Membe: Hatutawaomba radhi Rwanda

Membe: Hatutawaomba radhi Rwanda

kabila ni weak na ana jeshi weak sana...mbona jk hamchokozi museveni na inajulikana wanasaidia vita drc...leave alone RWanda jk hana ubavu wa kufanya mediation..madagascar wamepoteza muda weeeee mwisho wa siku kale ka dj kamesema kanagombea na wasimchanganye haiwahusu yeye kuwa rais....

Kigogo....hapa suala si kumchokoza mtu, maanake huu sio mchezo wa kitoto wa kuputa watu wazichape! Kama nilivyokwambia hapo juu hii ni strategic move ya kuondosha balaa la vita katika nchi tunazopakana. Adha ya wakimbizi kutoka Congo sisi ndio tunaozijua, adha ya wakimbizi toka Burundi sisi ndio tulihangaika nazo, adha ya wakimbizi toka Rwanda sisi ndio tulihangaika nazo. Sasa suala la Burundi lilikwisha kwa msaada wa Tanzania na nchi marafiki baada ya lile jeshi la kabila moja kukubali mazungumzo na waasi kuanzia CNDD-FDD and FNL. Sasa Kagame hataki mazungumzo na waasi halafu anaweka proxy forces kule Congo. Hilo kimkakati halikubaliki.....!
 
Mbona hawaambii Marekani wapatane na ALQAEDA????????????
Au awaambie Nigeria Wapatane na Boko Haramu????????????????

Kwani hufahamu kuwa Marekani na serikali ya Afghanistan wana mazungumzo na Taliban....! Hufahamu kuwa Pakistan inafanya mazungumzo na kundi la marehemu Beitullah Mehsud....!
 
Kwani hufahamu kuwa Marekani na serikali ya Afghanistan wana mazungumzo na Taliban....! Hufahamu kuwa Pakistan inafanya mazungumzo na kundi la marehemu Beitullah Mehsud....!
JK ndo mshauri ama????
 
Mi nashindwa kuelewa Kikwete ana maslahi gani na vita ya Kongo hadi kujiingiza kwenye migongano ambayo ni totally BASELESS. Au ndio ule uvumi kuwa Riziwani anataka kuingia kwenye biashara ya almasi na mbao za Kongo?

Membe na Kikwete wanaweza kuwa wanatafuta sifa kwa kuwa watu wengi wanapenda siasa za KI_GANGWE lakini kidiplomasia haiiweki nchi yetu pazuri. Huku Chini Malawi mgogoro hawajautatua, then wanatafuta ugomvi wa KUNUNUA na Rwanda, hatujui kesho itakuwa nani??

Mind you Tanzania ndio nchi yenye uchumi dhaifu na maendeleo duni kwa sasa kwenye ukanda wa Afrika mashariki huku bajeti yake ikiwa tegemezi kwa asilimia 41. Kwa uchumi huu wa hospitali hazina dawa na akina mama wanalala wanne wanapojifungua hatuna haja ya kutafuta migogoro na majirani. FDLR hawatuhusu sisi watanzania na ni matatizo ya ndani ya Rwanda kwa nini tujihusishe?? Je siku Kagame akiibuka na kumshauri Kikwete aende walau kutoa POLE kwa mjane wa Mwangosi, Kikwete atafurahi?? Mbona Membe na CCM yake hawajakaa kwa majadiliano na watu wa Mtwara kuhusu matumizi ya gesi but wanataka majadiliano kwenye nchi za watu?? Wajanja tumenusa kitu hapo...

Pale DRC kuna makampuni ya Kimataifa kutoka Marekani,na mataifa makubwa ukipeleka jeshi katika nchi ambayo USA inamaslahi NCHI YAKO INALIPWA PESA na Serikali ya marekani.Na tumepeleka majeshi haraka ndani ya DRC,ili Rais wa Obama akifika Tanzania tumwambie,sasa tupatie fedha ya kusaidia kutuliza vita ndani ya DRC.

Unacheza na usanii wa Kibongo,lazima Obama achomolewe pesa.!!!!!
 
Hakuna kuomba Radhi.Naunga mkono msimamo wa serikali ya Tanzania.Pia ili kuepusha haya huko baadae Serikali ya Tanzania ifanye mazungumzo na vikundi vya Uamsho
 
Mkuu hii ni large strategic plan....sio Tanzania tu! Vita ya Congo SADC imeshasema basi, tuwaonee huruma waafrika wenzetu wanaokufa bila hatia. Imefika wakati tuwe na Congo yenye amani ili majirani zake nao wapumzike. Kwa sasa amani ya Congo inasumbuliwa na Rwanda tu na vinginevyo....! Political will imeshapatikana.....lakini Rwanda hawataki wanang'ania vita kwanza kwa kisingizio cha FDLR na pili kwa kuanzisha proxy forces in Congo ambazo siku zote zina-destablise Congo. Sasa wakuu wamesema 'imetosha' ni muda wa kusoma alama za nyakati tu. One option ni kuwa na mazungumzo na FDLR na kuweka tume ya usuluhishi, kitu ambacho Kagame and inner circle hawakitaki. Sasa Kagame na genge lake aachwe aendelee kuuawa watu tu freely mpaka lini? Option ya pili ni kumng'oa Kagame kama individual na kuwa na mtu moderate ambaye atakubali suluhu ya kisiasa. Bahati mbaya option hiyo ni ngumu kwa sasa hata ukiandaa coup de tat still inabidi kuwa na back up army kwa vile inner circle ya Kagame inahusisha watu wengi. Kisa cha Gen. Kayumba Nyamwasa kukimbilia South Africa ni kutokana na option hiyo ya pili. Sasa option ya tatu iliyopo ni kuzibana hizo proxy forces zake, then baadae kubana b.u.m.b.u zake mpaka akubali suluhu ya kisiasa...!
Asante sana mkuu, kuna mijitu humu sijui ni mitusi au ni uelewa mdogo kwamba Tanzania isijiingize katika mambo ambayo hayaihusu. Kama ni mtanzania basi ana uwezo kufikiri mdogo sana. Utulivu wa Congo ni kitu muhimu kwa Tanzania, haitapokea wakimbizi ambao wanaleta tamaduni ambazo ni hatarishi kwa Tanzania, silaha na ujambazi, magonjwa, kufekwa misitu nk. Mtu mwenye mawazo hayo aende kigoma, biharamuro nk ataona athari nilizozitaja. Mimi namsupport Kikwete kwa asilimia mia.
 
pale drc kuna makampuni ya kimataifa kutoka marekani,na mataifa makubwa ukipeleka jeshi katika nchi ambayo usa inamaslahi nchi yako inalipwa pesa na serikali ya marekani.na tumepeleka majeshi haraka ndani ya drc,ili rais wa obama akifika tanzania tumwambie,sasa tupatie fedha ya kusaidia kutuliza vita ndani ya drc.

Unacheza na usanii wa kibongo,lazima obama achomolewe pesa.!!!!!

hizi ni propaganda chafu za watusi na m 23 ! Siku zenu zinahesabika.
 
asante sana mkuu, kuna mijitu humu sijui ni mitusi au ni uelewa mdogo kwamba tanzania isijiingize katika mambo ambayo hayaihusu. Kama ni mtanzania basi ana uwezo kufikiri mdogo sana. Utulivu wa congo ni kitu muhimu kwa tanzania, haitapokea wakimbizi ambao wanaleta tamaduni ambazo ni hatarishi kwa tanzania, silaha na ujambazi, magonjwa, kufekwa misitu nk. Mtu mwenye mawazo hayo aende kigoma, biharamuro nk ataona athari nilizozitaja. Mimi namsupport kikwete kwa asilimia mia.

nafarijika sana ninapogundua kuna watanzania tunaloliona hili! Hatutakata tamaaa mpaka vibaraka kama kagame wakose pa kutokea.
 
