peri
JF-Expert Member
- Mar 22, 2011
- 2,579
- 1,170
Acha ubinafsi, bataka ya mwenyezi Mungu ndio nini?
mkuu unajua kusoma kweli?
Wapi nimeandika bataka?
Na huo ubinafsi ni upi?
Kuwaambia vijana wenzangu kua waachane na uzinzi ndio ubinafsi?
Acha ubinafsi, bataka ya mwenyezi Mungu ndio nini?
baba mmchame mama mhuru,,mkuu utakuwa mkatili sana..
binafsi mimi ni mchaga wa machame,
Wachaga tuko hivi, hakuna ubaguzi dhidi yetu ila tu, kuna miiko ambayo iko na si kwa nia ya kutuondolea umoja wetu. Lugha zetu ni tofauti kwa kila aina ya mchaga muuru, ataongea tofauti na mmachame ama msiha ama mrombo lkn mmarangu, oldmoshi, na Mkirua wote wanaongea kichaga cha aina moja. Kidogo mkibosho na mmachame wanaweza kusikilizana lkn nayo pia sio sana.
tuje kwenye mada yako iko hivi wachaga wote huoana isipokuwa mkibosho na mmachame tu, laana hii iliwekwa toka enzi za mambabu wakati wa utawala wa mangi kwamba, enzi za mangi wa Kibosho, aliwah kutok ana kupigana vita na Mangi wa Machame kisa wanagombea maeneo na eneo hilo sikumbuki vyema lilikuwa sijui ni eneo la mto WERUWERU sina hakika sana.
sasa ikatokea kwamba vijana wa kibosho walikuwa wanawaua vijana wa machame kwa ukatili sana yaani wanawachoma visu na kuwacharanga kama nyama, ndipo ikawekwa amini Mmachame asiolewe KIBOSHO wala asijenge nyumba kuangalia Kibosho.
Kwa macho yangu nimeshuhudia baadhi ya ndoa za mkibosho na mmachame zikiteseka ama kwa kupata watoto walemavu, ama kuuana, ama ugonjwa nk kwasababu ya mwiko uliowekwa, lkn pia nimeshuhudia hata waliokaidi na kujenga nyumba ikaelekea kibosho wakipata shida sana kwenye hizo nyumba hii ni kweli na haipingiki.
Ukivuka kibosho kwenda maeneo mengine yote iwe old mosh uru, vUNJO, Kilema, marangu, mwika, rombo hawa wanaoana pasi tatizo lolote unless kama familia kama famili ama ukoo kama ukoo una miiko yake.
Nasema ukoo kama ukoo kwasababu, Mushi ni ukoo mkubwa sana na kuna baadhi ya kaka zao wallizaa na dada zao lkn baada ya dada kuzaa walipatiwa maeneo mengine wakaish huko lkn koo zikabadilishwa kwasababu ilihesabika kwamba ni laana kukaa na mtoto wa dada nyumba moja. Mwiko uliowekwa kwenye watu kama hawa ni wasioane manake ni ndugu moja hivyo wakioana watapata laana. mfano hai tunaoweza kuuona ni kama vile Mushi hawaoi kwa Shoo, ama Massawe hawaoi kwa Shuma, ama kama vile mmachame hawezi kumuoa Msiha manake hawa ni dada na kaka kabisa walizaa na ukioa hapa umeoa dada yako mpaka ifanywe mila ya kuvunja undugu ndipo mnaweza labda kupata baraka za watoto.
Kuhusu case ya kwamba Mmchame na muuru hawaoani mimi binafsi naipinga kwani baba yangu mdogo kabisa ni mmachame wa hapa hapa Uduru ni loya mzuri na mkewe ni Muuru ni profesa wa watoto Prof Petronila Ngiloi, wanamaisha mazuri sana na watoto wanao tena waliosoma na maisha yao ni supa hivyo kwa maelezo haya wewe mtoa mada umepotoshwa na waliokuambia.
mimi ni MeSijui namna ya kukusaidia! maana hata jinsia yako siipati kama ni mwanamke sihitaji ku argue na wewe kwani hujui mimi vigezo vyangu kwa ke ni vipi?
