Nimemsikiliza yule Mwanafunzi mchina , wakati anahojiwa, lakini kiswahili anacho ongea si kiswahili sahihi sana japo anajitahidi sana na ninapenda kumpongeza kwa kuiweka Tanzania ktk Ramani ya Dunia.
Mfano nimesikia akisema " watoto mengi", "nilitumia masaa nyingi" napata wasiwasi sana kwenye mfumo wetu wa Elimu na kujiuliza maswali yasiyo na majibu pengine.
1. Inawezekana mitihani ya sasa ivi ni kama ya kuchagua huhitaji kujua kila kitu. Au ni udhaifu wa mitihani yetu kwa kuwa haina mtihani wa kuongea japo sidhani kama ni muhimu sana kuwa na mtihani wa "oral"
2. Inawezekana wasahihishaji waliamua kupotezea baadhi ya makosa ambayo hayana athari kwenye tafsiri iliyokusudiwa na mwandishi.
3. Watoto wa sasa ivi wavivu kusoma hadi kupelekea asiye kiwezea vizuri kiswahili akifanya bidii anakuwa bora kuliko wale wanao kijua vizuri.
Funzo kwa watz
Kumbe hata yale ambayo tunadhani hatuna maarifa ya kutosha tukiweka bidii tunaweza kushangaza Dunia.
Sina maana amependelewa. Naheshimu bidii yake na natambua kuwa ni mwanafunzi mwenye akili sana.