Mchaga wa Uru na wa Machame hawafungamani

Mchaga wa Uru na wa Machame hawafungamani

Nakubaliana na wewe kwa kiasi fulani ingawa sio sana
Kipindi cha Mangi Sina(mangi wa kibosho) kulikuwa na ugomvi mkubwa wa ardhi. Hivyo vita kati ya Machame na Kibosho ilikuwa kawaida sana. Katika tawala za wakati huo Mangi alikuwa anawaangalia vijana na alikuwa anawateua toka miongoni mwa vijana wa ukoo wa kimangi kwenda kusomea umangi kwa mangi wa jirani. Ilitokea kuwa Mangi Sina alisomea umangi na ujasiri kwa mangi wa machame mangi Shangali kama sikosei. So Mangi Sina aliwajua Wamachame vilivyo. Baada ya yeye Sina kutawazwa kuwa mangi alianza mikakati ya kudhoofisha jeshi la mangi wa machame. Siku moja aliunda mbinu! Alijitangazia kufa! Walichinja ngombe na kwa usiri mkubwa waliweka umbo la mtu kwa kutumia ngozi ya ngombe! Baada ya muda ile ngozi ilianza kuzingwa na nzi. Wapelelezi wa kimachame hawakufanya utafiti wa kutosha hivyo waliamini kuwa kweli Mangi Sina amefariki. Walianza kujipanga kuvamia Kibosho. Wakati huo jeshi la kibosho lilikuwa limejiandaa vilivyo. Walizingira eneo fulani lililokuwa mapito ya askari wa Machame. Kwa wale wa Kibosho Umbwe na Lyamungo wanajua eneo linaitwa Mashangala! Eneo hilo lilikuwa na aina fulani ya kitu kuzama yaani TINDIGA. Siku jeshi la machame linapanga kuvamia kibosho, Jeshi la kibosho lilishajipanga hivyo walivyojua kuwa sasa jeshi la machame liko katikati yao waliwavamia toka pande zote hivyo kuwachanganya askari wa machame hivyo kuwa rahisi kwa askari wa kibosho kuwaswaga kuelekea Mashangala. Kwa kweli wengi wa askari wa machame walizama mashangala na waliosalia nao waliuwawa kikatili. Kwa wale waliookoka ndio waliotoa ushuhuda. Kuanzia wakati huo ukawa ndio mwanzo wa uhasama mkubwa kati ya jamii hizo. Nyumba ya kibosho ikijengwa mlango unaangalia magharibi! Ya mmachame mlango magharibi. Uhasama umeendelea kwa miongo kadhaa. Kwa hakika tunashuhudia mabadiliko makubwa sana. Kaka yangu kaoa machame na nakubalika mbaya kabisa. Mimi nina rafiki yangu mpendwa Mmachame! Yaani watu hufikiri sisi ni ndugu! Watoto wanafunga shule wanaamua wanaenda wapi? Wacha trip zetu na familia. Mama zetu mashoga wakubwa na sisi ndio tumewaunganisha. Jamani nawahakikishia kizazi cha visasi hakipo tena kati ya jamii hizi 2, na kama kipo kiliathirika kwa kiwango kikubwa. Imebakia kuwa historia tu! Sisi ni ndugu! And thats what I know. I stand to be corrected.
Eeka Mangi

binafsi mimi ni mchaga wa machame,
Wachaga tuko hivi, hakuna ubaguzi dhidi yetu ila tu, kuna miiko ambayo iko na si kwa nia ya kutuondolea umoja wetu. Lugha zetu ni tofauti kwa kila aina ya mchaga muuru, ataongea tofauti na mmachame ama msiha ama mrombo lkn mmarangu, oldmoshi, na Mkirua wote wanaongea kichaga cha aina moja. Kidogo mkibosho na mmachame wanaweza kusikilizana lkn nayo pia sio sana.

tuje kwenye mada yako iko hivi wachaga wote huoana isipokuwa mkibosho na mmachame tu, laana hii iliwekwa toka enzi za mambabu wakati wa utawala wa mangi kwamba, enzi za mangi wa Kibosho, aliwah kutok ana kupigana vita na Mangi wa Machame kisa wanagombea maeneo na eneo hilo sikumbuki vyema lilikuwa sijui ni eneo la mto WERUWERU sina hakika sana.

sasa ikatokea kwamba vijana wa kibosho walikuwa wanawaua vijana wa machame kwa ukatili sana yaani wanawachoma visu na kuwacharanga kama nyama, ndipo ikawekwa amini Mmachame asiolewe KIBOSHO wala asijenge nyumba kuangalia Kibosho.

