wise-comedian
JF-Expert Member
- Aug 4, 2011
- 3,290
- 3,946
Wanasiasa si wa kuamini bila uthibitisho,kuna watu waliwahi kumchafua lowasa hadi tukawaamini wakamkosesha ikulu...sasa wanaona aibu hata kumuomba msamaha.
Daudi Bashite Hakusoma UDSM Mkuu. Alisoma MUCCOBS ambapo inasemekana alidisco mara tatu na baadae akatoka na cheti kwahiyo kuna uwezekano chuo cha MUCCOBS walimuuzia Paul Makonda cheti cha degree. haiwezekani mtu adisco mara tatu katika chuo hicho hicho baadae eti anatoka na cheti cha kumaliza masomo. Huyu daudi alishajijengea tabia ya kufoji elimu.Salam..
Binafsi, nimeamua kuyaweka maoni yangu katika mtindo huu "WATETEZI WA DAUDI BASHITE NA ULEMAVU WA FIKRA". Kwasababu robo tatu (3/4) ya wanaccm wamekuwa watetezi wakubwa kwenye ishu ya vyeti feki vya ndugu yetu DAUDI BASHITE.
Hakuna mtanzania mwenye akili anaweza kupinga vita dhidi ya dawa za kulevya, lakini vita hiyo hakuhalalishi mtu kughushi vyeti.
Ndugu zangu wanaCCM, Athari za tabia hii ni kutengeneza wataalamu bandia ambao baadaye hawatathaminika katika soko la ajira la kimataifa na mwishowe kulitia doa taifa letu. So ni jambo njema sana kwa mtu kuwa na vyeti halali,,, Mwanaccm hivi unajisikiaje katika sehemu unayofanyia kazi usikie kuna mtu analipwa msharaha mkubwa alafu na nyeti vya kughushi?
Haiingii akilini kwanini wanaCCM wanang'ang'ania watu wenye vyeti feki(mfano DAUDI) wawepo serikalini kwakuwatetea kwa kivuli cha madawa ya kulevya.
Kama kweli DAUDI ana vyeti halali ajitokeze kujibu tuhumu hizi. Mfano kaka NCHEMBA japokuwa maelezo yake yalikuwa yanaukakasi sana juu ya elimu yake.
Hapa wanaCCM tujenge tabia ya UTHUBUTU kwa maslahi ya taifa. Na kutoa kauli kama "CCM BILA VYETI FEKI INAWEZEKANA" kama ilivyo kauli ya HAPA KAZI TU.
Ndugu zangu wanaccm kuhalalisha vyeti feki ni kuzalilisha chuo kikuu cha dar es salaam, kwasababu ndugu DAUDI alisoma hapo so tusije tukaonekana kuwa wote ni walewale yani VYETI FEKI.
Kimsingi naomba kutoka sasa tubadilike, matangazo ndio kama haya.
View attachment 477235
Mr mkiki.
Sasa hapo ndio bwana makonda anatakiwa atoke kifua mbele na vyeti vyake halali kuanzia kile cha kuzaliwa hadi cha ubatizo na kuwaziba midomo hao wenye chuki nao..Tatizo hakuna ushahidi juu ya hayo mnayotulazimisha tuyaamini,kama haujui siasa ni mchezo mchafu sana,ili tuamini hayo madai yenu tuleteeni huyo aliyemuuzia vyeti kuthibitisha vinginevyo ni hila tu na chuki zisizo za msingi.
Ndugu, Jamaa na Marafiki, Njooni Tumtetee Makonda Dhidi ya Mapapa Wauza Unga Wanaomzushia...Baada kuona mjadala tena mrefu humu ndani leo na mimi naona nitoe uzi wangu ili tupate kujadili wote na ikiwezekana kila mmoja awe amepata jibu sahihi.
Hii ni kutokana na swala linaloendelea ambapo mimi siwezei kukubaliana nalo wala kulikataa ila naweza kulikubali endapo tu itakuja evidence itakayoonyesha hii ni kweli, si jambo lingine nalozungumzia hapa ni swala la kusema RC wa Dar amechukua jina ambalo si la kwake, hebu tujiulize maswali yafuatayo ili tupate kujiridhisha na kuweza kumaliza utata wa swala hili.
