Ndugu wa 'mume' wa Ufoo waja na mapya

Ndugu wa 'mume' wa Ufoo waja na mapya

Shadow

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2008
Posts
2,897
Reaction score
679
Ndugu wa mume waja na mapya

09:49

NA JESSICA KILEO
FAMILIA ya aliyekuwa mzazi mwenzake, Mwandishi wa ITV na Radio One, Ufoo Saro, Anthery Mushi (40), imevunja ukimya na kudai inapata wakati mgumu kuamini kwamba ndugu yao alijiua mwenyewe.

Imesema suala hilo inaliachia Jeshi la Polisi lishughulikie ili kubaini undani wake.

Kaka wa marehemu, Isaya Mushi alidai hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), wawakati mwili wa Mushi, aliyejiua kwa kujipiga risasi na kumuua mama mkwe wake, Anastazia Saro pamoja na kumjeruhi mchumba wake Ufoo, ukiagwa.

Mushi alidai wapo katika wakati mgumu wa kuamini kwamba ndugu yao alijiua mwenyewe, kwani haiwezekani mtu akajipiga risasi sehemu mbili ambazo ni kidevuni na upande wa bega la kushoto.

Alidai sio kazi yao kutoa hukumu, kwani wanasubiri upelelezi wa polisi kutoa jibu lililo sahihi kuhusiana na tukio hilo.

Baada ya kifo cha ndugu yetu, wanafamilia tulifanya uchunguzi wa awali na bado linatuwia vigumu kutambua upi ni ukweli kuhusu jambo hilo kuhusiana na kifo hiki,î alidai.

Kaka huyo alidai katika uchunguzi wa madaktari, walibaini kuwa marehemu alijipiga risasi mbili sehemu tofauti.

Akisoma risala kwa waombelezaji, Mushi alidai marehemu alizaliwa Januari 3, 1973 katika kijiji Uru Ongoma Timbirini wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro.

Mushi alisema alisoma Shule ya Msingi Ongoma Timbirini kutoka mwaka 1981 hadi 1987 na alijiunga na Shule ya Sekondari ya Zanzibar na baadaye alisoma kozi mbalimbali, ikiwemo uandishi wa habari.

Alisema mwaka 1994 alijunga na Kituo cha Televisheni cha ITV na mwaka 2002 alikwenda STR na hadi mauti inamkuta alikuwa akifanya kazi Umoja wa Mataifa, Sudan, akiwa mtaalamu wa habari.

Kwa upande wake, dada wa marehemu, Eviolatha Mushi alisema alipokea kwa masikitiko msiba wa mdogo wake kwa sababu alikuwa mtu mwelewa na msikivu katika jamii ambayo wamekulia.

Eviolatha alitoa wito kwa wanandoa kumshirikisha Mungu katika maisha yao na sio mwanadamu, hali itakayosaidia kutatua matatizo wanayopitia kwa kuwa neno la Mungu linasema kila mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke lazima atalamba mauti, hivyo hawana budi kukubaliana na neno hilo.

Naye, mdogo wa marehemu, Happy Mushi, alisema hadi sasa hawezi kuamini chochote hadi polisi itakapotoa majibu ya upelelezi .

Alisema Oktoba 9, mwaka huu, marehemu alimpigia simu na kumwambia anamshukuru Mungu, kwani ametoka kufanya kazi katika mazingira magumu, hivyo muda si mrefu anaweza kuhamia Tanzania, na kwamba yupo nchini kwa ajili ya kumalizia nyumba yake ambaye ipo Mbezi, Dar es Salaam.

Lakini cha kushangaza kabla ya wiki alisikia katika vyombo vya habari vikitangaza kaka yake amejiua mwenyewe pamoja na familia ya mke wake,î alisema.

Mwili wa marehemu ulisafirishwa jana kwenda kijijini kwao Ongoma Timbirini na unatarajiwa kuzikwa leo.

Wakati huo huo, Ufoo aliyelazwa Muhimbili hali yake imetengemaa na ameanza kutembea pamoja na kwamba daktari anayemhudumia anakataza watu kuingia kumtazama.

Ofisa wa Habari wa MNH, Aminiel Eliegaisha, alisema jana kuwa, Ufoo anaendelea vizuri na ameanza mazoezi ya kutembea, ingawa bado hawajaanza kuwaruhusu watu kwenda kumtaza kwa sababu ameshonwa sehemu nyingi na kwamba wanahofia kidonda kutokupona haraka.

Tukio hilo la mauaji lilitokea Oktoba 13, mwaka huu, eneo la Kimbamba nyumbani kwa wazazi wa Ufoo, ambapo alikwenda akiwa na mzazi mwenzake Anthery Mushi.

Mushi alimuua mama wa Ufoo kwa kumpiga risasi zinazosadikika tano na kumjeruhi kabla ya kujiua mwenyewe.


source: Uhuru Online
 
Na kweli katika hali ya kawaida mtu hawezi kujipiga risasi mara mbili !!"" kunahitajika kufanyika kitu zaidi ya uchunguzi.
 
