Meditation in your daily routine

Meditation in your daily routine

Mara nyingi Meditation niifanyayo ni ile ya wakati wa kulala na uwa hivi:-
1.Nahakiksha sina kilevi chochote.

2.Naondoa mawazo yote hasa ya kifamilia, kazi,marafiki na aina yoyote ya usumbufu/furaha.
3.Najiuliza hasa mimi ni nani na nipo kwa ajiri ya Nini alafu ili iweje.
4.Nini nilichofanya kuanzia kulipopambszuka mpaka kiza kilipoingia.
5.Nini cha kufanya siku inayofuata na kwa nini nifanye alafu ili iweje.
Baada ya Kama nusu saa au saa nzima:-
1.Ni nani nimemkwaza na kwanini nilifanya/ilitokea vile na nini kilifanyika baada ya hapo.
2.Wapi nilipata furaha/faraja na Nini hasa kilisababisha na kwanini alafu ili iweje.
3.Nini matarajio yangu kwa familia na taifa.
4.Kwanini nahitajika/sihitajiki (Nini Umuhimu/Hasara) kwa binadamu wenzangu.
Baada hapo ni Kulala kunakoambatana na Sala/dua.
Meditation ya namna hii ni usaidia sana kujisahihisha/kuzidisha juhudi na kuongeza Itabidi Mahala pake Kazi pia uongeza marafiki/networks.
 
Mshana, Asante sana kwa mada nzuri katika kufundisha watu vitu vya muhimu.

Pia kuna website ambayo naisimamia katika kufundisha watu mada mbalimbali za kujitambua hasa meditation, yoga, spiritual awakening, elimu za kale ambazo zina siri kubwa, maisha, wisdom na kathalika. Nawakaribisha sana.

Ndugu ubarikiwe sana nimeingia humo nimejifunza mengi!
 
Meditation kwa kiswahili ni tahajudi, tahajudi maana yake ni mazoezi ya kiufahamu ya kufanya jambo moja kwa wakati mmoja kimawazo kifikra na kimatendo bila kuchanganya na jambo Lingine lolote kwa kuwaza kwa kunena na kwa kutenda
Ooooho asanteee kwa elimu ngoja niende playstore nikadownload meditation musics
 
eo ni siku ya kimataifa ya Yoga , Meditation au Tahajudi.

Siku hii imeadhimishwa kwa mazoezi ya Yoga kwenye fukwe za bahari ya Hindi eneo la Coco Beach ambapo mgeni rasmi ni Waziri wa Habari, Vijana , Sanaa na Utamaduni, Mhe. Nape Mnauye na kuhudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Darisalama, Paul Makonda.

Kwa wasio jua kuhusu Yoga, meditation au tahajudi karibuni pande hizi.
Psychic Powers: Ni Nguvu za Kufanya Miujiza. Wengi wanazo bila ...
Mafunzo ya Meditation Bure. Ni Kupitia Brahima Kumaris Meditation ...
Ni Leo Jioni Pale ...."Karibuni Njooni Tumediteti!" | JamiiForums ..
"Will Powers!", "Faith Healing!"-NgMiujiza Ya Uponyaji kwa Imani ...

Jifunze: Namna ya kufanya TAHAJUDI (Meditation)... | JamiiForums ...
Meditation (Tahajudi a.k.a Tafakuri Kina) | JamiiForums | The Home ...
Mwanzo wa meditation | JamiiForums | The Home of Great Thinkers
Je unataka kuishi maisha ya amani na utulivu? Fanya hivi ...
Meditation in your daily routine | JamiiForums | The Home of Great ...
Ushuhuda wa ukweli kuhusu meditation | JamiiForums | The Home of ..
Your Brain on Meditation | JamiiForums | The Home of Great Thinkers
Sitaki tena kupaa angani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers
Jinsi Ya Kupanga Na Kupangua Ubongo Ili Kutimiza Ndoto (Hypnosis ...
Sex huweza kutumika kama njia kufikia roho yako (sex is a gate way ...
Kwanini tunanaongelea sana watu tufanye meditation? | Page 2 ...
Washa Na Kuzima taa au mshumaa kwa nguvu ya fikra | P
Jinsi ya kutoka nje ya mwili (Astral Projection)
Faida Za Kimwili (Afya) Na Kiroho (Imani) Za Kufunga |

Kwanini tunanaongelea sana watu tufanye meditation?
Mawasiliano ya kiroho katika milango nane ya fahamu
Ni wakati wa kujitambua (Jua ulikotoka)
Kuna siri gani kwenye ulimwengu wa kiroho ukilala chali? | Page 7 ...


Mwana jf Mtambuzi ni mwana tahahajudi mkuu humu jukwaani. Wengine ni kina
mshana jr, MziziMkavu, Rakims na wengine wengi.

Karibuni tutafakari.

Pasco
Asante kwa hii
 
Mshana muda wa kukaa unaambiwa ukae mwili usiwe na maumivu sasa mbona style ya kukaa huku miguu imekunjwa ni lazma itauma na kupata ganzi, Hapo inakuaje?
Mwanzoni lazima upate maumivu ila kila ukipata maumivu pumzika
Pia punguza sana kula nyama
 
Mwanzoni lazima upate maumivu ila kila ukipata maumivu pumzika
Pia punguza sana kula nyama
Halafu kwenye meditation naona zinaandikwa faida tu, Je hasara zake ni zipi?
Kuna thread ya rakims nmesoma ukihisi kuchemka gonga kidole uache, ukihisi nini sijui gonga kidole uache, kidole unagongaje?Je ukisitisha tu ghafla nini kinatokea?
Na ukipata mshituko katikati ya kumeditate haiwezi kukuathiri? Kudisturb mind?
 
Halafu kwenye meditation naona zinaandikwa faida tu, Je hasara zake ni zipi?
Kuna thread ya rakims nmesoma ukihisi kuchemka gonga kidole uache, ukihisi nini sijui gonga kidole uache, kidole unagongaje?Je ukisitisha tu ghafla nini kinatokea?
Na ukipata mshituko katikati ya kumeditate haiwezi kukuathiri? Kudisturb mind?
Binafsi sijawahi kuona hasara za meditation, kwenye kugonga kidole Kwakweli sijui vizuri
Mengine yote hakuna shida kwakuwa meditation ni tendo la hiari
 
Kwanza mniwie radhi nitachanganya lugha kiingereza na kiswahili
Pili post yaweza kuwa ndefu tuvumiliane lakini nitajitahidi kuifupisha

Wanaforum tumekuwa na masomo mengi mazuri juu ya meditation hasa toka kwa Pasco Mtambuzi heshima kuu kwao na ndugu yetu Rakims
Ni masomo ambayo kwa kiasi kikubwa yaliwanufaisha wengi lakini bahati mbaya sana tulipitiwa na kudhani kuwa wote wako kwenye ile level moja nasi ya uelewa hivyo masomo mengi yakawa in deep na kiufundi zaidi bila kuelewa kuwa wasomaji wengine walihitaji kwenda nao kuanzia chini kabisa

Meditation bado ni kitu kigeni kwenye familia zetu na kwa kiasi kikubwa inahusishwa na nguvu za giza hasa kutokana na mapokeo yetu kwenye mambo kama hayo, hivyo ni vigumu mno kuwa na meditation huru uwapo nyumbani mtaani au kazini, lakini bado kukiwa na uhitaji mkubwa wa hiki kitu hasa kwa wale ambao tayari wana upeo na uelewa fulani wa meditation
Fuatana nami katika mada hii ambayo kwa njia mojawapo yaweza kukupa nafasi ya kufanya basics za meditation bila bughudha

1.Time management n discipline
Tengeneza utaratibu wa kufanya jambo moja kwa muda ule ule at least mara 5 kwa wiki! Yaani kwa mfano lazima uamke saa 12 kamili asubuhi, moja kamili lazima uwe uko njiani kwenda kazini saba kamili lunch mbili kamili dinner na saa nne kamili unapanda kitandani (huu ni mfano tu)

2.lishe na kinywaji
Hakikisha unakua na kipimo kisichobadilika kwenye chakula kuanzia asubuhi mpaka usiku, maji pekeyake ndio unaweza kunywa mengi bila kipimo maalum
chakula ni kwa ajili ya afya ya mwili na si ladha ya mdomoni hivyo usiongeze kipimo kwa ile ladha upendayo na kupunguza kipimo kwa chakula usichokipenda

3.Jambo moja kwa wakati mmoja chochote ufanyacho na muda hata wa dk tano ukipata jaribu kumakinika na kufanya breathing meditation au counting breath meditation kimya kabisa.

Kama unadrive concentrate kwenye driving kama uko kwenye usafiri wa jumuiya kaa kimya na kuwa mtulivu ukiendelea na meditation yako usihamaki kuhusu foleni nk mwachie dereva hiyo headache

Haya yaweza kuwa rahisi kuyasoma lakini practice ikawa ngumu lakini msingi wa meditation huanzia huku
Weza kuji control kwenye muda Weza kuji control kwenye lishe na Weza kuji control kwenye kufanya jambo moja kwa wakati mmoja baada ya hapo tutapeana hatua inayofuata
Asante
 
Back
Top Bottom