Kwenye akaunti yake ya facebook, kada wa CCM ndugu Yohana Mabena ameandika hivi
"Mh Mkuu Wa Mkoa Wa Dar-es-salaam Mimi binafsi na kupongeza sana kwa kazi zako unazozifanya kuhakikisha Jiji la Dar-es-salaam linakuwa Jiji la biashara na linakuwa Jiji la ushindani .
Pili naomba nikupe ushauri wangu kwa kutoa mfano Wa mtu mmoja tu au wawili Mh
Mwigulu Nchemba aliwahi tuhumiwa kuwa vyeti vyake vinatofautiana na ikazungumzwa sana kwenye mitandao na wanaccm tulipata utata sana kumtetea humu lakini kwa muda mchache alitoa vyeti vyake hadharani kila mtu aliviona na akaeleza sababu ya vyeti vyake kutofautiana jambo hilo likaisha.
Tatu kulikuwa na tuhuma dhidi ya Mh Zitto Kabwe kuwa hana shahada ya kwanza baadae akatoa cheti chake hadharani mjadala ukaisha.
Nikija kwako kuhusu tuhuma ya vyeti vyako ambayo inatupa shida sana sisi wengine wanaccm kukutetea humu kwasababu wewe ndiye pekee unayeweza kutuondolea utata huu .
Ushauri wangu Fanya kama walivyofanya viongozi wengine hao kwa kuweka vyeti vyao hadharani iliutuondolee utata huu kwani kukaa kimya au kuanza kubishana na Watu haisaidi hata kidogo njia pekee ya kuondoa utata huo wewe in kutuwekea vyeti hadharani na kama kuna ukweli kuhusu tuhuma hizo tupe sababu watanzania kuhusu hilo .
Huo ni ushauri wangu kwako Mkuu Wa Mkoa Wa Dar-es-salaam kwani ndiyo njia pekee ya kuondoa utata huu unaoendelea kila siku .
Kwani ni dhambi kubwa na ni kosa kubwa kwa kiongozi Wa umma kutuhumiwa na kushindwa kutoa Maelezo juu ya tuhuma zinazomkabili".
[HASHTAG]#Mytake[/HASHTAG]:
Makonda hana namna nyingine zaidi ya kutoka na kusafisha upepo huu. Hata wanaomsapoti humu unafikia wakati wanashindwa na kuishiwa pumzi. Kutoa vyeti tuu kwani bei gani? Kulia pekee hakuwezi kumsafisha. Hata kusingizia kuwa tuhuma hizi zinatokana na vita yake dhidi ya madawa ya kulevya hakuwezi kumwacha salama. It's high time for him to come out bravely and clean the windscreen before it becomes worse