Mdahalo kati ya Freeman Mbowe na Hamad Rashid ITV

Mdahalo kati ya Freeman Mbowe na Hamad Rashid ITV

Ndugu wana jamvi hili Tukufu,
Jana nilkuwa naangalia Luninga na hususan ITV. kipindi live kilikuwa ni Mdahalo kati ya Mbowe na Hamad. Kilichonisikitisha na Hadhira iliyohudhuria. Hawakuwa na discipline! Sasa je ni uchanga wa kuendesha na kuhudhuria midahalo au ni ushabiki? maana midahalo kama ile ushabiki upo lakini basi uwe na kiasi. Maana ilikaribia ngumi!!!! it was a shame!! mpaka ITV kwa busara wakaamua kukatisha matangazo mpaka pale hali ilipotulia. Je what kind of A lesson tumepata pale kama kweli tunataka sauti zetu zisikike? hata kama mnatofautiana mitazamo use arguments sio ushabiki usio na mipaka as if it was a campaign ya kutafuta mshindi!! Jamani WATANZANIA TUBADILIKE NA TUWE WASTAARABU MAANA NEXT TIME WATU WANAWEZA KUDHANIA MIDAHALO HAINA MAANA. Tuache utamaduni wa kutumia hoja ya nguvu na hisia kufikisha ujumbe badala tutumie nguvu ya hoja. Ni VEMA KWA WANDAAJI WAWE WANATOA ELIMU KWA HADIRA INAYOHUDHRIA KABLA YA KUANZA KURUSHA LIVE Its embarasing. Sijui wenzangu mnasemaje kuhusu hilo. Jamii forums as great Thinkers what do we suggest?
 
Kinachonifurahisha kwenye mjadala huu ni kuwa watu hawa hawa waliokuwa wanawapigia kelele CCM kukimbia midahalo leo wanaitaka CHADEMA nayo ikimbie mdahalo!

MWANZO WA KUISHIWA mara nyingi unakuwa namna hii!

Huu mdahalo ulitayarishwa kwa madhumuni ya kuishindilia msumari CUF na Chadema walitayarisha watu wengi kujaza ukumbi ili kumzomea Mh. Hamad Rashid. Fortunately, CUF walipata hizi taarifa na wao wakajaza watu wao. Sasa kama mngeendelea na mpango wenu wa kutaka kumzomea Mh. Hamad Rashid basi nyie mafisadi wadogo kutoka Sinza na Mbezi, mlionyang'anywa matonge na CCM, ndiyo mngekula kichapo kutoka kwa watoto wa Manzese, Buguruni, Kigogo, Tandika na Mbagala.
 
Yaani hata Kiswahili ni tatizo kwenu? Inaonyesha wengi wenu mlikuwa mnakimbia somo la Kiswahili darasani na badala yake mlikuwa mnakimbilia masomo mengine.

Mh. Hamad Rashid kamtoa show DJ na mmiliki wa only strip bar in Tanzania. Akabaki kujichekeshachekesha tu!

Utuambie alisema nini na maana yake nini? Hata kama alitumia nahau au methali vyote hivyo vina maana siyo kutumika tu. Rejea hoja ya msingi ya wachangiaji na utuweke sawa. Tatizo siyo Kiswahili.
 
.
Watu wote wa vibandiko duniani kote wanaishi kwa kujishuku, na wala hawajiamini. Udini ndio center ya mapambano yao. Sasa hivi wameshikamana sana na ccm kwa sababu ya waandamizi wote wa serikali ya bara na visiwani ni wa dini yao. Wee suburi 2015 ccm ije na jina la mgombea wa dini tofauti na yao watakavyopiga about turn. Ndio utazihirisha haya ninayozungumza hapa.
.

Unapomnyooshea kidole mwenzio, vingine vitatu vinakuelekea wewe mwenyewe. Sasa jiangalie mwenyewe uliyekuwa unashangilia CCM wakati wa Mtakatifu wa Kikatoliki na wakati wa utawala wa mtoto wa Mtakatifu lakini sasa baada ya kuona waakina Pengo hawana lao mkakimbilia huko kwenye chama cha madhabahuni!
 
Hamadi:

Issue ya katiba peleka bungeni na siyo nje ya bunge.

Anaunga mkono CDM kutimuliwa bungeni.

Hr uelewe kwamba hatutaki katiba mpya itakayo tengenezwa bungeni na kuuliza wanafiki waseme ndio bali mkutano wa katiba utakao shirikisha wadau wote! sawa sawa!
 
mimi nadhani ni sahihi kabisa kama alivyosema Mh. Mbowe kwamba HR/CUF imechanganyikiwa kutokana na mkanganyo mkubwa wa kikatiba baada ya MUAFAKA kati ya CCM na CUF zanzibar.... hatimaye wamebadilisha katiba ya Zanzibar ku accomodate MUAFAKA THUS... what is the effect to the UNION ..... everything is dumb...... and silent and CUF and CCM zanzibar intentionally did not want to root on this because it could have been a blessing for the opposition....
 
Wana Jf baada ya kufwatilia mdahalo wa jana kati ya Mh Hamad R na Mh Freeman, nilibaki na maswali mawili magumu kwangu dhidi ya kauli ya Mh Hamadi aliposema kuwa "CUF kutoshiriki uchaguzi wa 2015 ni sawa na kuwaachia NGURUWE shamba".

Sasa je,
1 Mh Hamadi anafananisha washiriki (watu au vyama) wengine kwenye uchaguzi kama HARAMU?

2.Mh Hamad anatuambia kwamba siasa(shamba) imeingiliwa na watu HARAMU?

Hebu nisaidieni wana Jf

wewe hata hujui lugha yako? hayo ni maneno ya kawaida kabisa katika lugha ya kiswahili na yanatumika kila siku.

ni kweli ukizira na kumwachia nguruwe shamba la mihogo atalimaliza.
 
mdahalo wa jana ulinishangaza sana kuhusu mbowe kwenye mambo mawili

(i) anataka kujadili katiba ili kuondoa ulaji wa CCM lakini hataki kujadili mishahara mikubwa ya wabunge ili kuondoa ulaji wa wabunge

(ii) anakataa kuunganisha nguvu za upinzani na vyama vingine kumbe kuna 100M ambazo chadema wanachukua kwa kuunda serikali kivuli. hataki agawaned hizi pesa na akina mrema

hawa ndio viongozi wetu wapendwa
 
wewe hata hujui lugha yako? hayo ni maneno ya kawaida kabisa katika lugha ya kiswahili na yanatumika kila siku.

ni kweli ukizira na kumwachia nguruwe shamba la mihogo atalimaliza.

Sasa kwa kutumia mtazamo huohuo wa mh HR tuna weza kukiita ccm chama cha manguruwe bila shaka watakaoziriwa hapa ni wao.
 
mdahalo wa jana ulinishangaza sana kuhusu mbowe kwenye mambo mawili

(i) anataka kujadili katiba ili kuondoa ulaji wa CCM lakini hataki kujadili mishahara mikubwa ya wabunge ili kuondoa ulaji wa wabunge

(ii) anakataa kuunganisha nguvu za upinzani na vyama vingine kumbe kuna 100M ambazo chadema wanachukua kwa kuunda serikali kivuli. hataki agawaned hizi pesa na akina mrema

hawa ndio viongozi wetu wapendwa

So what?

Hawawezi kuwa viongozi wako kwa mtizamo wako huo; wakatae.
 
Wana Jf baada ya kufwatilia mdahalo wa jana kati ya Mh Hamad R na Mh Freeman, nilibaki na maswali mawili magumu kwangu dhidi ya kauli ya Mh Hamadi aliposema kuwa "CUF kutoshiriki uchaguzi wa 2015 ni sawa na kuwaachia NGURUWE shamba".

Sasa je,
1 Mh Hamadi anafananisha washiriki (watu au vyama) wengine kwenye uchaguzi kama HARAMU?

2.Mh Hamad anatuambia kwamba siasa(shamba) imeingiliwa na watu HARAMU?

Hebu nisaidieni wana Jf
Wana JF Naomba kufafanua kauli ya Mh. Hamadi tukumbushane historia kidogo km mtakumbuka mwanzo kabisa kwenye huu mfumo wavyama vingi kulitokea uchaguzi mdogo kule zanzibar vyama vyote vilivyopata usajili viliususia uchaguzi ule isipokuwa chama cha Mh. Chemponda kilishiri nakuhali kuitwa kwa uchaguzi wa kwanza wavyama vingi kwa msingi huo basi CUF ikastuka na kujifananisha na mkulima aliyelima shamba la mihogo kisha akalitelekeza na kuachia wanyama waharibifu akiwemo nguruwe, naomba wanajamii muwe mnaelewa lugha ya picha msiwe mnaenda mbali kisi cha kumuwekea mtu maneno mdomoni.
 
Wana Jf baada ya kufwatilia mdahalo wa jana kati ya Mh Hamad R na Mh Freeman, nilibaki na maswali mawili magumu kwangu dhidi ya kauli ya Mh Hamadi aliposema kuwa "CUF kutoshiriki uchaguzi wa 2015 ni sawa na kuwaachia NGURUWE shamba". Sasa je, 1 Mh Hamadi anafananisha washiriki (watu au vyama) wengine kwenye uchaguzi kama HARAMU? 2.Mh Hamad anatuambia kwamba siasa(shamba) imeingiliwa na watu HARAMU? Hebu nisaidieni wana Jf
Una level gani ya elimu?
 
Wana JF Naomba kufafanua kauli ya Mh. Hamadi tukumbushane historia kidogo km mtakumbuka mwanzo kabisa kwenye huu mfumo wavyama vingi kulitokea uchaguzi mdogo kule zanzibar vyama vyote vilivyopata usajili viliususia uchaguzi ule isipokuwa chama cha Mh. Chemponda kilishiri nakuhali kuitwa kwa uchaguzi wa kwanza wavyama vingi kwa msingi huo basi CUF ikastuka na kujifananisha na mkulima aliyelima shamba la mihogo kisha akalitelekeza na kuachia wanyama waharibifu akiwemo nguruwe, naomba wanajamii muwe mnaelewa lugha ya picha msiwe mnaenda mbali kisi cha kumuwekea mtu maneno mdomoni.

Hata kama kwa manguli wa lugha ya kiswahili hii ndio mnasema ni lugha ya picha, tunaomba mtufafanulie kuwa ni picha gani, mnato au ya video Kwasababu kumfananisha mwenzako na nguruwe ambao kwa wengine ni haramu pia ni hayawani mimi naliona hii ni dharau katika ukomo wake. Hapa hakupaswa kutumia hii lugha kati hili, akubal itu kuwa ulimi uliteleza.
 
wewe ulitaka wagawane na Mrema?mrema na tlp mbatia na Nccr ni NGOS za Ccm hivyo wana mgao wao toka Ccm
 
JAMANI MNYONGE MNYONGENI HAKI YAKE MPENI

Kama kweli sisi ni watanzania na kiswahili ndio lugha yetu nadhani tunaelewa ktk lugha ya kiswahili kuna Nahau, Methali, Misemo nk. alicho tumia HR ni msemo ambao utumika sana ktk maongezi hasa ya waswahili wa PWANI mfano.... kumuachia FISI bucha, ....kumuachia nguruwe shamba, ukicheka na nyani utavuna mabua nk.
Walio matajiri wa lugha ya kiswahili hasa wakazi wa mwambao hutumia vizuri sana misemo hii waongeapo, na ndicho alichokifanya HR ktk kuonyesha msisitizo (wengine tumezoea msisitizo huonyeshwa kwa lugha ya kingereza)
na mkumbuke kunakiswahili chenye rahaja ya kiunguja na chenye rahaja ya Lamu, hivyo alichokifanya RH ni kutumia msemo na tamathali za semi(kama sijakosea) katika kuongea kwake pia mkumbuke HR kiswahilichake ni chenye rahaja za kiunguja hivyo tusihukumu hapa kuwa huyu Bwana ni mdini au kafananisha watu na nguruwe kama hatusjui vyema kiswahili tuombe msaada wa manguli wa kiswahili kama Prof Safari nk

Nilitegemea unayejua huo msemo ungeeleza maana yake!
 
why Nguruwe na isiwe nyani? ina maana hajui nguruwe ni sacred animal kwa baadhi ya watu?
 
Jenifa nafikiri uliangalia mdahalo lakini hukuelewa kilichozungumzwa swala la 100m hiyo pesa ni bajeti ya kiongozi wa upinzani na wala haingii kwenye chama kwa hiyo hata wakiungana sio kwamba hiyo pesa vyama vitagawana itabaki kuwa ni bajeti ya kiongozi wa upizani. Pili swala la mishahara hilo lilikua kwenye ajenda yao wakati wa kampeni na walisema kama watakamata dola basi watapitia upya mishahara yote ili iendane na wakati na hata kupunguza mishahara mikubwa ya wabunge. Acha kupotosha na kupindisha kilichosemwa na mboye ebo!
mdahalo wa jana ulinishangaza sana kuhusu mbowe kwenye mambo mawili

(i) anataka kujadili katiba ili kuondoa ulaji wa CCM lakini hataki kujadili mishahara mikubwa ya wabunge ili kuondoa ulaji wa wabunge

(ii) anakataa kuunganisha nguvu za upinzani na vyama vingine kumbe kuna 100M ambazo chadema wanachukua kwa kuunda serikali kivuli. hataki agawaned hizi pesa na akina mrema

hawa ndio viongozi wetu wapendwa
 
mdahalo wa jana ulinishangaza sana kuhusu mbowe kwenye mambo mawili

(i) anataka kujadili katiba ili kuondoa ulaji wa CCM lakini hataki kujadili mishahara mikubwa ya wabunge ili kuondoa ulaji wa wabunge

(ii) anakataa kuunganisha nguvu za upinzani na vyama vingine kumbe kuna 100M ambazo chadema wanachukua kwa kuunda serikali kivuli. hataki agawaned hizi pesa na akina mrema

hawa ndio viongozi wetu wapendwa

Kuna watu wanafikiri kwa niaba yako. Siyo bure.

Chadema ilitumia mtu wa elimu ya darasa la saba kugombe nafasi ya Makamu wa Rais kwa sababu katiba iliyopo haizuii.

Mishahara ya wabunge ni mikubwa kiasi hicho kwa sababu katiba iliyopo inaruhusu ubadhirifu.

Kama ungekuwa mtihani ungepata 0% na hoja yako mfu.

Wewe unaangalia mshahara wa mbunge badala ya kuangalia kinachosababisha mshahara wa mbunge kuwa mkubwa.

Kamanda Mbowe alikuwa sahihi. Ni suala la kujadili katiba inayoruhusu uozo uliopo, siyo kujadili uozo bila kuangalia kunachosababisha uozo.

Kama nyumba yako ya tembe inavuja usawa wa kitanda, dawa siyo kuhamisha kitanda na kuzoa maji. Ni kuangalia wapi panavuja ili pazibwe.

cuf wanaona wivu. hawaamini kama chadema ni chama imara kiasi hiki. imekula kwenu.

usitoe mada kila mtu akajua wewe ni kilaza anayekurupuka.
 
Hata kama kwa manguli wa lugha ya kiswahili hii ndio mnasema ni lugha ya picha, tunaomba mtufafanulie kuwa ni picha gani, mnato au ya video Kwasababu kumfananisha mwenzako na nguruwe ambao kwa wengine ni haramu pia ni hayawani mimi naliona hii ni dharau katika ukomo wake. Hapa hakupaswa kutumia hii lugha kati hili, akubal itu kuwa ulimi uliteleza.

Kaka nna mashaka na kauelewa kako kwenye hii lugha kwa wale waliosoma miaka ya nyuma kati ya 80s na 90s wakati huo unaingia kufanya mtihani wa kiswahi ukilazimika kuielewa fasi simulizi, andishi na misemo, methali na wakati huo unawekusa swali linalokutaka uifafanue lugha kweli kweli, kwanyakati hizi za walimu wa vodafaster ningumu sana kwa mwalimu kumfanya mwanafunzi wake kuwa mahili kwenye lugha ya kiswahili.
 
Back
Top Bottom