Mchungaji Gwajima: Daudi Albert Bashite alipata division Zero

Mchungaji Gwajima: Daudi Albert Bashite alipata division Zero

Kweli Mchungaji ni mdanganyifu wa kondoo wa bwana
 
Nijuavyo mm kwa awamu hii wateule huwa hawaguswi hata watanzania wapige kelele vp tutaishia kuumia tu.
Mfano halisi angalia kwa January alikuwa na kashfa nzito lkn ikapotezewa.
Kashfa ya farujohn naona pia kama waziri husika kapotezewa hivi.
 
na quote " mimi mchungaji gwajima nasema nina cheti cha division zero cha makondai''

w
atanzania tusiwe mbumbumbu kushangilia kila kila kitu ndio mana mr kibwetere aliua watu uganda kwa mambo ya kushangilia wachungaji.

tuulizane tangu lini necta wanatoa cheti kwa kwa mtu aliepata division zero.

think critically
What about results slip! Does it Indicate grades such as F, F, F, F, F, F, F, F, F,................... Fight Friends Fierce Fight For Food First
 
Huyu mchungaji kiboko aiseh,anazidi kutia aibu,mtumishi wa Mungu roho ya kisasi anaitoa wapi? Kama mtu kakufanyia ubaya kwa wewe mtumishi wa mungu unatakiwa ukae kimya umuache Mungu afanye yake,huu utetezi wake unanipa mashaka huenda ile tuhuma ni ya kweli,sio kwa povu hili,hili povu sio la nchi hii
 
Mkuu kinachonitisha sio ni nani kaumizwa. Ni utamaduni huu wa Ku deal na issues Sasa hivi ya Kabwe ikiwemo. Kama hana cheti anatakiwa awajibike. Ila swali ni kuwa, hatuna namna nzuri ya kushughulikia matatizo yetu. Viongozi na tunaoongozwa
Wa kujibu maswali yako ni mkuu wa nchi. Asingepotezea, watu wangekwisha nyamaza. Hii na ifananisha na issue ya Kitwanga, kashfa ilihusu Kuhusishwa kwake na Lugumi, akaja kufukuzwa kwa kitu kidogo, aka sevu kwenye kubwa, ikawa mwisho wa mjadala.
 
Ndo maana nikasema habari imekaa kiuongo anaposema anavyeti kumbe anamaanisha matokeo!!!Kuhusu kusoma Nyegezi ni kweli mzee wangu kamfundisha pale Fisheries
Mbona umekazania sana habari ya baba yako kumfundisha Makonda, kama angekuwa amemfundisha Magufuli si ndio uzi wote ungejaa statement yako.
Sasa fanya hivi, kwakua baba yako alimfundisha Makonda, muulize je wakati Makonda anajiunga hapo chuoni aliingia kwa qualifications zipi na vyeti kutoka shule zipi?
 
vyeti vya division zero vilikuwa. vinatolewa na necta miaka ya 90 hadi elfu 2 naa baada ya ndalchako. kuingia necta akafuta sasa kama umezaliwa juzi huwezi jua haya....
 
Hahahaaa hivi mtu unakaa unaanza kutetea mtu asiyekulisha, utapata stress bure kwa mambo yasiyo kuhusu mwishowe upate vidonda vya tumbo, wewe kaa utulie uanglie mechi
 
Watoto WA miaka ya 2000 bwana! Hebu prove uongo WA Gwajima kwa kuweka Cheti cha division 01 ya Bashite. Ni bora kukaa kimya kuliko kujichoresha kama hivi, ona sasa tushajua Rika lako.
 
Tujifunze unapojiona wewe ni msafi sana na kuanza kuchafua majina ya watu matokeo yake ndio haya.nasikia anashinda kwa masheikh na maaskofu wamuombee sijui ndo apate cheti hata aeleweki. Tujifunze jamani

Anajusumbua Mungu hapendi ujinga na hasafishi vyeti feki
 
kazi ya fasihi ni kufikisha ujumbe sio kuchambua sarufi.ujumbe umetufikia kama hujaelewa we ndo mbumbumbu na siyo watanzania
 
na quote " mimi mchungaji gwajima nasema nina cheti cha division zero cha makondai''

w
atanzania tusiwe mbumbumbu kushangilia kila kila kitu ndio mana mr kibwetere aliua watu uganda kwa mambo ya kushangilia wachungaji.

tuulizane tangu lini necta wanatoa cheti kwa kwa mtu aliepata division zero.

think critically
mimi nilipewa na necta cha ziro
 
Nategemea DC PAUL MAKONDA atamshtaki Bishop GWAJIMA mahakamani kwa kosa la kumdharirisha.

Nategemea JESHI LA POLISI litamkamata na kumhoji Bishop GWAJIMA kwa kumchafua MTUKUFU DC PAUL MAKONDA.

Nategemea Waziri wa Elimu Prof JOYCE NDALICHAKO atajitokeza hadharani kutoa ufafanuzi,Kuthibitisha au kukanusha hizi tuhuma zinazoendelea ili kulinda hadhi ya elimu ya Tanzania ambayo Inadharirika kwa hizi tuhuma za kufoji vyeti..

Nategemea MTUKUFU DC PAUL MAKONDA atajitokeza hadharani,kulikana jina la DAUD BASHITE,atajitokeza na vyeti vyake vya kuzaliwa,cheti cha darasa la saba,cheti cha form four,Six na cha chuo ili kutoa ukweli wa uhalali wa jina lake

Nategemea Mamlaka iliyomteua MTUKUFU DC PAUL MAKONDA Kwa maana taasisi ya Rais itatoa tamko,Either Kuiamrisha wizara husika ifuatilie uhakiki wa vyeti vya mkuu wa mkoa,Au itatoa taarifa ya kuthibitisha juu ya uhalali wa vyeti vya Paul Makonda,Na kujiridhisha ka amejipatia ajira serikalini kwa taarifa za uongo (Obtaining Employment with fake documents) ama Itengue uteuzi wake ili kulinda Hadhi ya utawala bora na Maadili ya Umma.

Nategemea Immigration kuanza uchunguzi Ili kujua kwamba MTUKUFU DC anahusika na wizi wa taarifa za mtu mwingine(Identity theft),Kujipatia hati ya kusafiria kwa taarifa za uongo (Obtaining passport using fake Information),Kusafiri nje ya nchi kwa kutumia taarifa za kughushi/Za mtu mwingine (Travelling with false documents)

#NB
Haya yote ni kwa manufaa ya MTUKUFU DC PAUL MAKONDA kwanza itasaidia kuweka ukweli bayana hii italinda hadhi yake na utu wake,Lakini italinda hadhi ya utawala bora na Maadili ya umma.

Lakini italinda na kusafisha elimu ya Tz ambayo imeshaanza kuingia dosari.

Pia italinda hadhi ya uwajibikaji na usawa kwa vyombo vyenye mamlaka ya kuthibitisha haya mambo kwani Ganzi waliyopigwa sasa plus ukimya unaleta shaka na walakini katika uwajibikaji na utendaji wao.

NATAMANI nisikie sauti ya MTUKUFU DC PAUL MAKONDA ikisema "DAUD BASHITE nikukute Central kesho saa nne"

NGOJA NINYWE KIROBA NILALE MAANA HAYA MAPAMBIO YA DAUD BASHITE yamekata usingizi wanguuu...
 
Back
Top Bottom