Mchaga wa Uru na wa Machame hawafungamani

mkuu usipotoshe, mimi ni mchaga, baba wa machame mama wa uru.
Wameoana takriban miaka 30 ilopita na bado wako pamoja.

Tatizo ndo za vijana wa leo haziendi bila uzinzi, mzini kwanza ndio muoane.
Hiyo baraka ya Mwenyezi Mungu itatoka wapi?
Unakuta watu ni wachumba lkn wana mtoto/watoto tayari. Hayo ni mafundisho ya wapi kama sio laana?

Acha ubinafsi, bataka ya mwenyezi Mungu ndio nini?

msome peri kwenye red alimaanisha nini na wewe umeandika nini.
je kati yako na yeye nani asiyeeleweka??
ukikurupuka basi kurukupa ukiwa na akili timamu usiache utimamu wa mwili kwingine
 
Last edited by a moderator:
Wewe inaelekea hujawahi kufika hata Moshi mjini. Hebu wachagga mlioko humu kuweni wakweli. Kuna wachagga wanaoonekana wachagga kuliko wachagga. Huku mjini tunawaona wanavyopuuzana na kudharauliana. Hapa Arusha kuna vyama vya kikabila vya kusaidiana katika matatizo, vya wachagga vimegawanyika kama ulivyotaja hapo juu, na hawakubali kwa mfano marangu kukaribishwa kwenye chama cha Kibosho. Na ukisikia yanayozungumzwa na wachagga wa sehemu fulani dhidi ya wachagga wa sehemu nyingine huwezi kuaamini wote ni wachagga. Dhambi ya ubaguzi inawatafuna. Mmachame na muuru, kwa mujibu wa makabila haya mawili yanavyochukuliana, hawawezi kamwe kuishi nyumba moja kama mke na mume. Hilo uliza popote uchaggani utapata jibu hilo.

binafsi mimi ni mchaga wa machame,
Wachaga tuko hivi, hakuna ubaguzi dhidi yetu ila tu, kuna miiko ambayo iko na si kwa nia ya kutuondolea umoja wetu. Lugha zetu ni tofauti kwa kila aina ya mchaga muuru, ataongea tofauti na mmachame ama msiha ama mrombo lkn mmarangu, oldmoshi, na Mkirua wote wanaongea kichaga cha aina moja. Kidogo mkibosho na mmachame wanaweza kusikilizana lkn nayo pia sio sana.

tuje kwenye mada yako iko hivi wachaga wote huoana isipokuwa mkibosho na mmachame tu, laana hii iliwekwa toka enzi za mambabu wakati wa utawala wa mangi kwamba, enzi za mangi wa Kibosho, aliwah kutok ana kupigana vita na Mangi wa Machame kisa wanagombea maeneo na eneo hilo sikumbuki vyema lilikuwa sijui ni eneo la mto WERUWERU sina hakika sana.

sasa ikatokea kwamba vijana wa kibosho walikuwa wanawaua vijana wa machame kwa ukatili sana yaani wanawachoma visu na kuwacharanga kama nyama, ndipo ikawekwa amini Mmachame asiolewe KIBOSHO wala asijenge nyumba kuangalia Kibosho.

Kwa macho yangu nimeshuhudia baadhi ya ndoa za mkibosho na mmachame zikiteseka ama kwa kupata watoto walemavu, ama kuuana, ama ugonjwa nk kwasababu ya mwiko uliowekwa, lkn pia nimeshuhudia hata waliokaidi na kujenga nyumba ikaelekea kibosho wakipata shida sana kwenye hizo nyumba hii ni kweli na haipingiki.

Ukivuka kibosho kwenda maeneo mengine yote iwe old mosh uru, vUNJO, Kilema, marangu, mwika, rombo hawa wanaoana pasi tatizo lolote unless kama familia kama famili ama ukoo kama ukoo una miiko yake.

