Dr. Wansegamila
JF-Expert Member
- Feb 3, 2012
- 2,920
- 7,942
Mchungaji Mbarikiwa Mwakipesile jumapili iliyopita wakati wa ibada katika kanisa lake linalojulikana kama, 'Kikosi kazi cha injili', alimuita mmoja wa waumini wake kijana anayeitwa Eliya na kuamuru ampatie simu yake, ambapo aliikagua na kukuta meseji ya WhatsApp kutoka kwa binti.
Kisha akampigia huyo binti akiwa hapo hapo madhahabuni kwa simu ya Eliya, na mwisho alimtimua Eliya ibadani.
Tukumbuke kuwa huyu mchungaji ametoka gerezani hivi karibuni baada ya kushinda rufaa yake ambapo awali alikua amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela kwa kosa la kuendesha kanisa bila usajili.
Nimeambatanisha clip hapa chini.
Je, unazungumziaje, hii ni sawa Mchungaji kukagua simu za waumini wake tena hadharani?
Mimi naona ni unajisi wa wazi wa haki ya faragha kwa waumini wake, mbaya zaidi inakua kama udhalilishaji kwa kufanya haya hadharani.
Hii inasikitisha sana.