Kwa macho yangu nimeshuhudia baadhi ya ndoa za mkibosho na mmachame zikiteseka ama kwa kupata watoto walemavu, ama kuuana, ama ugonjwa nk kwasababu ya mwiko uliowekwa, lkn pia nimeshuhudia hata waliokaidi na kujenga nyumba ikaelekea kibosho wakipata shida sana kwenye hizo nyumba hii ni kweli na haipingiki.

Ukivuka kibosho kwenda maeneo mengine yote iwe old mosh uru, vUNJO, Kilema, marangu, mwika, rombo hawa wanaoana pasi tatizo lolote unless kama familia kama famili ama ukoo kama ukoo una miiko yake.

Nasema ukoo kama ukoo kwasababu, Mushi ni ukoo mkubwa sana na kuna baadhi ya kaka zao wallizaa na dada zao lkn baada ya dada kuzaa walipatiwa maeneo mengine wakaish huko lkn koo zikabadilishwa kwasababu ilihesabika kwamba ni laana kukaa na mtoto wa dada nyumba moja. Mwiko uliowekwa kwenye watu kama hawa ni wasioane manake ni ndugu moja hivyo wakioana watapata laana. mfano hai tunaoweza kuuona ni kama vile Mushi hawaoi kwa Shoo, ama Massawe hawaoi kwa Shuma, ama kama vile mmachame hawezi kumuoa Msiha manake hawa ni dada na kaka kabisa walizaa na ukioa hapa umeoa dada yako mpaka ifanywe mila ya kuvunja undugu ndipo mnaweza labda kupata baraka za watoto.

Kuhusu case ya kwamba Mmchame na muuru hawaoani mimi binafsi naipinga kwani baba yangu mdogo kabisa ni mmachame wa hapa hapa Uduru ni loya mzuri na mkewe ni Muuru ni profesa wa watoto Prof Petronila Ngiloi, wanamaisha mazuri sana na watoto wanao tena waliosoma na maisha yao ni supa hivyo kwa maelezo haya wewe mtoa mada umepotoshwa na waliokuambia.
 
Last edited by a moderator:
Ndicho kilichompata Ufoo Saro na mpenzi wake marehemu Mushi. Uliza mchaga aliye karibu nawe atakupa details. Imagine marehemu Mushi hadi anajiua juzi alikuwa tayari na umri wa miaka 40, bado alikuwa anamsubiria Ufoo (licha ya kwamba walishazaa mtoto mmoja), tunaambiwa walikuwa wachumba! Inasemekana ni laana iliachwa na mababu tangu kale.
Poleni wafiwa. Ufoo ugua pole, ni mitihani ya dunia, amini Mwenyezi Mungu atakuvusha salama.

Hapo ndio kwenye jibu.
 
ingekuwa pouwa mkitoa comment huku mki-ahinisha makabila yenu pia.
:A S-rap:.

Mi mnyamwezi!
Sina matatizo na yyt!
Awe mchaga wa urru au machame au wa himo!
Kwangu woote ni meno meusi tu!
Sioni different yyt!
Teh teh teh teh!
 
Unaye ongea naye ni mchaga kindaki ndaki haswaa...Sasa mimi ninamifano halisi Wachagga wa sehemu zingine waliooana na Wamachame na maisha yanaenda vizuri tuu wala hamna tatizo......

Hakuna kitu kama iko,ukishaoa mchaga tayari ni tatizo....mzee wetu Mkapa wakati anaingia ikulu alikuwa Mr clean,sasa uliza kilitokea nini!! Mama mkapa alimwalibu kabisa...Uyu mama kwanza aliakikisha kila kitengo chenye hela anakaa mchaga mwenzie,,pili akamfundisha mkono mrefu kitu ambacho hakuwa nacho before mzee wetu mkapa..mwanamke wa kichaga acha tu.
 
Kaka naona hawa watu unawafahamu vizuri kuliko wanavyojifahamu wenyewe! japo wanajaribu kujibagua wenyewe kwa wenyewe duh! lakini umewaamulia leo!