Nasema ukoo kama ukoo kwasababu, Mushi ni ukoo mkubwa sana na kuna baadhi ya kaka zao wallizaa na dada zao lkn baada ya dada kuzaa walipatiwa maeneo mengine wakaish huko lkn koo zikabadilishwa kwasababu ilihesabika kwamba ni laana kukaa na mtoto wa dada nyumba moja. Mwiko uliowekwa kwenye watu kama hawa ni wasioane manake ni ndugu moja hivyo wakioana watapata laana. mfano hai tunaoweza kuuona ni kama vile Mushi hawaoi kwa Shoo, ama Massawe hawaoi kwa Shuma, ama kama vile mmachame hawezi kumuoa Msiha manake hawa ni dada na kaka kabisa walizaa na ukioa hapa umeoa dada yako mpaka ifanywe mila ya kuvunja undugu ndipo mnaweza labda kupata baraka za watoto.

Kuhusu case ya kwamba Mmchame na muuru hawaoani mimi binafsi naipinga kwani baba yangu mdogo kabisa ni mmachame wa hapa hapa Uduru ni loya mzuri na mkewe ni Muuru ni profesa wa watoto Prof Petronila Ngiloi, wanamaisha mazuri sana na watoto wanao tena waliosoma na maisha yao ni supa hivyo kwa maelezo haya wewe mtoa mada umepotoshwa na waliokuambia.
 
Last edited by a moderator:
mkuu usipotoshe, mimi ni mchaga, baba wa machame mama wa uru.
Wameoana takriban miaka 30 ilopita na bado wako pamoja.

Tatizo ndo za vijana wa leo haziendi bila uzinzi, mzini kwanza ndio muoane.
Hiyo baraka ya Mwenyezi Mungu itatoka wapi?
Unakuta watu ni wachumba lkn wana mtoto/watoto tayari. Hayo ni mafundisho ya wapi kama sio laana?

Acha kukalili kwa imani za kuja na boti...hao babu zako waliozaa bila ndoa mbona walidumu?swala si ndoa...bali uaminifu na nia ya dhati.Mungu hutazama nia na kusudi la wawili ndani ya Moyo...ndoa ni formality tu,muhimu maridhiano
 
tuje kwenye mada yako iko hivi wachaga wote huoana isipokuwa mkibosho na mmachame tu, laana hii iliwekwa toka enzi za mambabu wakati wa utawala wa mangi kwamba, enzi za mangi wa Kibosho, aliwah kutok ana kupigana vita na Mangi wa Machame kisa wanagombea maeneo na eneo hilo sikumbuki vyema lilikuwa sijui ni eneo la mto WERUWERU sina hakika sana.
Hili hata mimi niliwahi kulisikia way back,kutoka kwa shangazi yangu!
sasa ikatokea kwamba vijana wa kibosho walikuwa wanawaua vijana wa machame kwa ukatili sana yaani wanawachoma visu na kuwacharanga kama nyama, ndipo ikawekwa amini Mmachame asiolewe KIBOSHO wala asijenge nyumba kuangalia Kibosho.
Hili nalo niliwahi kulisikia na niliwahi kushuhudia ugomvi huu pale kiborloni
Kwa macho yangu nimeshuhudia baadhi ya ndoa za mkibosho na mmachame zikiteseka ama kwa kupata watoto walemavu, ama kuuana, ama ugonjwa nk kwasababu ya mwiko uliowekwa, lkn pia nimeshuhudia hata waliokaidi na kujenga nyumba ikaelekea kibosho wakipata shida sana kwenye hizo nyumba hii ni kweli na haipingiki.
Ila hili,dah!
Limenistua kidogo
Binafsi najua kuhusu laana lakini sujawahi kuishuhudia ikifanya kazi!
Napenda kukiri kusataajabu na kuna kitu nimekumbuka hapa!
 
Kiongozi nilichokiandika nimekipata kutoka kwa mchaga mtu mzima na nimefuatilia kwa wengine wawili watatu wote wanasema hivyo. Kuhusu hiyo ndoa ya wazazi wako, chunguza vizuri utasikia kuna tambiko walifanya kuzuia laana hiyo. Tena kama ni wa miaka 30 iliyopita lazima walifanya tambiko la ukweli haswa maana miaka hiyo imani hiyo ilikuwa na nguvu labda kuliko leo.

hivi hizi laana za wachaga wa machame zinawahusu pia wa marangu, kirua, rombo,old moshi?
 
