Katika uchaguzi wa mwaka 2005, nilibahatika kupanga foleni kwenye kupiga kura na ndugu mmoja jirani yangu mtaani (alikuwa amenipita mbali sana kiumri yaani mzee), aliniuliza unampa nani kura yako ya ubunge, nilimwambia kwa hilo ni siri yangu siwezi ivujisha, alicheka kiasi kisha akaniambia, "haya kijana we jifanye unajua sheria, lakini naomba ufahamu kuwa kwa jinsi kampeni zilivyokuwa zinaenda ilionekana wazi kabisa kuwa akili ya mgombea mmoja wa chadema ni sawa na wagombea 5 wa chama kikongwe, so make your better choice!'' nilicheka lakini nilifikiri kwa wepesi sana na nikamwambia mzee sasa unataka kuzeeka vibaya, Leo hii namkumbuka yule mzee (tayari ni marehemu) kwa maneno yake... naona kuwa alikuwa sahihi na hakumaanisha tu wabunge, bali pia hata washabiki na wapenzi wa chama hicho, uwezo wa kujenga hoja za msingi hakuna wanabaki kwenye machapisho ya khanga na taarab. Ndugu yangu tumia akili ya chekechea kabisa kama ya msingi huna, mbowe akapunguze mishahara by now, kama nani?