...ETHICAL case....anayejua tatizo ni Ufoo mwenyewe, sie tutabaki kupiga TARARIRAAAA ili mradi genge lichangamkeee....hata atakapokuja kuueleza uma yaliyojiri hatasema yote...Kila mtu ana yake moyoni (hata ninavyoandika nina yangu moyoni na hakuna hata mahali nimeshawahi vujisha even kwa rafiki zangu wa karibu (intimate/close friend(s))...

FIKIRI yako na Si ya mwenzio

Image0001.jpg
 
Mh,Ufoo kweli yamekukuta.uchunguzi wa polisi uwe wa kweli,kama Ana kesi ya kujibu apandishwe kizimbani na iwe funzo kwa wengine.
 
kwwani hapo nyumbani kwa Ufo hapakuwa na watu/mtu mwingine,?!, naye aje atueleze aliona na alifanya nini.
 
Nakweli haya ni mapya..

Nikama tuhuma zinaelekezwa kwa ufoo!!?..

Anaweza kumuua mama yake pia!!!?

Mmmh.?!?!!
 
Nasikitika sana

Yule mtoto wa marehemu ataishi kwa namna ya simanzi kubwa sana na sijui atawachukuliaje wanawake

sad part ni shina la ugomvi kuwa mali za kupita tu... tulizaliwa uchi, tunazikwa na nguo ambazo si ajabu hatujachagua... na makaburi tunapangiwa pia

bad stuff Ufoo..... bad stuff,

DAMU YA MTU HAIENDI BURE
 
Kunawezekana kwamba kulikuwa na mtu/watu watu wengine katika hiyo nyumba, sizani kama marehemu bibi angekuwa anaishi mwenyewe.

Ukweli utatoka mizimu ikianza kuwasumbua siku moja.

Ila hiyo risasi za sehemu alizotaja wow ni kama vile mtu alimpiga na kumkosa moja na kummalizia. Mbona tangu mwanzo wanasema risasi moja na shaiddi jirani alisema alisikia mlio mmoja, inakuwaje anatundu 2 marehemu?

Hapa lazima upande wa ufoo watataka kuficha maan ndio Kaka wa watu labda hata alikuta hati imewekwa kwa jina la demu na familia. Kamwe hawatasema ukweli.

Ila I hope polisi wanajua cha kufanya na kuangalia damu ilirukaje etc kama mtu alikuwa mbali au karibu au yeye. Na mengineyo mengi

RIP wote
 
Nakweli haya ni mapya..

Nikama tuhuma zinaelekezwa kwa ufoo!!?..

Anaweza kumuua mama yake pia!!!?

Mmmh.?!?!!

inawezekana stearing alikosea kutekeleza maelekezo.
 
Mbona linaelezeka kirahisi tu. Katika hali ya tukio hilo kuna uwezekano mkubwa kuwa kulikuwapo purukushani ya kujaribu kuzuia au kunyang'anyana hiyo silaha baada ya kumpiga mama mkwe. Purukushani hiyo inaweza kuelezea hiyo risasi ya begani. Baada ya huyo mwananume kupata tena udhibiti wa silaha yake, ndio akapata nafasi ya kumshambulia Ufoo na kudhani ameshawauwa wote wawili. Baada ya hapo, akajipiga risasi chini ya kidevu ili kujimaliza. Kama polisi wapo makini, sio kazi ngumu sana kubaini ni silaha ngapi/gani zilitumika katika tukio hilo. Hata hivyo, Ufoo anabaki kuwa shahidi muhimu sana katika tukio hili. Na ni kweli pia kuwa kuna uwezekano wa kuwepo kwa mambo mengi tu yaliyojificha kuhusiana na kadhia hii.
 
Hiyo mimba aliyonayo Ufo ni ya nani! Ndio beneficiary wa kadhia hii!
 
mi nafikiri police watakuja na ukweli mana hili jambo litakuwa limeanza siku nyingi mpaka kufikia hapo wata tress mazungumzo yao ya simu zao meseji zao na uzuri jamaa alikuwa nje lazma walikuwa wanawasiliana kwa mitandao.
Ukweli utajulikana tu
 
Hawa wachagga ovyo sana, ndiyo mama yangu alinikataza nisimchumbie Mmachame wanahusudu sana kitu kuliko utu! ona sasa tamaa yake ya kumdhurumu nyumba mzazi mwenzake ilivyomtokea puani! kampoteza mama na yeye kutokea tundu ya sindano! wapuuz sana hawa

Mkuu utatutoa katika mada maana kuna thread zao zipo nyingi ukitaka zitafute. Back to the Topic,,how come mtu ukajipiga risasi ya Bega na kichwa we mwenyewe kama kweli ulikuwa na lengo la kujiua si ungejipiga moja tu ya kichwa.
 
Back
Top Bottom