Mkuu Msemaji unwell, kwa kuanzia, japo Mchungaji Gwajima alisema anavyeti, hii sii kweli, emesema uongo ila common sense ulielekeza anamaanisha ana nakala na sio vyeti. Kuhusu huu uongo wa Gwajima, tumeuzungumza hapa.
Mchungaji Gwajima ni Mtumishi wa Mungu wa kweli au? Asema Uongo! Adai yeye ni zaidi ya Rais...
Pili vyeti vyovyote vya elimu, hospital, safari (passport), kuzaliwa, uraia, kifo etc, au cheti kingine chochote hata leseni, sio nyaraka za serikali bali ni personal documents, hivyo haziingii kwenye sheria ya nyaraka za serikali.
Passport na leseni ndizi nyaraka za serikali kwenye personal documents ambazo serikali inakuazima na kuweza kukunyanganya wakati wowote.
Sio kosa kisheria mtu mwingine yoyote kukutwa na personal document ya mtu mwingine yoyote as long as ameipata kihalali.
Nyaraka za serikali at person level ni barua zote za kiserikali mtu unapoandikiwa na sio kosa kwa barua hizi kukutwa kwa mtu mwingine yoyote.
Nyaraka za serikali ambazo ni kosa kisheria kukutwa kwa mtu mwingine, ni zile tuu zilizogongwa muhuri wa siri/confidential, Secret na Top Secrets.
Vyeti vya elimu vya mtu yoyote sio confidencial, sio secret wala top secrets documents hivyo sii kosa kisheria mtu mwingine yoyote kuwa navyo kihalali na ukikutwa na vyeti vya mtu mwingine isivyo halali, ni kosa la kukutwa na malí ya mtu kama wizi mwingine wowote na sio kosa la kukutwa na nyaraka za serikali.
Paskali