Mchina aliyepata "A" tisa NECTA

Mchina aliyepata "A" tisa NECTA

Mwishoni tutasikia serikali itasema "na wachina waliochukua nafasi za masomo waondoke kwao ili kumpatia nafasi mtanzania
 
Je huyo Mchina mpaka kafaulu vizuri hivyo alifundishwa na nani?na Wachina wenzie?
Na Je, alisoma shule gani?
Unless angekua kasoma shule ya serikali(tena sanasana ingekua 'ya Kata'),Sioni ajabu yeyote,somo hapo ni kujitaidi kupeleka watoto wetu shule za 'full package' kama kina Feza Marian etc!
NOTE,Private Schools na Government Schools ni Universe mbili tofauti kabisa.
 
Umeishiwa hoja wewe, issue haikuwa kulifanyia nini taifa, kama umeishiwa si unanyamaza tu, kwani lazima ujibu, ubishi mwingine bana...
Siwezi kunyamaza ninaposoma hoja ambazo ni za kitoto sana. Kuna kasumba Tanzania, kwamba mtu anayejua kingereza ndio mjanja, ni kasumba mbaya sana ndio maana baadhi ya watu wakishalewa wanaanza kuchomekea maneno ya kingereza. Kingereza sio kila kitu maishani.
 
View attachment 324142

Mara Nyingi Sana jina linaweza kuwa sababu ya wewe Kupenya ama Kukwama kwenye maisha. Baada ya matokeo ya Kidato cha Nne siku ya Jana Story kubwa ni Mchina aliye pata nafasi ya Pili kitaifa ambaye ni Mchina.

CongCong Wang ambaye amepata A tisa na B Moja Ya Kiswahili anasema Cong Maana yake ni Clever na Wang Maana yake ni King... So Jina lake lina maana Clever Clever King. Katika Mtihani wa Mock mkoa wa Dar alikuwa wa 2.

Alianza kusoma darasa la pili alipomaliza darasa la saba akaamua kuchagua NECTA badala ya Mfumo wa CAMBRIDGE sababu mfumo wa NECTA ni mgumu zaidi.

Kiswahili ni lugha yake ya 4 kujifunza anasikitika kupata B wakati MOCK alipata A.

Kati ya masomo aliyokuwa anafurahia zaidi ni somo la Historia ambalo mwalimu alikuwa anafundisha vizuri sana kama Movie.

Source: Clouds Media Group
Tumia akili yako vema. Umejiridhisha kwamba huyo ndo mchina pekee alifanya mtihani huo wa necta? Bila shaka jibu ni hapana! Sasa nenda utafute hao wengine wamekuwa wa ngapi? Sawa, private nyingi zimefanya vizuri Lakini hakuna pia private zilizofanya vibaya sana?!

Narudia kusema tumia akili yako VEMA
Tusitumie ufikiri mdogo kujustify mawazo duni!
 
Mkuu Jodeo mbona unanishambulia kwa matusi kiasi hicho?hii habari chanzo chake ni Clouds Media Group,Uungwana ni vitendo
 
Siwezi kunyamaza ninaposoma hoja ambazo ni za kitoto sana. Kuna kasumba Tanzania, kwamba mtu anayejua kingereza ndio mjanja, ni kasumba mbaya sana ndio maana baadhi ya watu wakishalewa wanaanza kuchomekea maneno ya kingereza. Kingereza sio kila kitu maishani.
Wewe mbishi...
 
Nimemsikiliza yule Mwanafunzi mchina , wakati anahojiwa, lakini kiswahili anacho ongea si kiswahili sahihi sana japo anajitahidi sana na ninapenda kumpongeza kwa kuiweka Tanzania ktk Ramani ya Dunia.

Mfano nimesikia akisema " watoto mengi", "nilitumia masaa nyingi" napata wasiwasi sana kwenye mfumo wetu wa Elimu na kujiuliza maswali yasiyo na majibu pengine.

1. Inawezekana mitihani ya sasa ivi ni kama ya kuchagua huhitaji kujua kila kitu. Au ni udhaifu wa mitihani yetu kwa kuwa haina mtihani wa kuongea japo sidhani kama ni muhimu sana kuwa na mtihani wa "oral"

2. Inawezekana wasahihishaji waliamua kupotezea baadhi ya makosa ambayo hayana athari kwenye tafsiri iliyokusudiwa na mwandishi.

3. Watoto wa sasa ivi wavivu kusoma hadi kupelekea asiye kiwezea vizuri kiswahili akifanya bidii anakuwa bora kuliko wale wanao kijua vizuri.

4. Je serikali imejiandaa vipi kupambana na matumizi ya fedha kwenye usahihishaji wa mitihani au wizi wa mitihani ( sina maana mchina kaiba)

5. Angeongeza bidii kidogo angepata A kali kabisa.

Je tinajifunza nini hapa?

Sina maana amependelewa. Naheshimu bidii yake na natambua kuwa ni mwanafunzi mwenye akili sana.
 
Sidhani kama hapa kwetu huwa kunakuwa na mtihani wa 'oral', na kama nipo sahihi saana huwa wanafanya mtihani wa 'kuandika' pekee. Na uzuri wa mtihani wa lugha, unaweza usijue namna nzuri ya kulitamka neno kwa ufasaha lakini, ukaweza kuliandika ufasaha.
 
Dah....kweli watu tunatofautiana mimi kitambo hicho D ya Kiswahili nafurahi kukimbia penalti kulinda kijiti changu cha 11 mchina kaweka B Duh..Hongera zake Binti wa Kichina
 
Tuhuma za fedha kutumika kuhonga wasimamizi na walinzi wakati wa mitihani, hasa kwenye shule binafsi, awamu hii ya utumbuaji majipu izifanyie kazi.
 
Back
Top Bottom