Meditation in your daily routine

Meditation in your daily routine

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
365,944
Reaction score
845,955
Kwanza mniwie radhi nitachanganya lugha kiingereza na kiswahili
Pili post yaweza kuwa ndefu tuvumiliane lakini nitajitahidi kuifupisha

Wanaforum tumekuwa na masomo mengi mazuri juu ya meditation hasa toka kwa Pasco Mtambuzi heshima kuu kwao na ndugu yetu Rakims
Ni masomo ambayo kwa kiasi kikubwa yaliwanufaisha wengi lakini bahati mbaya sana tulipitiwa na kudhani kuwa wote wako kwenye ile level moja nasi ya uelewa hivyo masomo mengi yakawa in deep na kiufundi zaidi bila kuelewa kuwa wasomaji wengine walihitaji kwenda nao kuanzia chini kabisa

Meditation bado ni kitu kigeni kwenye familia zetu na kwa kiasi kikubwa inahusishwa na nguvu za giza hasa kutokana na mapokeo yetu kwenye mambo kama hayo, hivyo ni vigumu mno kuwa na meditation huru uwapo nyumbani mtaani au kazini, lakini bado kukiwa na uhitaji mkubwa wa hiki kitu hasa kwa wale ambao tayari wana upeo na uelewa fulani wa meditation
Fuatana nami katika mada hii ambayo kwa njia mojawapo yaweza kukupa nafasi ya kufanya basics za meditation bila bughudha

1.Time management n discipline
Tengeneza utaratibu wa kufanya jambo moja kwa muda ule ule at least mara 5 kwa wiki! Yaani kwa mfano lazima uamke saa 12 kamili asubuhi, moja kamili lazima uwe uko njiani kwenda kazini saba kamili lunch mbili kamili dinner na saa nne kamili unapanda kitandani (huu ni mfano tu)

2.lishe na kinywaji
Hakikisha unakua na kipimo kisichobadilika kwenye chakula kuanzia asubuhi mpaka usiku, maji pekeyake ndio unaweza kunywa mengi bila kipimo maalum
chakula ni kwa ajili ya afya ya mwili na si ladha ya mdomoni hivyo usiongeze kipimo kwa ile ladha upendayo na kupunguza kipimo kwa chakula usichokipenda

3.Jambo moja kwa wakati mmoja chochote ufanyacho na muda hata wa dk tano ukipata jaribu kumakinika na kufanya breathing meditation au counting breath meditation kimya kabisa.

Kama unadrive concentrate kwenye driving kama uko kwenye usafiri wa jumuiya kaa kimya na kuwa mtulivu ukiendelea na meditation yako usihamaki kuhusu foleni nk mwachie dereva hiyo headache

Haya yaweza kuwa rahisi kuyasoma lakini practice ikawa ngumu lakini msingi wa meditation huanzia huku
Weza kuji control kwenye muda Weza kuji control kwenye lishe na Weza kuji control kwenye kufanya jambo moja kwa wakati mmoja baada ya hapo tutapeana hatua inayofuata
 
Mkuu mshana jr kwa wale wageni wa hii kitu hebu tuweke vizuri,hivi kuna chakula au vinywaji ambavyo havitakiwi kwa mtu anaejifunza meditation?
 
Vipo epuka vyakula vya makopo epuka kula nyama sasa epuka kula vyakula vya mafuta mengi epuka kula mikalangizo na mapochopocho epuka vileo juice za dukani na soda

ASUBUHI kula vizuri si lazima ushibe lakini hakikisha kina virutubisho vingi muhimu

MCHANA kula ushibe si lazima ule vizuri lakini chochote ambacho kitajaza tumbo

USIKU kula kidogo au chakula chepesi kwa kuwa unaenda kupumzika

Kumbuka kuwa na kipimo kile kile na muda ule ule kwa kila mlo
Pendelea vyakula vya kuchemsha zaidi na vilivyo fresh matunda kwa wingi pia ni mazuri
 
Mshana, Asante sana kwa mada nzuri katika kufundisha watu vitu vya muhimu.

Pia kuna website ambayo naisimamia katika kufundisha watu mada mbalimbali za kujitambua hasa meditation, yoga, spiritual awakening, elimu za kale ambazo zina siri kubwa, maisha, wisdom na kathalika. Nawakaribisha sana.

Poa Apollo nineshachungulia huko tayari na ku LIKE
 
Last edited by a moderator:
Huyo Rakim hapo juu hatari sana. Anajua sana hii elimu ya meditation lakini nasikia ni tapeli. Tunakuomba kaka mshana jr utuelekeze hapa kwa weledi na usawa. Natanguliza shukrani za dhati kwa niaba ya wenye hamu ya kujifunza
 
Last edited by a moderator:
Meditation ni mchakato unaotaka ustahimilivu mwingi sana na kwa changamoto za maisha tulizo nazo leo hii wengi hushindwa na kuishia kusoma makala nyingi nzuri sana bila kufanya kwa vitendo, lakini naamini tukifundishana vile vitu rahisi kwanza na mtu akaamua kuvitendea kazi basi tunaweza kufaulu kwa kiwango fulani
 
Huyo Rakim hapo juu hatari sana. Anajua sana hii elimu ya meditation lakini nasikia ni tapeli. Tunakuomba kaka mshana jr utuelekeze hapa kwa weledi na usawa. Natanguliza shukrani za dhati kwa niaba ya wenye hamu ya kujifunza

Binadamu Ni Aina Ya Roho Iliyoumbwa Na Yule Aliekamilika Kwa Kila Kitu... Roho Hii Ilipoumbwa Haikuachwa Wazi Hivi hiviBali Ilibumbwa Kwa Madongo Na Kuchanganywa Kwa Sayansi ya hali ya juu ambayo haikuwekwa ubongoni mwa Dongo Lile... Dongo Hili Liliumbwa Kwa Maji Maji Machafu Yenye Harufu Ambalo Ni Dongo Linalokuwa Na Kukomaa Kila Baada Ya Muda Liliokadiriwa.... Nisiende Mbali Sana Maana Uzi Umeanzishwa Na M/jamii Anaenitambua Kama Tapeli Pia Umekuwa Commented Na Mtu Aliemezeshwa Imani Ya Kuwa Rakims Ni Tapeli....

Niseme Hivi Rakims Si Tapeli Rakims Ni Kama Wewe Na Ni Kiumbe Mfano Wa Gari Ikiishiwa Betri Basi Itazima...

Ningeweka Point Nzuri Hapa Ninaitambua Lakini IT GONNA BE POINTLESS.. maana hawatasoma Comment Watasoma Username:

hawataquote Comment, wataquote USERNAME;

Teach Them... Mtakatifu Perfect Man... mshana jr

Rakims
 
Rakims you know exactly what happened between me and you and heavens knows too, lets keep it off JF for the sake of the forum.....!!!
 
We All do mistakes but when someone realized that he was passing through hard times and had not forget what he is done and going to collect it dat isnt mistake that is called unlimited thinking if i were someone who you think i am, were i bn using this username?? like what others do i were did it too...
but i am who i am, and it will always be me....
japo kuwa mnatumia fake username na avatars haiwabadilishi u are still you...

"Rakims"
 
Last edited by a moderator:
mshana, asante sana kwa mada nzuri katika kufundisha watu vitu vya muhimu.

Pia kuna website ambayo naisimamia katika kufundisha watu mada mbalimbali za kujitambua hasa meditation, yoga, spiritual awakening, elimu za kale ambazo zina siri kubwa, maisha, wisdom na kathalika. Nawakaribisha sana.

mkuu appolo mungu na akuzidishie kwa uamuzi wa kupeana huduma kama hizi.nakiri mimi ni mmoja wa watu waliokua na giza kuhusu mambo haya.

Big up kwa makamanda wenzako akina mshana jr, mkuu ramkins,pasco na wengine woote.mungu awazidishie na msichoke jamani asanteni sana

long live jamii forum
 
Binadamu Ni Aina Ya Roho Iliyoumbwa Na Yule Aliekamilika Kwa Kila Kitu... Roho Hii Ilipoumbwa Haikuachwa Wazi Hivi hiviBali Ilibumbwa Kwa Madongo Na Kuchanganywa Kwa Sayansi ya hali ya juu ambayo haikuwekwa ubongoni mwa Dongo Lile... Dongo Hili Liliumbwa Kwa Maji Maji Machafu Yenye Harufu Ambalo Ni Dongo Linalokuwa Na Kukomaa Kila Baada Ya Muda Liliokadiriwa.... Nisiende Mbali Sana Maana Uzi Umeanzishwa Na M/jamii Anaenitambua Kama Tapeli Pia Umekuwa Commented Na Mtu Aliemezeshwa Imani Ya Kuwa Rakims Ni Tapeli....

Niseme Hivi Rakims Si Tapeli Rakims Ni Kama Wewe Na Ni Kiumbe Mfano Wa Gari Ikiishiwa Betri Basi Itazima...

Ningeweka Point Nzuri Hapa Ninaitambua Lakini IT GONNA BE POINTLESS.. maana hawatasoma Comment Watasoma Username:

hawataquote Comment, wataquote USERNAME;

Teach Them... Mtakatifu Perfect Man... mshana jr

Rakims

Hahahahaha jamaa unajaribu kijisafisha wewe lakini wapi, watu ndio tushakujua kuwa we ni mwizi tuu hata uongee nn
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom