Mchungaji Gwajima: Daudi Albert Bashite alipata division Zero

Acha uongo miaka gani hiyo walikuwa wanatoa vyeti acheni uongo wa kijinga,Paul kasoma Nyegezi chuo cha uvuvi alitumwa jina la Paul Makonda na mzee wangu kamfundisha mwambieni huyo Gwajima aache wendawazimu
Hakuna haja ya povu. Muda utasema.
 
Pamba ya jioni...wanaitaga elimu ya watu wazima.. Nadhan akisema cheti cha zero anamaanisha matokeo ya zero..nna uhakika hata icho cheti cha Paulo hana ila ni matokeo yao..
Ila hata kama umepata zero unaweza kupata result slip hahaa! Miti inateleza kama imemwagiwa Castrol!
 
Alimaliza wapi na lini? Na jina lipi alitumia form four? Alichaguliwa wapi kidato cha tano? Tusidanganyane humu
 
Watanzania wanaongoza kwa umbeya,kamwe sijawahi ona sehemu mtu kaanzisha thread na akasema aulizwe swali lolote kuhusu fani flani,ila habari za watu ni mafundi,halafu unalalamika kuwa nchi aiendelei,hakika wale maadui zetu watatu Tanzania kwa akiri za dizaini hii kamwe hatuta kuja kuyashinda.
 
Hivi kwenye hii kamati ya bunge katika wauliza maswali na TL yumo? Maana kama Lissu ni mmoja wa wauliza maswali kitakacho tokea.............
 
Aspomtimua basi na watumishi wengine wenye vyeti feki wasifukuzwe,,na waliofukuzwa warudishwe kazini
 
1)Au hamchukulii hatua kwa sababu naye ana PHD feki?
2)kwa nn amchukulie hatua wakati naye ya kwake ni Fake?
 
Acha kupanic... Wacha dawa ikuingie ewe Bashite mdogo.
 
huyu mchungaji utadhani SEKILOJO CHAMBUA alimvisha kanzu jogi duu dunia lukumbalukumba
 
Kwa bongo huyo anaweza asitumbuliwe kwa kuonyesha udhaifu wa kuteua watu waliofeli sasa bwana yule huwa ataki kuonekana kafeli kwenye teuzi zake atabaki nae tuu...
 
Kwa dua zile za mashekhe, walakhi watu pamoja na Gwajima wajisumbua tu! Tena waliomwombea dua ni mashekhe vingunge, aaahhhh Sidhani! Kama ikatokea kelele hizi zikamletea matatisi sitozikubali tena dua!
 
Mbona kuna Mkuu wa mkoa mwingine naye alipata zero
Mkuu wa mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka ni kweli alipata division ziro A level kama ilivyo kwa Mbowe. Kwangu mimi kupata division ziro sio issue. Kuna sababu nyingi ambazo zinaweza kumfanya mtu apate division ziro; kwamba mtu anaweza kuwa na uwezo darasani lakini bado akapata division ziro kutokana na sababu mbalimbali. Wengi hapa hatuna maelezo kama Ole Sendeka baada ya kupata division ziro alirudia mtihani au vipi. Kuna taarifa Mbowe yeye alirudia na baadaye akajiendeleza na kupata shahada.

Sasa suala la Ole Sendeka kupata division ziro haliwezi kulinganishwa na hilo la Makonda (kama ni kweli) la kutumia cheti cha mtu mwingine. Hii ikithibitika inaweza kuwa "criminal offence", maana yake atakuwa alidanganya ili kupata nafasi ya kujiunga na vyuo na baadaye kuwa katika nafasi aliyonayo! Sijui sifa za mtu kuteuliwa kuwa mkuu wa mkoa, lakini sidhani kama udanganyifu ni miongoni mwa sifa hizo. Hili ni moja ya jaribu kubwa kwa JPM. Hoja sasa ni kwamba watu wanataka wamwone mkuu wa nchi anayesimama kila siku majukwaani akilia kuwa kuna watumishi hewa au walioghushi vyeti anachukua hatua gani kwa mtu aliyemteua yeye mwenyewe.

Hoja kwamba watu walikuwa wapi wasiyaseme hayo hadi alipoanza kutaja 'watuhumiwa wa madawa ya kulevya' haipaswi kupewa nafasi katika jambo hili maana ushiriki wake katika vita hivyo bila kujali kama ameshiriki vizuri au la, hakumpi kinga ya kuchukuliwa hatua iwapo anathibitika kutenda maovu. Na hili la tuhuma zake kuhusu elimu yake na matumizi ya cheti kisicho chake ni muhimu sana likafanyiwa kazi kwa kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya utendaji kazi wake na utata wa elimu yake.
 
hata kama..ila dogo ana busara na anajua uongozi!!! nawahakikishia ataendelea kuwa kiongozi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…