Ndicho kilichompata Ufoo Saro na mpenzi wake marehemu Mushi. Uliza mchaga aliye karibu nawe atakupa details. Imagine marehemu Mushi hadi anajiua juzi alikuwa tayari na umri wa miaka 40, bado alikuwa anamsubiria Ufoo (licha ya kwamba walishazaa mtoto mmoja), tunaambiwa walikuwa wachumba! Inasemekana ni laana iliachwa na mababu tangu kale.
Poleni wafiwa. Ufoo ugua pole, ni mitihani ya dunia, amini Mwenyezi Mungu atakuvusha salama.

Cc 2013 Nicholas Nyakageni.
Nyie wachaga hebu njooni mregebishe huku ati!
 
Last edited by a moderator:
Ivi gfsonwin haya makitu ya kibosho (Mangi Sina) VS Wamachame ni applicable siku hizi? Mbona niliwahi kuambiwa hayapo tena?
 
Last edited by a moderator:
wachaga wa machame wana laana gani??

Huyo mtoa mada alizoongelea hapo juu za Machame against Uru na wewe ukaenda mbali zaidi kuihusianisha kibosho nzima!!! Swali langu ni je, zinayagusa au zinawagusa watu wa maeneo mengine ya uchagani ambao hayahusiani na hayo maeneo ya kibosho na Uru pale ambapo mtu wa maeneo hayo atakapo inuka kwa moyo mmoja na kuoa Machame, Uru na Kibosho? Na je laana hizo ni subjective kwa baadhi ya watu na wengine ni objective?(nimekosa maana ya maneno rasmi ya hayo ya kingereza kwa kiswahili). Wewe unaamini katika laana?
 
Alivyoelezea gfsonwin.......ndivyo wengi wetu tunavyojua.......hili la mtoa mada......labda ni la juzi juzi........
Hata mie ndivyo navyojuwa/Nilivyowahi kusimuliwa. Tatizo likitokea jambo kama hili kila mmoja huwa mjuvi matokeo yake tunabaki kulishana visivyoliwa humu!
 
Ivi gfsonwin haya makitu ya kibosho (Mangi Sina) VS Wamachame ni applicable siku hizi? Mbona niliwahi kuambiwa hayapo tena?

ndugu yangu mambo ya mangi sina sijui na mangi wa meli sijui niliyakuta na mifano niliiona kwa watu ambao kwangu walikuwa wakubwa sana yaani naweza kusema walikuwa wazazi.
mifano hiyo ndiyo niliyofunziwa binafsi, lakin kkwa wale wa umri wangu wapo waliooana na labda kwa sababu ya udogo wa umri labda ndio maana hatujaanza kuona impact kwenye hili.

lakin pia laana huenda kiazai cha 3-4 mbona sasa kutoka mangi sina sisi ni kizazi cha 5 hivi?? inamaana imesha kwisha ila tu watu wanaish kwa mapokeo ama ndo ile staili kwamba laana huwaga inajiongeza yenyewe.

nimewah kushuhudia mtu akisema wazi siku mwanangu akiolewa na mkibosho hata kama nimekufa basi nitageuka nyoka nije nimuume afe, nilipochunguza nikaona kwa kauli hii ya mzazi iwapo mwanae atakengeuka basi lazima atapatwa na balaa na atakufa tuuu
 
Tafiti zinaonyesha Kuwait wanaume wengi wa machame wanaoa wanawake wa Uru.
 
Huyo mtoa mada alizoongelea hapo juu za Machame against Uru na wewe ukaenda mbali zaidi kuihusianisha kibosho nzima!!! Swali langu ni je, zinayagusa au zinawagusa watu wa maeneo mengine ya uchagani ambao hayahusiani na hayo maeneo ya kibosho na Uru pale ambapo mtu wa maeneo hayo atakapo inuka kwa moyo mmoja na kuoa Machame, Uru na Kibosho? Na je laana hizo ni subjective kwa baadhi ya watu na wengine ni objective?(nimekosa maana ya maneno rasmi ya hayo ya kingereza kwa kiswahili). Wewe unaamini katika laana?

kwanza kabisa naamini laana zipo na hufanya kazi manake ata Mungu mwenyewe alishasema ya kwamba laana ni kizazi cha 3-4.

wamachame laana ya kutooana na wakibosho iliwekw kwasababu wakibosho walimwaga damu ya vijana wa kimachame, na hii iliwekwa na ikafanya kazi kwa kizazi husika. hakuna laana wala mwiko wa kuoa sehem yyte zaid ya kibosho na siha na siha ni kaka na dada na machame hivyo kuoa huko ni kuoa ndugu
 