Hawa watu mie nawafahamu vizuri mkuu,,unakuta Mangi katoka kibosho kaja mjini anashona viatu baada ya miaka mitatu ana bonge la hardware...ukianza kufatilia siri ya mafanikio ni nini kumbe wenzetu mchana fundi viatu usiku yupo kwenye magodauni anapiga,,baadae anajisifia sisi mafaita yani acha tu.
 
Mi ni MROMBO namshukuru mungu tunapiga popote. I am proud to be a chagga

lazima uwe proud kuwa mchaga mkuu,we ukienda Tra pale ukionyesha tu meno kuungua kwenye interview umepita..wengine wanaambiwa waache maneno wapige shule sasa jiulize inji hii mchaga tu ndio kasomea kuajiliwa tra.
 
Tusizunguke, kuna kaugomvi fulani wachaga kwa wachaga ka kubaguana
Tulikuwa mkoa fulani kikazi na tukana na vijana wawili wa kichaga ambao walikuwa co workers. Ikatokea mmoja alifiwa na mzazi wake aliyekuja kumtembelea, katika kikao tukaamua tuunde timu ya kusindikiza, ingawa sisi tuliwaona wote wachanga lakini wao licha ya kujisikia hivyo hawakuwa wanakaribiana sana labda kwa sababu ya asili zao wa kwao ingawa hawakuonyesha wazi kwetu, tulichukulia kitu cha kawaida tu.

Tulipoanza msafara wa kwenda huko mimi nikiwa mmojawapo, tulikuja kushtushwa tulipofika Moshi mjini tukisubira ndugu wa upande wa mfiwa waje tuanze msafara kuelekea kijijini huko kwao Machame, tukashuhudia vijana wale wanaanza kuzozana kichaga ambacho sisi hatukijui. Baada ya kufika wale ndugu wa mfiwa kabla ya kuanza safari kijana yule wa kichaga aliyemsindikiza mwenzake alitoweka baada ya ugomvi ule na mwenzake, basi tukaendelea na msafara huku tukifikiria tusiojua ya wachaga movie ile iliyotokea.

Huko msibani hutakosa kunasa mawili matatu ya matukio yale, mmoja aliyeshuhudia hilo akiwa ndiye mchanga pia wa kutoka eneo tofauti alituambia kuwa kilichotokea ni sababu ya tofauti zao za kikabila, huko nje ya Moshi tunaonekana sote wachaga, lakini tukishafika hapa tofauti zetu zinakuwa wazi. Yule kijana mwenzake aliyeamua kutofuatana naye ni wa kutoka Uru. Nimekuja ambiwa tena na watu kadhaa hadi nikakiri jambo hili lipo na si uzushi.

Siku moja tunatoka safari ya Arusha kufika Moshi mjini tulishuhudia maiti barabarani watu wameizunguka, tulipokaribia na kushuhudia nini kimetokea, watu walikuwa wanaichunguza maiti ile kwa kuchukua kijiti kufungua mdomo wa maiti na kuona meno, kisha wanataja ni mchaga wa maeneo gani na kwamba huyo anatoka sehemu ya wachaga wezi na wizi sana, na kitambulisho ni meno yake. Sisi wengine tulibaki tumeduwaa na mambo yao. Tukaendelea na safari huku tukiwa na story za habari hiyo, kwa bahati pale ndani kwenye msfara gari tuliyosafiria dereva alikuwa mchaga, alitupa mengi ambayo yanaakisi ukweli wa mleta mada.

hahahaha mkuu kumbe wanajuana ata kwa meno tu...ndio maana utakuta wengine meusii,wengine kama gold,,,wengine kama uchafu ivi kumbe ni ID.
 
Wapelestina ndiyo kina nani huwa namsikia rafiki yangu mmoja Mkibosho akimponda dada mmoja ananiambia achana naye Mpalestina.
 
wala sina ukatili, nipo kawaida tu, wachaga hatuna sifa hiyo.

kweli mkuu wachaga hamna ukatili??...wakati nchi ipo kwenye crisis kipindi cha Nyerere(rip) wasomi wa kichaga walimkimbia mzee wetu badala ya kumsaidia kipindi ambacho nchi iliwaitaji kuliko,,,wakiongozwa na mzee Edwin Mtei uyu mzee pamoja na kulipwa mshahara mkubwa kuliko rais kipindi hicho alitukimbia wakati wa matatizo watu wakila yanga Ye akaenda zake kuishi kifahari marekani....Leo hii wamerudi baada ya kuona siasa inalipa eti wanasema wanataka kutukomboa,hivi kuna mchaga ana uchungu na mmakonde,nndengereko au mhehe?usione tunasapoti mkuu,hatuna tu altenative
 
