Tusizunguke, kuna kaugomvi fulani wachaga kwa wachaga ka kubaguana
Tulikuwa mkoa fulani kikazi na tukana na vijana wawili wa kichaga ambao walikuwa co workers. Ikatokea mmoja alifiwa na mzazi wake aliyekuja kumtembelea, katika kikao tukaamua tuunde timu ya kusindikiza, ingawa sisi tuliwaona wote wachanga lakini wao licha ya kujisikia hivyo hawakuwa wanakaribiana sana labda kwa sababu ya asili zao wa kwao ingawa hawakuonyesha wazi kwetu, tulichukulia kitu cha kawaida tu.
Tulipoanza msafara wa kwenda huko mimi nikiwa mmojawapo, tulikuja kushtushwa tulipofika Moshi mjini tukisubira ndugu wa upande wa mfiwa waje tuanze msafara kuelekea kijijini huko kwao Machame, tukashuhudia vijana wale wanaanza kuzozana kichaga ambacho sisi hatukijui. Baada ya kufika wale ndugu wa mfiwa kabla ya kuanza safari kijana yule wa kichaga aliyemsindikiza mwenzake alitoweka baada ya ugomvi ule na mwenzake, basi tukaendelea na msafara huku tukifikiria tusiojua ya wachaga movie ile iliyotokea.
Huko msibani hutakosa kunasa mawili matatu ya matukio yale, mmoja aliyeshuhudia hilo akiwa ndiye mchanga pia wa kutoka eneo tofauti alituambia kuwa kilichotokea ni sababu ya tofauti zao za kikabila, huko nje ya Moshi tunaonekana sote wachaga, lakini tukishafika hapa tofauti zetu zinakuwa wazi. Yule kijana mwenzake aliyeamua kutofuatana naye ni wa kutoka Uru. Nimekuja ambiwa tena na watu kadhaa hadi nikakiri jambo hili lipo na si uzushi.
Siku moja tunatoka safari ya Arusha kufika Moshi mjini tulishuhudia maiti barabarani watu wameizunguka, tulipokaribia na kushuhudia nini kimetokea, watu walikuwa wanaichunguza maiti ile kwa kuchukua kijiti kufungua mdomo wa maiti na kuona meno, kisha wanataja ni mchaga wa maeneo gani na kwamba huyo anatoka sehemu ya wachaga wezi na wizi sana, na kitambulisho ni meno yake. Sisi wengine tulibaki tumeduwaa na mambo yao. Tukaendelea na safari huku tukiwa na story za habari hiyo, kwa bahati pale ndani kwenye msfara gari tuliyosafiria dereva alikuwa mchaga, alitupa mengi ambayo yanaakisi ukweli wa mleta mada.