Uru ndo nini?karne ya 21 bado tunajadili makabila????????????????
 
naomba kuuliza ndugu zangu wana JF,asilimia kubwa ya wachaga ni wakristo sasa naomba kuuliza hivi hayo mambo ya mila za kutambikia mizimu kidini wanayachukuliaje? kwanini TB Joshua au wainjilist wasiwaombee ili kufuta hizo laana znazosababishwa na mashetan? au kwao dini na tambiko ni kitu kimoja. asanteni
 
Hakika, matambiko na Ukristo ni mbali kama shetani na Msalaba.

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
binafsi mimi ni mchaga wa machame,
Wachaga tuko hivi, hakuna ubaguzi dhidi yetu ila tu, kuna miiko ambayo iko na si kwa nia ya kutuondolea umoja wetu. Lugha zetu ni tofauti kwa kila aina ya mchaga muuru, ataongea tofauti na mmachame ama msiha ama mrombo lkn mmarangu, oldmoshi, na Mkirua wote wanaongea kichaga cha aina moja. Kidogo mkibosho na mmachame wanaweza kusikilizana lkn nayo pia sio sana.

tuje kwenye mada yako iko hivi wachaga wote huoana isipokuwa mkibosho na mmachame tu, laana hii iliwekwa toka enzi za mambabu wakati wa utawala wa mangi kwamba, enzi za mangi wa Kibosho, aliwah kutok ana kupigana vita na Mangi wa Machame kisa wanagombea maeneo na eneo hilo sikumbuki vyema lilikuwa sijui ni eneo la mto WERUWERU sina hakika sana.

sasa ikatokea kwamba vijana wa kibosho walikuwa wanawaua vijana wa machame kwa ukatili sana yaani wanawachoma visu na kuwacharanga kama nyama, ndipo ikawekwa amini Mmachame asiolewe KIBOSHO wala asijenge nyumba kuangalia Kibosho.

Kwa macho yangu nimeshuhudia baadhi ya ndoa za mkibosho na mmachame zikiteseka ama kwa kupata watoto walemavu, ama kuuana, ama ugonjwa nk kwasababu ya mwiko uliowekwa, lkn pia nimeshuhudia hata waliokaidi na kujenga nyumba ikaelekea kibosho wakipata shida sana kwenye hizo nyumba hii ni kweli na haipingiki.

Ukivuka kibosho kwenda maeneo mengine yote iwe old mosh uru, vUNJO, Kilema, marangu, mwika, rombo hawa wanaoana pasi tatizo lolote unless kama familia kama famili ama ukoo kama ukoo una miiko yake.

Nasema ukoo kama ukoo kwasababu, Mushi ni ukoo mkubwa sana na kuna baadhi ya kaka zao wallizaa na dada zao lkn baada ya dada kuzaa walipatiwa maeneo mengine wakaish huko lkn koo zikabadilishwa kwasababu ilihesabika kwamba ni laana kukaa na mtoto wa dada nyumba moja. Mwiko uliowekwa kwenye watu kama hawa ni wasioane manake ni ndugu moja hivyo wakioana watapata laana. mfano hai tunaoweza kuuona ni kama vile Mushi hawaoi kwa Shoo, ama Massawe hawaoi kwa Shuma, ama kama vile mmachame hawezi kumuoa Msiha manake hawa ni dada na kaka kabisa walizaa na ukioa hapa umeoa dada yako mpaka ifanywe mila ya kuvunja undugu ndipo mnaweza labda kupata baraka za watoto.

Kuhusu case ya kwamba Mmchame na muuru hawaoani mimi binafsi naipinga kwani baba yangu mdogo kabisa ni mmachame wa hapa hapa Uduru ni loya mzuri na mkewe ni Muuru ni profesa wa watoto Prof Petronila Ngiloi, wanamaisha mazuri sana na watoto wanao tena waliosoma na maisha yao ni supa hivyo kwa maelezo haya wewe mtoa mada umepotoshwa na waliokuambia.

Kwa uchambuzi huo sihitaji uthibitisho zaidi japo mimi sijui lolote kuhusu kanda hiyo!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom