Anza kujifunza kwa Kuelezea Ray's theory ya maji naWeupe .Mie pia nasoma kitu na kukielewa lakini kukielezea kwa kuongea dah! Kiukweli huwa nashindwa, hata huyo mchina simshangai
Uko sahihi. Kitu ambacho baadhi ya GTs hawakijui ni kwamba lugha yo yote ni taaluma, yaani wanaoizamia wanajifunza sayansi yake - kinachoifanya kuwa njia ya kuwasiliana. Kwa hivyo Kiswahili na Kiinglish au Kiarabu ni taaluma (somo katika shule za msingi na sekondari, na uwanja maalumu katika vyuo vikuu). Si kila mzungumzaji (native speaker) wa Kiswahii au Kiingereza anaweza kushinda mtihani wa Kiswahili au Kiingereza ngazi yo yote ile ya shule bila kujifunza au kusomea sayansi yake (isimu na fasihi). Kama ingekuwa ni rahisi namna hiyo basi vijana wa Kitanzania ambao Kiswahili ni lugha mama, wangekuwa wanapata A katika somo la Kiswahili. Kiswahili ni somo kama masomo mengine - ulijifunza sanyasai yake na ukaimudu hata kama wewe ni mchina, utapata A. Tunampongeza sana huyo binti wa Kichina. Huyu binti anatakiwa awe kielelezo kwa watoto wa Kitanzania kwamba ukifanya masomo yako kwa bidii, the limit is the sky!Mkuu kiswahili cha kuandika huumizi kichwa ni kama kujua hisabati, sarufi, kivumishi, nomino na mzizi mkuu wa neno baaaas biashara imeisha. Wapo wazungu wanafeligi somo la english je wajua hlo pia wapo wabongo ndo mamasta katika kunfuu. Ukibisha muulize Mkoroshokigoli
Umewahi kukutana na mtu anaandika essay iliyonyooka ila kuongea english ni broken? Kuna kitu kinaitwa craming unameza 4 exams kuelewa baadae.....[/QUO
Yaani!
Wapo wengi wanajua Kingereza cha kuandika tu lakini cha kuongea ni shida, hata yule mchina anajua Kiswahili cha maandishi lakini cha kuongea ni shiiiiiiiiiida.Umewahi kukutana na mtu anaandika essay iliyonyooka ila kuongea english ni broken? Kuna kitu kinaitwa craming unameza 4 exams kuelewa baadae.....
Hhizo halina Ubishi mkuu, wengi hawajui Kiswahili cha kuongea lakini cha maandishi darasani wanajua hata kwa English ndiyo hivyo hivyo wengi hawajui Kingereza cha kuongea lakini cha maandishi ni wakali sana.Unaweza kujua lugha ukashindwa kutamka maneno bali ukajua kuyaandika.
Watanzania wengi ni malimbukeni wanaamini kujua English ni ujanja hawathamini lugha ya Taifa matokeo yake mchina kawapa Somo zuri angalau sasa wataanza kujitambua na kuithamini Lugha ya Taifa.Mbona wabongo wanafumua A za kingereza, kifaransa na kiarabi hamshangai
Ni kutokana na kutoithamini Lugha yetu na kuamini kuwa English ni bora kuliko KiswahiliUmeishajiuliza shule nzima wanafunzi wanaongea kiswahili inakuaje wengine wanapata F.
kiswahili cha darasani kile cha mitaala kina utofauti kidogo na Kiswahili cha Mtaani hivyo ni rahisi kwa mwanafunzi kufaulu pasipo kujua kutamka vyema Maneno pindi akiwa anaongea, wengi hawajuia Kiswahili cha kuongea lakini cha kuandika ni hodari wakubwa.Nimemsikiliza yule Mwanafunzi mchina , wakati anahojiwa, lakini kiswahili anacho ongea si kiswahili sahihi sana japo anajitahidi sana na ninapenda kumpongeza kwa kuiweka Tanzania ktk Ramani ya Dunia.
Mfano nimesikia akisema " watoto mengi", "nilitumia masaa nyingi" napata wasiwasi sana kwenye mfumo wetu wa Elimu na kujiuliza maswali yasiyo na majibu pengine.
1. Inawezekana mitihani ya sasa ivi ni kama ya kuchagua huhitaji kujua kila kitu. Au ni udhaifu wa mitihani yetu kwa kuwa haina mtihani wa kuongea japo sidhani kama ni muhimu sana kuwa na mtihani wa "oral"
2. Inawezekana wasahihishaji waliamua kupotezea baadhi ya makosa ambayo hayana athari kwenye tafsiri iliyokusudiwa na mwandishi.
3. Watoto wa sasa ivi wavivu kusoma hadi kupelekea asiye kiwezea vizuri kiswahili akifanya bidii anakuwa bora kuliko wale wanao kijua vizuri.
4. Je serikali imejiandaa vipi kupambana na matumizi ya fedha kwenye usahihishaji wa mitihani au wizi wa mitihani ( sina maana mchina kaiba)
5. Angeongeza bidii kidogo angepata A kali kabisa.
Je tinajifunza nini hapa?
Sina maana amependelewa. Naheshimu bidii yake na natambua kuwa ni mwanafunzi mwenye akili sana.
Kwani mmakonde inakuwaje anashindwa kuitamka m na msukuma anashindwa kusema road na anasema load?Samahan wakuu...unawezaje ukaandika halafu ukashindwa kuongea??
Kuongea sio sawa na kuandika,japo unayoyaandika ndio unayoyatamkaNimemsikiliza yule Mwanafunzi mchina , wakati anahojiwa, lakini kiswahili anacho ongea si kiswahili sahihi sana japo anajitahidi sana na ninapenda kumpongeza kwa kuiweka Tanzania ktk Ramani ya Dunia.