Hizo ndio sera zetu za nje?
Nikuingilia sovereignity ya nchi nyingine ambayo tunapaswa kuomba radhi.
Kama Membe ataendelea kung`ang`ania kutoomba radhi,then Rwanda watatangaza mgogoro na sisi kitu ambacho kitashusha hadhi ya nchi yetu kimataifa.
Tuwe wepesi wa kukiri makosa sio ngangari hata kwa vitu ambavyo tumekosea.
 
wenje kauliza toka lini rais kikwete akawa msemaji wa fdlr, tunasubiri jibu kwa membe.

wanja sijui wenje....ndio yule matusi man? Kweli chadema chama cha fujo...hivi mpaka rais akipendekeza amani kwa jirani mnapinga wakati hapa tulipokea wakimbizi wa rwanda zaida ya 3,000,000 wakasababisha matatizo chungu mbovu...leo rais anapendekeza njianzuri ya kupatanza kuacha vita...chadema wana dhihaki hatua ya kikwete...
Mheshimiwa zitto hakika ni pekee yake mwenye upeo chadema nzima wengine...ni wapo tu .....siasa za maji machafu
 
Napongeza msimamo wa serikali. Na anayesema kwamba JK aombe radhi, huyo mtu hajitambui kwanini yeye ni mtanzania na hana uelewa mpana wa mambo. Sio mfuatiliaji wa siasa za maziwa makuu. Mambo ya PR za kusema kwamba eti Tanzania inaionea wivu Rwanda kwa maendeleo ni upumbavu mtupu. kama hakutakuwepo na m23 na FDLR then wao wanaona ndo mwisho wao wa uporaji wa mali Congo. Genocide waliyofanya kina Nkunda mbona haiongelewi na hao ni wanyarwanda. Kuna makaburi ya mass grave Congo. Walipoingia Congo waliingia kwenye makambi na kuua raia wa kihutu. Kagame hafai lazima athibitiwe. N nachukia sana wanaoleta siasa kwenye mambo ya utaifa.
Mkuu chukua tano, you are great thinker
 
Hizo ndio sera zetu za nje?
Nikuingilia sovereignity ya nchi nyingine ambayo tunapaswa kuomba radhi.
Kama Membe ataendelea kung`ang`ania kutoomba radhi,then Rwanda watatangaza mgogoro na sisi kitu ambacho kitashusha hadhi ya nchi yetu kimataifa.
Tuwe wepesi wa kukiri makosa sio ngangari hata kwa vitu ambavyo tumekosea.

Hata kama watatangaza mgogoro, so what? Tumia ubongo wako kufikiri Tanzania inapata athari kubwa sana kutokana na mgogoro wa Congo wewe nenda Kigoma utajua matatizo yaliyoletwa na wakimbizi. Tanzania imechoka kupokea wakimbizi wanaotokana na upuuzi wa Kagame
 
Kigogo....hapa suala si kumchokoza mtu, maanake huu sio mchezo wa kitoto wa kuputa watu wazichape! Kama nilivyokwambia hapo juu hii ni strategic move ya kuondosha balaa la vita katika nchi tunazopakana. Adha ya wakimbizi kutoka Congo sisi ndio tunaozijua, adha ya wakimbizi toka Burundi sisi ndio tulihangaika nazo, adha ya wakimbizi toka Rwanda sisi ndio tulihangaika nazo. Sasa suala la Burundi lilikwisha kwa msaada wa Tanzania na nchi marafiki baada ya lile jeshi la kabila moja kukubali mazungumzo na waasi kuanzia CNDD-FDD and FNL. Sasa Kagame hataki mazungumzo na waasi halafu anaweka proxy forces kule Congo. Hilo kimkakati halikubaliki.....!
Kikwetu unanikosha mno, kuna mijitu humu sijui ndo michora mazombie kwenye paper zao . Posting zao za kipuuzi kabisa
 
Back
Top Bottom