Shutuma ulizompelekea Membe hazijaanza leo. Ni shutuma ambazo hutolewa na maadui zake kisiasa, ambao nitawataja kwa majina na nafasi zao wanazoshika ktk jamii, nitafanya hivyo tu pale utakaponiambia, Membe anatishia vipi usalama wa nchi, na ni muongo vipi, alimdanganya nani, na lini?. Sijawahi kumsikia Membe akisema kwa mtu yeyote kuwa anautaka Urais mwaka 2010, lakini napenda kukufahamisha kuwa hakuna dhambi yeyote kwake kugombea nafasi hiyo, kama ilivyo kwa Mtanzania yeyote. Tatizo hapa ni kuwa kuna watu wamejipanga kuutaka Urais, na wanaona kuwa mwanaume huyu ni kikwazo kwao, wanaanza kutafuta kila namna ya kumchafua.