Membe: Hatutawaomba radhi Rwanda

Membe: Hatutawaomba radhi Rwanda

Baba yako akigombana na jirani huwezi kusimama upande wa jirani hata kama jana yake alimkwida mama yako. Lazima utakuwa upande wake. Ndicho kimefanyika hapa. Ni busara ya kawaida.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Kucha hizooo! Ohooo!

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Baba yako akigombana na jirani huwezi kusimama upande wa jirani hata kama jana yake alimkwida mama yako. Lazima utakuwa upande wake. Ndicho kimefanyika hapa. Ni busara ya kawaida.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums

Hapo sasa nimewaelewa kumbe ndicho mnachokifanya. Lakini mfano wako hauna mashiko baba si sawa na rais, kumbe ndo maana anafanya blanda mnamuangalia kwa sababu baba yenu. Baba anafananishwa na mfalme sio rais kaka.
 
Ushauri wa JK haukuwa mzuri huwezi kukaa meza moja na jambazi. Ila kwa yeye anaweza maana anakaa nao anakula nao wale wa EPA wa RADA wote anaishi nao. Rwanda are serious hawamchekei mtu na ndio maana wanaendelea. Watanzania watu wa ajabu sana eti leo wengi mnamtetea. Hivi kila siku mnamponda kwa maamuzi yake yasiyo na mashiko leo mnamtetea nini sasa? kachemsha kachemsha na hajawahi patia PERIOD !!
Kafulie huko, hivi nyinyi mnapotaka congo iongee na majambazi wa m23 mnafikiria nini? Eti mnajidai mmekomboa rwanda mmekomboa kutoka kwa nani? Kagame anaweza kulinganishwa na Samora? Wacheni upuuzi. Vita vyenu vya kugombea madaraka vimetuletea balaa nchini kwetu kwa kukosekana amani sehemu za magharabi nyinyi kwa kiburi chenu mnaona sawa tu. Genocide mmejitakia wenyewe kwa uroho wenu wa madaraka, tumewastahi vya kutosha lakini hamuelewi kwa kiburi chenu. Haya nendeni kaongeeni na hao ndugu zenu rwanda sio nyinyi peke yenu kwanza wao ndio wengi.
 
Hapo sasa nimewaelewa kumbe ndicho mnachokifanya. Lakini mfano wako hauna mashiko baba si sawa na rais, kumbe ndo maana anafanya blanda mnamuangalia kwa sababu baba yenu. Baba anafananishwa na mfalme sio rais kaka.

Wala hili sio suala la baba na jirani. Bali ni suala la busara ya Kikwete (Watanzania) na upumbuwazi wa Kagame. Baada ya miaka 19 ya kutumia maguvu Kagame bado haoni busara ya kubadilisha mbinu, hata pale anaposhauriwa. Hata wale watoto wote waliokuwa na miaka 18 mwaka 1994 hivi sasa wanakaribia miaka 40. Kwa hiyo FDLR kwa vyovyote vile hivi sasa sio jeshi la watu walioshiriki kwenye Genocide.
 
Huombi radhi huku unaomba usuluhisho. How ridiculous is this?
 
safi sana mh B membe,kidiplomasia alichofanya kikwete ilikuwa sahihi,Tanzania tunakuwa waadhirika sana wa matatizo ya Rwanda,Tunataka eneo lote la ukanda wa maziwa makuu liwe na amani,biashara zifanyike,maisha yaboreke na sio kila siku vita- vita tu watu hawalimi,shule zimefungwa,nyumba za ibada hakuna watu kisa hakuna amani,Mashariki ya congo balaa kisa kagame,umeshauriwa kaa na wenzako muongee mpatane kama ulikuwa utaki jibu ni raisi sema hapana aiwezekani na ndio maana ya ushauri.Tanzania chonde tusiombe radhi kama wanamwaga mboga ss tumwage ugali,Membe kwa hili tuaminishe kuwa wewe ni nyerere mpya katika diplomasia ya Afrika
 


this is coming from wenje???? one of those classless politicians waliojazana CDM anaongea upuuzi wowote kisa bunge lipo LIVE

Duuh! Mbona umewafagilia hivyo wanasiasa wa CDM? Classless inaweza ikawa na maada kuwa wao ni "down to earth" wasiokuwa na madaraja na wasiojiona kuwa wao ni zaidi ya wapiga kura wao. True politicians in deed.
 
Kama kweli Tanzania ni Taifa kubwa basi hatustahili kuomba radhi kwa Rwanda ila inatakiwa kumuonyesha Kagame na wanyarwanda wote kwamba Tz ni baba wa Uhuru ktk bara hili la Africa, kwahiyo inatakiwa kwanza kabisa awamu hii inakuwa ya mwisho kwa Kagame kuiongoza Rwanda na baada ya hapo tunahamia kwa M7.Nawaomba ccm wafanye mpango wa kuhakikisha kwamba mtu wao ambaye walimweka madarakani kule kenya nae anang'oka na ccm waache tabia ya kupigia debe chama rafiki bila kumtathimini mgombe wake, Kenyetta alishinda kwa msaada cm na leo hii Kenyetta yuleyule kaigeuka ccm na serikali yake.

00
 
Aitaka serikali ya Kagame ipatane na wapinzani badala ya kutumia mabavu.

Asisitiza Tanzania ipo tayari kuwapa ushirikiano kama ikiombwa.


Hakika tuwaombe radhi kwa lipi? Mtu akiwa na uchafu mgongoni ukamwambia "Ndugu yangu mgongoni kwako kuna kinyesi cha binadamu ulilala chale ukakilalia ulikuwa unafanya nini?" Badala ya kufikiria uchafu uliopo mgongoni anaanza kutafakari swali la "Ulikuwa unafanya nini" Siwezi kumwomba radhi mtu huyo, wacha abaki na kinyesi chake. Inzi watamuumbua kwa kumzonga.
 
Ndugu zangu pamoja na kuwa na uzalendo haina maana tushabikie hata mifarakano isiyo ya msingi. Ushauri wa Rais JK haukuwa mbaya ila hakutumia busara katika namna ya kuutoa kwa mhusika. Namheshimu sana Rais Kagame kwa uongozi madhubuti nchini Rwanda. Ana haki ya kukataa ushauri hasa hasa ushauri ule unapotolewa bila kuzingatia kiini cha mgogoro na kama wahusika wako tayari kuufanyia kazi. Siasa za Rwanda sio kama za Tanzania. Damu iliyomwagika Rwanda ni nyingi na hakuna pande isiyo na hatia (tofauti ni idadi ya vifo na muda uliotumika). Lazima tuelewe kuwa hao masalia wa FAR na Interahamwe bado wanahusika na kupanga na kuendeleza mashambulizi dhidi ya Rwanda mpaka leo.

Namuelewa Rais Kagame anapokasirishwa na hotuba na ushauri mwepesi uliotolewa na kiongozi (Rais Kikwete) hadharani kwa suala nyeti bila kutumia busara ya kwanza kumshauri kwa faragha. Wenzi wetu wa magharibi wanaita "cheap political rhetoric". Sisemi Rais Kagame hana mapungufu, la hasha. Nanena kuwa kusema vitu ni rahisi lakini unapokuwa kiongozi ni lazima utumie busara kabla hujatoa matamko ambayo yanaangukia kwenye hisia za watu. Rais Kagame anaongea kwa hisia kwani yaliyotokea nchini Rwanda yanamgusa kama kiongozi mkuu, mnya-Rwanda na vile vile (tuwe wakweli) kwa kuwa ni m-Tutsi. Ni wa-Tutsi na wa-Hutu waliowastaarabika ndio walikuwa wahanga wakuu wa mauaji siku zote milipuko ya mauaji inapotokea Rwanda. And so, I am not condoning President Kagame's reactionary approach but I understand...
 
Mi nashindwa kuelewa Kikwete ana maslahi gani na vita ya Kongo hadi kujiingiza kwenye migongano ambayo ni totally BASELESS. Au ndio ule uvumi kuwa Riziwani anataka kuingia kwenye biashara ya almasi na mbao za Kongo?

Membe na Kikwete wanaweza kuwa wanatafuta sifa kwa kuwa watu wengi wanapenda siasa za KI_GANGWE lakini kidiplomasia haiiweki nchi yetu pazuri. Huku Chini Malawi mgogoro hawajautatua, then wanatafuta ugomvi wa KUNUNUA na Rwanda, hatujui kesho itakuwa nani??

Mind you Tanzania ndio nchi yenye uchumi dhaifu na maendeleo duni kwa sasa kwenye ukanda wa Afrika mashariki huku bajeti yake ikiwa tegemezi kwa asilimia 41. Kwa uchumi huu wa hospitali hazina dawa na akina mama wanalala wanne wanapojifungua hatuna haja ya kutafuta migogoro na majirani. FDLR hawatuhusu sisi watanzania na ni matatizo ya ndani ya Rwanda kwa nini tujihusishe?? Je siku Kagame akiibuka na kumshauri Kikwete aende walau kutoa POLE kwa mjane wa Mwangosi, Kikwete atafurahi?? Mbona Membe na CCM yake hawajakaa kwa majadiliano na watu wa Mtwara kuhusu matumizi ya gesi but wanataka majadiliano kwenye nchi za watu?? Wajanja tumenusa kitu hapo...


kaka umetumwa na kagame nini? si mumeanza kwa kusema mama salma ni mhutu cousin wa hybarimana!! hahaaa inaonesha ufuatilii mambo, tz haifungamani na upande wpwote hiyo ndo sera ya mambo ya nje toka nyerere, tz ilipereka majeshi lebanon, darful, angola, msumbiji,comoro!! kote huko rizwan anataka madini lol myonge myongeni lakini hili!!
 
Hapa ndipo utakapogundua tofauti kati ya watanzania na wafuasi wa chadema. nashukuru mungu mimi ni mtanzania.
 
Anaiomba Rwanda ipatane na wapinzani na TZ iko tayari kutoa msaada wakati tumeshindwa kupatana na UKAWA? Au hao sio wapinzani? Aibu hii kujipambanua kwenye mambo usiyoweza kuyafanya?
 
Back
Top Bottom