1: Mmiliki halali wa hicho cheti yuko wapi na anajihusisha na nini?, na je ni kwanini asijitokeze au asichukuliwe ili kumaliza mzizi wa fitna badala ya kumsubiri huyo mtu anayedhaniwa amechukua jina la mtu na kulitumia ndo afanye hivyo?.
2: Endapo akijitokeza huyo mhusika (mmiliki halali wa hicho cheti) anapaswa kuulizwa maswali kadhaa
A) ni kwann alikubali jina lake litumiwe na mtu mwingine na kupelekea huyo mtu kujiendeleza kielimu na si yeye binafsi
B) kwann alisubiri watu wajitokeze na si yeye binafsi asiende kwenye vyombo vya sheria ili kuchukua hatua juu ya swala hilo?.
C) atatuthibitishiaje umma tupate kuamini kuwa yeye ndo mmiliki halali wa hilo jina?
3: kama kuna mtu mwenye ushahidi mbali na mhusika kamili ambaye bado hajatoka mbele ya kadamnasi kuthibitisha kuwa bwana Daudi Bashite alibadilisha jina na baadae akaitwa Paul Makonda ni kwanini asijitokeze na kuweka mambo hadharani ili watu wajue ukweli badala ya kupiga kelele kwenye mitandao ya kijamii.
4) familia ya mtu ambaye cheti chake kilichukuliwa either kwa kununuliwa au kwa kukitoa kawaida iko wapi? na kwanini hawataki kujitokeza hadharani ili kuwafungua watanzania wengi wanaoamini au wasiamini hii sinema kama ni kweli au la?
5) Walimu, wanafunzi wenzake na Daudi Bashite pamoja na Paul Makonda wako wapi? Na kwanini wasijitokeze na kutoa ushahidi kamili licha ya huu unaosadikika?
6) na je ni kwanini wasifatwe ndugu wa karibu wa familia ya paul makonda na kuhojiwa juu ya hili swala ili kupata jibu sahihi mbali na kuendelea kupiga kelele kwenye mitandao ya kijamii?
NB: kuna kipindi kulikuwa na maswala kama haya ya bwana Daud Bashite na ikapelekea kuandikwa kwa kitabu cha "MAFISADI WA ELIMU" kuna baadhi ya viongozi ambao mpaka leo wapo madarakani, na watu wamekosa ushahidi wa kusema kwamba wamechukua vyeti vya watu na kujiendeleza kielimu au la.
Mtazamo wangu kama ni kweli huyu jamaa alichukua vyeti ni heli yakatumiwa hayo maswali kama njia mojawapo ya kusema ukweli kuliko kusema, kuandika sana haya mambo kila siku kwenye mitandao ya kijamii na hata kwenye baadhi ya vyombo vya habari bila ya kuwa na ushahidi yakinifu na kuwafanya watanzania kuacha kufanya mambo mengine na kujadili hili jambo kila siku.
[HASHTAG]#huu[/HASHTAG] ni mtazamo wangu tu ambao utatusaidia kumaliza huu utata wa bwana Daud Bashite/Paul Makonda.
Ushahidi umewekwa kama mhusika anaona anachafuliwa ashitaki wanaomchafua, serikali ilipohakiki vyeti haikulazimika kutafuta wamiliki halali wa vyeti ilitafuta watu ambao wamejipachika sifa ambazo sio zao. Waziri wa Elimu ajiandae na swali hili la nyongeza juu ya uhalali wa vyeti na ninavyomjua atasimama kwenye ukweli, baadhi ya watu hutumia vyeti vya watu ambao wameshafariki hivyo sio rahisi kumpata mhusika kuja kutoa ushahidi nafikiri hata ushahidi mwingine unaweza kutumika kuthibitisha.Tatizo hakuna ushahidi juu ya hayo mnayotulazimisha tuyaamini,kama haujui siasa ni mchezo mchafu sana,ili tuamini hayo madai yenu tuleteeni huyo aliyemuuzia vyeti kuthibitisha vinginevyo ni hila tu na chuki zisizo za msingi.
