza kufungua mtandao Zanzibar - Tanzania.. wajanja wakamzunguka ndipo akanawa mikono na kuhamia US..
Nimekusikia Mkandara,
Wewe kaa na data zako na mimi nakaa na data zangu juu ya Mwikalo. Nikiendelea kuteremsha data za Mwikalo nitakuwa simtendei haki JF kwani yeye mwenyewe ni member wa JF na Tanzanet kadhalika, na ana watu wake hapa JF. Kwa hiyo mimi natuliza boli, ili tuendelee na mada. Nitahitimisha tu kwa kurudia kwamba Mwikalo ninayemfahamu mimi hana ubavu wa kufadhili kampeni za Membe.
Nikirudi kwa Mudhihir, Mbunge wa Mchinga naona kachanganyikiwa baada ya kupata mkono wa chuma. Hana point juu ya ujenzi wa kiwanda cha saruji Lindi mjini ambako sio jimbo lake wala jimbo la Membe. Mji wa Lindi unakaribia kuitwa kijiji, waalimu na waganga wanaukimbia, njaa haijaacha kutesa, kila mkuu wa mkoa wa Lindi ameshindwa kabisa kuufufua mji wa Lindi. Leo hii Membe anafanikiwa kuleta kiwanda cha saruji kitakachoinua uchumi, Mudhihir anataka kijengwe nje ya Lindi mjini na hivyo kuua kabisa matumaini ya kufanya mji wa Lindi uwe manicipal.
Kwa taarifa sio kiwanda cha saruji tu kitakachojengwa Lindi mjini, bali hoteli ya kitalii na kiwanda cha kubangua korosho. Haya yote ni mafaninikio ambayo hakuna mbunge yeyote aliyethubutu kuyaleta mjini Lindi isipokuwa mbunge wa Mtama (sio Lindi mjini) Membe, utashangaa kazi ya mbunge wa Lindi Mjini.
Membe akiwa mbunge tu na sio uwaziri, kajenga clinics kwenye jimbo lake, na amekuwa mbunge wa kwanza katika mkoa wa Lindi kujenga ofisi ya bunge yenye wafanyakazi wapatao 25 wanaolipwa kwa fedha ya mshahara wake. Ni mbunge wa kwanza kusambaza ambulances kwenye jimbo lake ili kuokoa maisha ya akina mama wanaozaa na kupoteza vichanga. Ni mbunge wa kwanza kupongezwa na wafadhili kwa matumizi halali ya misaada ya wafadhili.
Ni mbunge wa kwanza kupeleka jopo la wapiga kura wake 15 (bila kujali vyama vyao) kwa fedha yake Dodoma bungeni kusikiliza bunge na kujifunza namna bunge linavyotunga sheria. Hapa tunapoongea vijiji takriba 10 vya jimbo la Mudhihir vimetoa maombi serikalini vikiomba vijiunge jimbo la Membe ili vinufaike na maendeleo yasiyo yakibaguzi yanayoloetwa na Membe.
Mudhihir amefanya nini katika jimbo la mchinga? Alikuwa mbunge wa kwanza kushikwa ugoni hadi akakatwa mkono. Amekuwa mbunge wa kwanza kuanzisha bendi ya muziki (Mchinga sound?)ambayo tayari imemshinda. Amekuwa mbunge wa kwanza kumfanya mgombea urais wa tiketi ya ccm kupata chini ya asilimia 3 za kura zote, na kulazimisha CCM iibe kura kunusuru aibu.
Nitasisitiza kwamba Mdhihir kachanganyikiwa mana anaona mwisho wa ubunge wake. Anatumiwa na wabaya wa JK wanaoona kwamba Membe ni royal kwa kikwete na kwamba ana asilimia kubwa ya kuwa rais. Jimbo la Mdhihir na Lindi Mjini watafurahi kupata mbunge kama Membe.
Mikoa ya kusini imekuwa marginalized sio tu na central government bali na wabunge wa mfano wa Mudhihir, Magani, Majogo, Kitende, nk. Wakati umefika kwa mikoa hii kupata wabunge wanaojali wapiga kura wao, wabunge wa mfano wa Membe.
Membe ana haki ya kugombea uraisi, na ni wananchi tu ndio watakao amua kama anafaa au lah. Wananchi hao ni zaidi ya Kanda2, MgonjwaUkwimwi, Mkandara, na ni zaidi ya JF. JF tunaweza kumwona hafai wananchi wakaona vinginevyo, na kinyume chake.
Kwa mtazamo wangu, Membe hatagombea urais 2015 kwa sababu kashatimiza ndoto zake za kuleta mafanikio katika jimbo na mkoa wake. Uwaziri wa mambo ya nje kwa Membe ndio kikomo cha ambitions zake kisiasa. Kuwakilisha nchi yake katika mataifa mengine ndio urais wa Membe, sio kutawala nchi. Kama Membe atagombea urais basi ni kwa maombi ya wananchi na si matakwa yake. Haya ni mawazo yangu.
MgonjwaUkimwi,
Mkuu majungu siyawezi kama una taarifa zake nzito kaa nazo nilichoandika mimi ni kukosoa pale nilipoona umekosea kwani najua fika niliyoyaandika - Mwikalo tulikuwa naye hapa, (wakati nikiwa Ottawa) hivyo unaweza kufahamu mengi lakini sidhani kama ulikuwa karibu naye kwani ningekufahamu. Zaidi ya hapo sina, chonga ukipenda!
kuhusiana na MEMBE bila shaka niko nawe kwa sababu CCM leo hii hakuna mtu ambaye binafsi naweza kumfikiria kiti cha Urais baada ya JK kwa sababu lugha ni ile ile..Watu kama Mwakyembe, mama Kilango na wengineo ni maadui wa chama, hawabebeki wala kutamanika,, hivyo sijui nani kabakia huko?
wewe jamaa Muongo na mjivuni kama Membe a.k.a MBOPO.MAENDELEO gani kayaleta Membe? kwani kuna mbunge ambaye hajapeleka AMBULANCE jimboni kwake?
Ndesamburo kila miezi sita anapeleka AMBULANCE jimboni wako wengi Martha Mrata SIO mbunge wa kuchaguliwa lakini kapeleka Singida AMBULANCE,madawa,computer n.k wewe kupeleka Ambulance alizokuombea Mwikalo kwa vyama vya hisani Marekani unataka kujipa credit? hebu nenda Mufindi kwa MUNGAI, Musoma vijijini kwa MKONO,Isimani kwa LUKUVI uone nini maana ya kupeleka maendeleo kwa watu wako.
wewe jamaa muongo sana juu umesema kuwa MEMBE ni waziri masikini kuliko wote kwenye baraza la JK, nikakuuliza MEMBE ni masikini mbele ya CELINA KOMBANI,Balozi IDD SEIF,KAPUYA,NSANZUNGWAKO,KAPUYA,WASSIRA?
hivi sasa umsema kuwa MEMBE kwenye mshahara wake anawalipa wafanyakazi 25 aliowaajiri yeye binafsi,kima cha chini ni shilingi laki moja na kitu,hawa ni wafanyakazi wa kati hivyo tuseme kila mmoja anampa mshahara wa laki tatu na nusu kwa wafanyakazi 25 ni karibu milioni 10,jee Membe ana mshahara wa zaidi ya milioni kumi?kwani ana mahitaji yake binafsi sio kulipa wafanyakazi wa bunge waliopo Mtama TU.
huyu ndiye uliyesema kuwa ni waziri masikini hata kama hivyo umezua maswali mengi pesa hizi anapata wapi kama sio fisadi? au wafanya kazi hawa wanalipwa na Malinzi?
Rais MWENYEWE anapata mshahara kama milioni tatu vipi MEMBE awe na mshahara zaidi ya milioni kumi?
nakumbuka Zitto KABWE aliwahi kusema humu humu kuwa kuwalipa wafanyakazi yaani PA wao ni kazi kubwa yeye anamlipa mfanyakazi wake kama laki tano kama sikosei,vipi Membe amudu wafanyakazi 25 toka mfukoni mwake?
Fanikio lingine ni kuwa Membe alipeleka watu 15 ambao umesema ni wapiga kura wake,mstari unaofuatia ukasema kuwa toka vyama mbali mbali,sasa kama wanatoka vyama mbali mbali hawawezi kuwa wapiga kura wake watapigia vyama walivyonavyo.
hivi kuwapeleka watu Bungeni ni fanikio?MUSSA AZZAN ZUNGU mbunge wa ILALA kila mara anapeleka wanafunzi wa shule mbalimbali bungeni sio watu 15 WA Membe ndani ya miaka 9 alikuyokaa bungeni.
MUDHIHIR sio mbunge wa kwanza kushikwa ugoni na hakukatwa mkono kilichotokea ni ajali ya gari kila mtu anajua.Kwani Membe kama ni mtakatifu angezaa na mama wa kizungu Canada na kumtelekeza?angempa nyumba mbunge kijana msichana aliye bungeni wakati si mke wake wala ndugu yake?.
Mudhihir hakuwahi kutoa asilimia tatu hayo ndio majungu tunayompiga vita Membe KILA SIKU.
YEYE MEMBE kama ni mfanisi kwenye kamati ya Mtandao kwa uchaguzi wa 2005 HAKUWAHI kuwa Mwenyekiti wa kamati,Mwenyekiti alikuwa Lowassa na makamu wake ni LUCAS SELELII, yeye alipewa nafasi ndogo tu ya kupitia magazeti yanasema nini chini ya uenyekiti wa Salva Rwemamu na DR.shoo.sasa anataka kujitia kuwa yeye ndiye alikuwa kila kitu kwenye Mtandao wakati kazi imefanywa na LOWASSA na Selelii na wengine wengi sioni sababu ya kuwataja hapa.MEMBE inakuwaje wewe msomi unakuwa chini ya SELELII kama bosi wako kwenye timu ya Mtandao wakati Selelii ana elimu ya darasa la saba au form four.
kujipendekeza na kuleta uchonganishi ni hapa unaposema kuwa Mudhihir anatumiwa na wabaya wa JK sio kweli unataka upate support ya JK kwenye ugomvi wako na Mudhihir.
unasema Kwa vile Membe ni Royal kwa JK sio kweli mtu Royal kwa JK ni KAPUYA hawa ndio walisababisha kura nyingi zitoke mikoa ya Tabora hadi Bukoba kwenye mkutano mkuu wa kumpa mgombea ndani ya CCM, kama ni Royal asingemzunguuka jk kwenye suala la OIC kwa JK kasema vingine halafu nyuma ya pazia kaenda kukutana na KARDINAR PENGO kumwambia kuwa maaskofu watie presha kulipinga suala hilo,
baada ya kuwapanga maaskofu akarudi tena kwa sura nyingine kuwa suala hili litashughulikiwa kwa njia nyingine wakati ni yeye aliyemzunguuka JK kwa maaskofu.
Eti kila kijiji kinataka kiwe jimbo la MEMBE kwa maendeleo,kama MEMBE anapendwa asingesababisha mdogo wake afukuzwe kazi mamlaka ya Airport kwa kuchelewa kurudi kazi kwa kuhangaika jimboni kumsaidia MEMBE uchaguzi 2005 na hatimaye huyo mdogo wake amepewa ukuu wa wilaya katika mkoa mmoja wa mwambao.kama jimboni kwake kahangaika ndio unasema ana nafasi kuwa ya kuwa rais 2015?
maendeleo ajenge mashule, apeleke vijana vyuo vikuu, kifupi aende KARATU,ROMBO,MWANGA,SAME,MUFINDI,ISIMANI,MUSOMA VIJIJINI akaone wabunge wa maeneo hayo walivyokuwa watu wa vitendo na si porojo za kupeleka watu 15 ndani ya miaka tisa bungeni kuwa ni maendeleo.