Media za Tanzania zinaweza kufa kipindi hiki cha miaka mitano ya CCM

Allency

JF-Expert Member
Jan 27, 2011
7,622
2,000
Kwa sasa zimeshakufa binafsi sikumbuki mara ya mwisho nilinunua gazeti lini,kwa sasa labda tutayanunua kufungia maandazi na kuwapa watoto kujaladia madaftari,hata tv channels wengi hatuangalii kabisa wala kuzisikiliza huwa naangalia channels za kenya na nje pamoja na za michezo,cartoon na wild animals,siwezi kupoteza muda wangu kuangalia channels za ndani...

Mkuu angalia basi hata TBC1 uone walivyotekeleza kwa kishindo
 

LOTH HEMA

JF-Expert Member
Dec 6, 2015
5,347
2,000
Kifo cha media nyingi kisitazamwe kwa mtazamo mfupi,automatically kitaua fani na umahiri wa waandishi,hasa habari za uchunguzi.Magazeti mengi yanapokufa hupunguza ajira nyingi za watu,huondoa ujuzi na ubunifu wa kazi za uandishi,kazi za uchapishaji usambazaji na uuzaji,athari zake ni kubwa kwa jamii
 

big IQ

JF-Expert Member
Dec 16, 2012
445
1,000
Masanja anasherehekea ongezeko kubwa la followers kwenye Instagram yake kwa kipindi cha miezi mitatu relate these to your post
 

LOTH HEMA

JF-Expert Member
Dec 6, 2015
5,347
2,000
Haya mambo ya kisiasa ni ya hovyo sana,siasa huinua na pia siasa hushusha,hapa ni haiba na utashi tu wa mtawala aliyeko madarakani.Kuua media moja kunaharibu mfumo wa ajira za familia nyingi pamoja na vipaji vya waandishi na wachoraji,pia kuna makampuni ya uchapaji kukosa kazi na mapato kupungua.Viwanda vya makaratasi ya kuchapia kukosa wateja.Wanasiasa wanabomoa wakifikiri wanajenga
 

Mnyapesimeka

JF-Expert Member
Jan 31, 2018
7,874
2,000
Mimi nilipenda kusoma vitabu kupitia gazeti la raia mwema la jenerali ulimwengu kupitia kusoma vitabu nilipata bahati ya kwenda mpaka ulaya miaka sita Leo hii magazeti ya Aina ile hayapo naona habari za kuisifu CCM tu huu ni ujinga wa taifa upuuzi wa kiwango Cha mwisho na haina tija kwa taifa kabisa.
 

Mnyapesimeka

JF-Expert Member
Jan 31, 2018
7,874
2,000
Imagine taifa ambalo gvt inafunga mtandao kisa tu vyombo vya usalama vinadhibiti matakwa ya mtu mmoja tu Kati ya watu milioni 60 hili ni taifa la kipumbavu kwa viwango vyote vya ulimwenguni imagine mtandao unaleta kipata Cha watu milioni tano kwenye taifa halafu unaufunga ili kibaba kimoja chenye watoto Kama sisi tukipe mamlaka ya kutuongoza aisee miaka kumi ijayo mliofunga mtandao Leo mtajidharau Sana kukaona kababa hako kamezeeka maisha c milele acheni watu wafurahie nchi Yao msitutese kwa jinai zenu.
 

FIKRA HAI

JF-Expert Member
May 22, 2013
229
225
Hivi kwanini tupo hivi? Kwani miaka yote iliyopita Chama gani kiliongoza? Hakuwa na vyombo vya habari? Binafsi natamani sana tulete Hoja zenye kujenga kuliko ujinga huu!
 

Gatekalii

JF-Expert Member
Nov 5, 2016
286
500
Nazipa pole media za Tanzania hasa zile zisizopokea ruzuku ya serikali zinaweza kufa kibudu.

Sababu hivi nani atanunua magazeti ya kusifu na kuabudu ayasome sasa hivi.

Kama mlipigwa pini mitano iliyopita na mkaona sawa mkidhani adui yenu ni Lissu basi andikeni mmeumia maana ukosoaji kwasasa hautavumiliwa.

Pili kipindi Cha bunge kilileta mvuto sana kwahiyo vigazeti vyenu viliuzauza kipindi cha bunge kwasasa andikeni mmeumia maana ile kamati kuu ya CCM pale bungeni yenyewe ni ndioooooooo. Wakikosoa kwa makelele na hoja kuntu Kama za kina Lissu basi watakuwa wanaigiza.

Nazipa pole media za bongo hasa magazeti kwa JamiiForums sina shaka itaendelea kung'aa kwasababu ya nature yake ambayo ni user-generated content.

Media zilizomsifia Magu kifo chenu kipo km 2 toka hapa tulipo.
Jipe pole wewe
 

Mnyapesimeka

JF-Expert Member
Jan 31, 2018
7,874
2,000
Kielelezo Cha ujinga hapa tz utakipata kwa wafuasi wa chadema na wafuasi wa lisu.
Wanaojaribu kupunguza nguvu za watesi wa taifa mnawaona wabaya wakati hawana hata mbwa wa polisi subirini dola ikose mtu wa kuwakemea mtamtafuta mbowe hamtamuona mtatamani kupindua serikali. Waliofikiria kuwe na mfumo wa multi partism sio wajinga ila kwakuwa mnajenga mfumo utakaoumiza watoto wetu sote wenu na wetu haina shida acha maisha yaendelee.
 

Gatekalii

JF-Expert Member
Nov 5, 2016
286
500
Wanaojaribu kupunguza nguvu za watesi wa taifa mnawaona wabaya wakati hawana hata mbwa wa polisi subirini dola ikose mtu wa kuwakemea mtamtafuta mbowe hamtamuona mtatamani kupindua serikali. Waliofikiria kuwe na mfumo wa multi partism sio wajinga ila kwakuwa mnajenga mfumo utakaoumiza watoto wetu sote wenu na wetu haina shida acha maisha yaendelee.
Yote haya unayanena kwasababu kura hazikutosha upande wa chadema, laiti Kama zingetosha Wala usingesema
 

binti kiziwi

JF-Expert Member
Aug 4, 2014
4,643
2,000
Zife tu wakose kazi na mitaji ife, walidhani watakufa CDM tu? Tutajifunza siku nyingine kuwaza madhara ya tunayoyashabikia in the long run.
 

124 Ali

JF-Expert Member
Apr 25, 2010
7,694
2,000
Watanzania wengi sana wanahitaji magazeti mfano Kampuni zinazotafuta na kutangaza tenda watu wanaopotelewa na nyaraka muhimu kama hati zanyumba paspoti na vyeti wanatangaza magazetini wanafunzi waliomaliza masomo wanaotafuta ajira huduma za mahakama matangazo ya sammons ya kuitwa mahakamani nk taarifa muhimu kutoka serikali kila chombo cha habari kina umuhimu kama sio kwako ni kwa watu wengine.
Hayo unayo yasema sio habarinya kila siku
 

Mkare

JF-Expert Member
Dec 21, 2010
504
225
Sasa hapo unazungumzia media house, sijui kwa hawa media workers 'waandishi' maana press zina_freez na kualikwa hakupo vile waaandishi wengi wanavyojichukua na hawapendi kujiongeza na field nyingine, dadadeki!.
Watafungua Youtube Channels
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom