Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 15,311
- 9,739
Ndugu zangu Watanzania,
Habari ndio hiyo kuwa mahakama kuu kanda ya Mbeya imemuachia huru mchungaji Mbarikiwa Mwakipesile ambaye alifungwa kifungo cha miaka mitatu na siku 14 jera kwa kosa la kuendesha shughuli za kanisa pasipo kuwa na kibali cha kufanya hivyo kama sheria zinavyotaka.
Ambapo baada ya kufungwa jela aliamua kukata rufaa kupitia mawakili wake.na baada ya kukata rufaa na kesi kuendeshwa.hukumu ikatoka ikitupilia mbali maombi yake ya kuachiliwa huru na badala yake mahakama hiyo ikatoa hukumu ya kumtaka kulipa kiasi cha shilingi milioni kumi ama kuendelea kutumikia kifungo chake hicho mpaka kiishe. .
Ambapo hata hivyo amefanikiwa kulipa pesa na kiasi hicho cha millioni kumi kilichoamuliwa na mahakama na hivyo kufanikiwa kuachiliwa huru.
Rai yangu ni kuwasihi watanzania wenzangu kutambua kuwa nchi yetu inaendeshwa kwa misingi ya sheria ,katiba na utawala bora.ambapo kila kitu lazima kizingatie sheria katika uanzishaji wake.hata katika suala la kuanzisha kanisa mimi naamini Mchungaji Mbarikiwa Mwakipesile akiomba kibali atapewa bila shida ya aina yoyote ile pale atakapo timiza vigezo vinavyohitajika.
Hii ni kwa kuwa Taifa letu na serikali yetu hasa Rais wetu mpendwa kipenzi cha watanzania mama samia suluhu Hasssan, angependa kuona Taifa letu lote linamjuwa Mungu na kuwa na hofu na Mungu na hivyo kufanya matendo ya kila mmoja wetu kuwa yenye uungwana, upendo,ukarimu , unyenyekevu,huruma ,utu,hekima na busara.
Kumcha Mungu pia kutapunguza na kuondoa katika jamii matendo ya rushwa,ukatili ,ufisadi na wizi. Matendo na Vitendo kama vile ubakaji,mauaji kwa imani za kishirikina au kutimiza masharti ya waganga kama yale ambayo mtu anaua arubino au kubaka mtoto wake wa kumzaa au kubaka kikongwe au kuuwa watu kwa NONDO kwa fikira na imani za kupata utajiri yangekwisha katika jamii kama sote tungekuwa na hofu ya Mungu. Na kubaki kutambua kuwa utajiri unapatikana kwa kufanya kazi kwa bidii, juhudi,maarifa na kujituma kwa hali ya juu.
Kama kila mtu angekuwa na hofu ya Mungu moyoni mwake hata matendo ya viongozi wetu yangekuwa ni ya huruma na wala tusingesikia mambo ya rushwa na ufisadi .kwa kuwa kila mtu angejuwa kuwa mali na pesa ni vya kupita na hakuna anayezikwa na pesa wala magari wala ufahari wote wa Dunia hii. kila kiongozi angetambua kuwa kuna kufa na kuna Mungu yupo hai anaangalia kila kitu afanyacho mwanadamu, maana yeye huona hata yale ya moyoni mwetu wanadamu na hata yale ya sirini na gizani ,kwake Mungu yapo na kuonekana peupe kabisa. .
Lakini pamoja na kuhitaji yote haya ni vyema kila mtu azingatie sheria ikiwepo hiyo ya kupata vibali. Lakini pia ya kaisari mpe kaisari na yaliyo ya Mungu mpe Mungu . Ukitaka kufundisha neno la Mungu na kuchunga kondoo wake basi fanya hivyo kwa moyo wote na kwa kumtanguliza Mungu wako.na ukitaka kufanya siasa basi fanya siasa.
lakini usitake kufanya siasa halafu ukatumia mwamvuli wa kanisa lako kupenyeza ajenda zako ama hisia zako za kisiasa na itikadi za kisiasa. Hilo litakuwa ni jambo la hatari sana tena sana sana na litakalo leta mgawanyiko kwa unaowaongoza,maana dini ni imani na unakuwa unacheza na mioyo ya watu na hisia zao. Hivyo ni bora kuwalisha kondoo wako neno la Mungu na misingi yake na kufanya rejea na nukuu kutoka katika biblia takatifu.
Tusilete na kuweka uanaharakati makanisani au misikitini kwa kutumia nyumba hizi za ibada kuyageuza kuwa majukwaa ya kisiasa kueneza sera na ajenda za vyama vyetu. Tunavyovipenda na ambavyo ni wanachama wake au wakereketwa au mashabiki au wafuasi wake.
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
0742-676627.