Last edited by a moderator:
matumbo hacha kusakama ndugu zetu Wachagga! Acha porojo zako zisizokuwa na msingi!

mkuu mie sisakami mtu,,naongea ukweli..au unabisha awa jamaa sio wabinafsi,wachoyo na mkono mrefu?!
wenyewe ata ukiwakuta jf utaona tu wanapeana mashavu sijui wanajuana vipi utaona wanalushana tu cc Heaven on earth cc nicas Mtey cc Preta cc Smile cc Nivea cc Ben Saanane cc Nicolaus cc Pdidy cc Nivea cc @gfson cc Philemon Mikael cc Bigirita cc Safety last cc JMUshi cc Frola Msoffe yani sijui wanajuana vipi tu
 
Last edited by a moderator:
Wapelestina ndiyo kina nani huwa namsikia rafiki yangu mmoja Mkibosho akimponda dada mmoja ananiambia achana naye Mpalestina.

mpalestina ni mmachame,,hatari hao.
 
Last edited by a moderator:
kweli mkuu wachaga hamna ukatili??...wakati nchi ipo kwenye crisis kipindi cha Nyerere(rip) wasomi wa kichaga walimkimbia mzee wetu badala ya kumsaidia kipindi ambacho nchi iliwaitaji kuliko,,,wakiongozwa na mzee Edwin Mtei uyu mzee pamoja na kulipwa mshahara mkubwa kuliko rais kipindi hicho alitukimbia wakati wa matatizo watu wakila yanga Ye akaenda zake kuishi kifahari marekani....Leo hii wamerudi baada ya kuona siasa inalipa eti wanasema wanataka kutukomboa,hivi kuna mchaga ana uchungu na mmakonde,nndengereko au mhehe?usione tunasapoti mkuu,hatuna tu altenative

matumbo,

Umefunguka balaa hawa jamaa mbona unawajua sana unaishi nao.
 
Last edited by a moderator:
matumbo,

Umefunguka balaa hawa jamaa mbona unawajua sana unaishi nao.

Nawafahamu vizuri sana sababu nimeishi nao na kufanya nao ishuz kibao...Wenyewe wananiona nuksi kweli leo,wanachungulia thread wanakimbia.
 
Last edited by a moderator:
Mleta mada ni mkweli. Kuna historia ya mauwaji kati ya mmachame na muuru. Hata muuru alikuwa akijenga nyumba milango haiwekwi kutazama upande wa machame. Inawezakana wapo wanaoishi pamoja bila tatizo ila hujui kesho na pia kuzidisha maombi ni muhimu sana. Nitagoogle kitabu cha mangi marealle lazima atakuwa ameyaelezea hayo kwa ufasaha zaidi.
 
mkuu mie sisakami mtu,,naongea ukweli..au unabisha awa jamaa sio wabinafsi,wachoyo na mkono mrefu?!
wenyewe ata ukiwakuta jf utaona tu wanapeana mashavu sijui wanajuana vipi utaona wanalushana tu cc Heaven on earth cc nicas Mtey cc Preta cc Smile cc Nivea cc Ben Saanane cc Nicolaus cc Pdidy cc Nivea cc @gfson cc Philemon Mikael cc Bigirita cc Safety last cc JMUshi cc Frola Msoffe yani sijui wanajuana vipi tu

we matumbo mbona unajifanya unatujua sana...ukimaliza kutudiscuss

kakojoe ulale...

cc Asprin huyo ulimsahau pia ngoja nimrushe nae
 
Last edited by a moderator:
Ndicho kilichompata Ufoo Saro na mpenzi wake marehemu Mushi. Uliza mchaga aliye karibu nawe atakupa details. Imagine marehemu Mushi hadi anajiua juzi alikuwa tayari na umri wa miaka 40, bado alikuwa anamsubiria Ufoo (licha ya kwamba walishazaa mtoto mmoja), tunaambiwa walikuwa wachumba! Inasemekana ni laana iliachwa na mababu tangu kale.
Poleni wafiwa. Ufoo ugua pole, ni mitihani ya dunia, amini Mwenyezi Mungu atakuvusha salama.

mbona we laana yako huisemi...uko tu kuidscuss ya Mushi...

Inasemekana..inasemekana..inaasemekana ....Insemekana...hamna hata uhakika mmekalia inasemekanaa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom