Media za Tanzania zinaweza kufa kipindi hiki cha miaka mitano ya CCM

Sio zinaweza kufa zimeshaanza kufa zipo kwenye sakaratulmauti,hazijitambui zinafanya nini ila tunaowasikiiza tunajua kuwa hawa wapo katika kukata roho.
 
Watafungua Youtube Channels
Bila kupita TRCA na 1m hawatoboi halafu...%kubwa ya hao watu wanaopenda kujiita waandishi wa habari wengi wao wamezoea kuajiriwa hawana uwezo wakusimama wenyewe! niambie Mtu kama TIDO na exposure yake kaishia kuwa Mkurugenzi anaechaguliwa cha kurusha hewani
 
Mimi nitanunua tu kwani kuna vitu muhimu kama matangazo ya tenders matangazo ya kupotelewa vitu, hati za watu kuitwa kwenye mashauri nafasi za kazi matoleo maalumu taarifa za kibenki kila robo mwaka nk bila kusahau kusoma nyota

Vyote ulivyoorodhesha vinapatikana mtandaoni bila taabu au unaweza kulipa 500 kwa muuza magazeti na ukapitia habari zote unazozitaka then ukasepa
 
Wakaulize gazeti la uhuru lina wateja kiasi gani?Msimu huu wao na uhuru hawana tofauti!
Mzalendo gazeti bado lipo? Kwa ujumla hakuna uhuru wa habari Tanzania. Hata taarifa kwenye tv hazina mvuto. Ugomvi wa wataka kuendelea kuangalia tamthilia au mpira na wanaotaka taarfa ya habari haupo tena.
 
Back
Top Bottom