Mkuu hebu rejea nyuma na kuangalia viongozi wote waliotuumiwa kwa kesi kama hivi walitoa ushahidi wao?, mm nadhani hili litaisha kama kwa wengine wa awali ambao waliandikwa kwenye kitabu cha "mafisadi wa elimu' au wengineo wa juzi juzi hapa1. Kwa sababu umesema HUWEZI KUBALIANA NALO, basi hutakubaliana nalo hta ushahidi ukiletwa.
2. Na kama Paul Makonda "original" amekufa na hayupo, utaendelea kutokuamini..??
3. Na kama yeye KWELI ni Paul Makonda the real one, kwanini asioneshe vyeti vyake ili kuondoa utata huu na maisha yaendelee na wote wanaomtuhumu waone aibu..???
Mimi mwenyewe mwanzoni nilikuwa napuuzia nikidhani ni kashfa za kisiasa, ila sasa naanza kuamini ni kweli kwa sababu it costs nothing kuonesha cheti chako. Watu wamemtyt jamaa
Kama huyo mtuhumiwa hajakana mashitaka mpaka leo ni kwann hatua zingine zisitumike kama ambavyo nimependekeza ili kuumaliza huu utata na watanzania wote tukajua mbivu au mbichi juu ya hili swala.mshukiwa ndiye anayetakiwa kukana mashtaka. Tatizo ni pale mshukiwa anapoulizwa swali kuhusu jina lake halisi na uhalali wa vyeti vyake, yeye anakua bize kuzungumzia ushoga wake, kukosa mtoto na madawa ya kulevya. kazi rahisi kufunga mjadala ni hii
- anatakiwa kukana kua yeye si Bashite. baada ya kukana, uchunguzi utafanyika kijijini kwao ili kubaini kama yeye si Bashite kweli au kadanganya. au
- anatakiwa akubali kua yeye ni Bashite. baada ya kukubali kua yeye ni Bshite, itabidi atuonyeshe vyeti vyake vya kidato cha nne vyenye jina la Bashite alivyovitumia kuombea chuo.
Shida siyo kukubali au kutokubali kuhusiana na swala. Issue iko hivi kama mshtakiwa hataki kutoa majibu sahihi ili kuweka mambo wazi ni kwann watu ambao wanaushaidi kuhusiana na swala hili wasijitokeze na kukitia kimbutua mchanga na watu wakajua?. Maana tukiendelea hivi mwisho wa siku naona itakuja kama kipindi kile cha " mafisadi wa elimu" ilivyokuwaga na hatukuwa na ushahidi kama ni kweli watu walichukua majina ya watu au la?1. Kwa sababu umesema HUWEZI KUBALIANA NALO, basi hutakubaliana nalo hta ushahidi ukiletwa.
2. Na kama Paul Makonda "original" amekufa na hayupo, utaendelea kutokuamini..??
3. Na kama yeye KWELI ni Paul Makonda the real one, kwanini asioneshe vyeti vyake ili kuondoa utata huu na maisha yaendelee na wote wanaomtuhumu waone aibu..???
Mimi mwenyewe mwanzoni nilikuwa napuuzia nikidhani ni kashfa za kisiasa, ila sasa naanza kuamini ni kweli kwa sababu it costs nothing kuonesha cheti chako. Watu wamemtyt jamaa
Mi sidhani kama bunge litajadili kuhusiana na swala la mtu kufoji vyeti maana itahitaji ushahidi wa kina ili kudhibitisha hili. Pia tukumbuke kama yeye ni kweli alifanya hilo swala basi kuna haja ya kuwafanyia uchunguzi mpaka wale wengine waliobadi na kukili kwa sababu nao watakuwa wamefanya makosa.Hii movie itaisha vizuri pale bunge litakapomweka kitimoto na kuchambua makosa yake yote, na kumwachie rais aamue. Kwa sasa aachwe azunguke nyumba zote za ibada huku akilia kama alivyokuwa akiliza binadamu wenzake.