nimekumiss
Kiongozi nilichokiandika nimekipata kutoka kwa mchaga mtu mzima na nimefuatilia kwa wengine wawili watatu wote wanasema hivyo. Kuhusu hiyo ndoa ya wazazi wako, chunguza vizuri utasikia kuna tambiko walifanya kuzuia laana hiyo. Tena kama ni wa miaka 30 iliyopita lazima walifanya tambiko la ukweli haswa maana miaka hiyo imani hiyo ilikuwa na nguvu labda kuliko leo.
Nakubaliana na wewe kwa kiasi fulani ingawa sio sana
Kipindi cha Mangi Sina(mangi wa kibosho) kulikuwa na ugomvi mkubwa wa ardhi. Hivyo vita kati ya Machame na Kibosho ilikuwa kawaida sana. Katika tawala za wakati huo Mangi alikuwa anawaangalia vijana na alikuwa anawateua toka miongoni mwa vijana wa ukoo wa kimangi kwenda kusomea umangi kwa mangi wa jirani. Ilitokea kuwa Mangi Sina alisomea umangi na ujasiri kwa mangi wa machame mangi Shangali kama sikosei. So Mangi Sina aliwajua Wamachame vilivyo. Baada ya yeye Sina kutawazwa kuwa mangi alianza mikakati ya kudhoofisha jeshi la mangi wa machame. Siku moja aliunda mbinu! Alijitangazia kufa! Walichinja ngombe na kwa usiri mkubwa waliweka umbo la mtu kwa kutumia ngozi ya ngombe! Baada ya muda ile ngozi ilianza kuzingwa na nzi. Wapelelezi wa kimachame hawakufanya utafiti wa kutosha hivyo waliamini kuwa kweli Mangi Sina amefariki. Walianza kujipanga kuvamia Kibosho. Wakati huo jeshi la kibosho lilikuwa limejiandaa vilivyo. Walizingira eneo fulani lililokuwa mapito ya askari wa Machame. Kwa wale wa Kibosho Umbwe na Lyamungo wanajua eneo linaitwa Mashangala! Eneo hilo lilikuwa na aina fulani ya kitu kuzama yaani TINDIGA. Siku jeshi la machame linapanga kuvamia kibosho, Jeshi la kibosho lilishajipanga hivyo walivyojua kuwa sasa jeshi la machame liko katikati yao waliwavamia toka pande zote hivyo kuwachanganya askari wa machame hivyo kuwa rahisi kwa askari wa kibosho kuwaswaga kuelekea Mashangala. Kwa kweli wengi wa askari wa machame walizama mashangala na waliosalia nao waliuwawa kikatili. Kwa wale waliookoka ndio waliotoa ushuhuda. Kuanzia wakati huo ukawa ndio mwanzo wa uhasama mkubwa kati ya jamii hizo. Nyumba ya kibosho ikijengwa mlango unaangalia magharibi! Ya mmachame mlango magharibi. Uhasama umeendelea kwa miongo kadhaa. Kwa hakika tunashuhudia mabadiliko makubwa sana. Kaka yangu kaoa machame na nakubalika mbaya kabisa. Mimi nina rafiki yangu mpendwa Mmachame! Yaani watu hufikiri sisi ni ndugu! Watoto wanafunga shule wanaamua wanaenda wapi? Wacha trip zetu na familia. Mama zetu mashoga wakubwa na sisi ndio tumewaunganisha. Jamani nawahakikishia kizazi cha visasi hakipo tena kati ya jamii hizi 2, na kama kipo kiliathirika kwa kiwango kikubwa. Imebakia kuwa historia tu! Sisi ni ndugu! And thats what I know. I stand to be corrected.
Eeka Mangi
Ndicho kilichompata Ufoo Saro na mpenzi wake marehemu Mushi. Uliza mchaga aliye karibu nawe atakupa details. Imagine marehemu Mushi hadi anajiua juzi alikuwa tayari na umri wa miaka 40, bado alikuwa anamsubiria Ufoo (licha ya kwamba walishazaa mtoto mmoja), tunaambiwa walikuwa wachumba! Inasemekana ni laana iliachwa na mababu tangu kale.
Poleni wafiwa. Ufoo ugua pole, ni mitihani ya dunia, amini Mwenyezi Mungu atakuvusha salama.
umeshatoa mkono sweta wako. Ni muhimu kwa afya yako.
Hebu tuambie kabila lako.
mkuu matumbo unachafua hali ya hewa hapa jukwaani
usitumie kichwa kama mwamvuli wa kijikimgia mvua
jaribu kufikiri hata kidogo tu.
mkuu punguza jazba kidogo