Mchakato wa uanzishaji wa Taasisi ya Uzalendo na Malezi Tanzania (TUMT)

Mchakato wa uanzishaji wa Taasisi ya Uzalendo na Malezi Tanzania (TUMT)

Joined
Apr 27, 2025
Posts
2
Reaction score
0
TAARIFA RASMI | MCHAKATO WA KUANZISHA TAASISI YA KITAIFA YA UZALENDO NA MALEZI TANZANIA (TUMT)

Kwa mujibu wa haja ya dharura ya taifa katika kujenga msingi imara wa maadili, uzalendo wa kweli, na malezi chanya ya kizazi kijacho, Klabu ya Uzalendo Wilaya ya Kibaha imeanza rasmi mchakato wa kuanzisha Taasisi ya Kitaifa ya Uzalendo na Malezi Tanzania (TUMT).

Taasisi hii inalenga kuwa chombo makini, endelevu na cha kitaifa, kitakachoshughulika na tafiti, mafunzo, sera, na program za kijamii zinazojikita katika kuimarisha utu, uzalendo wa vitendo, na kulea viongozi waadilifu wa kesho.

MAONO YA TAASISI: Kujenga jamii ya Watanzania wenye uzalendo hai, maadili mema, na dhamira ya dhati ya kuchangia maendeleo ya taifa.

MALENGO MAHUSUSI:

1. Kukuza elimu ya uzalendo na maadili katika ngazi zote za jamii.

2. Kutoa miongozo ya kitaifa ya malezi yenye muktadha wa kitanzania.

3. Kukuza na kuendeleza vipaji vya vijana kwa misingi ya maadili, utaifa na uwajibikaji.

4. Kuanzisha makongamano, mijadala ya kitaaluma, na tafiti kuhusu malezi, uzalendo na uongozi.

5. Kuwezesha ushirikiano kati ya serikali, taasisi za elimu, asasi za kiraia na sekta binafsi katika kujenga utamaduni wa kizalendo.

6. Kusaidia watoto walioathiriwa na changamoto za ukosefu wa malezi bora katika familia.

MSINGI WA KIPEKEE WA TAASISI HII: NIPAN itakuwa taasisi huru, ya kitaaluma, na ya kimaadili, inayojengwa juu ya msingi wa ushirikiano wa sekta zote za kijamii. Dira yake ni kuhakikisha kizazi kijacho kinalelewa katika misingi ya uadilifu, uzalendo, na nidhamu ya kitaifa.

WITO WA USHIRIKIANO:

Klabu ya Uzalendo Wilaya ya Kibaha inatoa wito kwa:

Wasomi na watafiti,

Viongozi wa taasisi za elimu,

Wadau wa maendeleo ya vijana,

Asasi za kiraia na mashirika ya kitaifa/kimataifa,

kuungana katika kuunga mkono wazo hili la kimkakati lenye lengo la kuhakikisha Tanzania inakuwa na jamii inayojitambua, inayojielekeza, na inayowajibika kwa taifa lake.

Imetolewa na:
Klabu ya Uzalendo – Wilaya ya Kibaha
Arafati Y. Kilongola, Mwenyekiti
Simu: 0622 953 678
0629 426 537 (WhatsApp)

#TUMT
#MaadiliNaUzalendo
#MaleziBoraNiNguzoYaMaendeleo
#TanzaniaYaKizalendo
#UzalendoClubTanzania
 
Back
Top Bottom