Kama ni me hujitambui unachoona kizuri kwangu cha weza kuwa kibaya, ndio maana nikikutana na msichana awe na face ya ajabu au nzuri lazima nigeuze kichwa kusaminisha nyuma! kwangu mwanamke lazima awe na kijiusafiri japo ukizidi sipendi na napenda mdada mwenye umbo dogo la mimi kuhendo, tofouti na mwingine wala siwezi zungumzia nafsi yake sasa unajitia ujinga hapa sehemu hii wanapenda hivi mbona mimi na ndugu zangu wa damu hatupendi wanawake wa aina moja?
Usifikiri wachaga wengi wa zamani hatuwafahamu na face zenu nzuri na rangi nyeupe (ambayo mimi si mpenzi) kifuani hilo, huku nyuma mmepigwa pasi! siku hizi kidogo mmegundua kumbe usafiri wa binti mama ana uwezo wa kumtengenezea mtoto akiwa mdogo ndio kizazi cha akina lulu,wolper n.k tunaona wana usafiri na maumbo mazuri!
Usinilazimishe kupenda unachopenda ishia hapo hapo!!!!!!!!
sijajua ni kabila gani unalotaka kulielezea kuwa lina miguu mizuri.:smile-big:
mimi ni me, kwa inshort maumbile ya watu hayahusiani na kabila zaidi ni mfumo wa kuishi. wamama wa uchagani ni wachapa kazi, hilo tu linaweza kubadilisha mjengeko wa maumbile yao bila kugusia barabara zenye mlima kilimanjaro, na tope, kama ambavyo wa mama wa kizungu walivyo na mikono mikubwa na vifua vipana.
binafsi hilo la kutembelea mikono sijaliona kwenye ukoo wetu, na ajabu ni kwamba hata me na ke kwa ujumla waliozaliwa wako waliojifunza marshal arts na wacheza mpira wazuri tu lakini hawatembelei mikono.
tukirudi kuhusu nachopendelea ni kuwa;.
binafsi navutiwa na wanawake wenye curve zaidi na sio makalio mkubwa. japo natofautiana na wewe, kuwa mimi si mpenzi wa vipotabo navutiwa zaidi na high breed kwani hata uzao wake nauhakika sio cachexia
matumbo hacha kusakama ndugu zetu Wachagga! Acha porojo zako zisizokuwa na msingi!haikambe manka!!nyinyi wachaga mnashilikiana kwenye ujambazi tu zaidi ya hapo chui na paka.
another haters.Mimi nimeishi uchagani miaka 10 sasa. It is terrible. Ngoja nisali kwanza then narudi
Anti-chagga wamejaza hii thread.
ingekuwa pouwa mkitoa comment huku mki-ahinisha makabila yenu pia.Teh teh teh! I was trying to call you so you can defend you chaga tribe!
Thats all!
mkuu usipotoshe, mimi ni mchaga, baba wa machame mama wa uru.
Wameoana takriban miaka 30 ilopita na bado wako pamoja.
Tatizo ndo za vijana wa leo haziendi bila uzinzi, mzini kwanza ndio muoane.
Hiyo baraka ya Mwenyezi Mungu itatoka wapi?
Unakuta watu ni wachumba lkn wana mtoto/watoto tayari. Hayo ni mafundisho ya wapi kama sio laana?
kwanza kabisa naamini laana zipo na hufanya kazi manake ata Mungu mwenyewe alishasema ya kwamba laana ni kizazi cha 3-4.
wamachame laana ya kutooana na wakibosho iliwekw kwasababu wakibosho walimwaga damu ya vijana wa kimachame, na hii iliwekwa na ikafanya kazi kwa kizazi husika. hakuna laana wala mwiko wa kuoa sehem yyte zaid ya kibosho na siha na siha ni kaka na dada na machame hivyo kuoa huko ni kuoa ndugu
naomba kuuliza ndugu zangu wana JF,asilimia kubwa ya wachaga ni wakristo sasa naomba kuuliza hivi hayo mambo ya mila za kutambikia mizimu kidini wanayachukuliaje? kwanini TB Joshua au wainjilist wasiwaombee ili kufuta hizo laana znazosababishwa na mashetan? au kwao dini na tambiko ni kitu kimoja. asanteni
Uongo mkubwa huu! Bora hata ungesema Mkibosho na Mmachame ingawa nayo ilikuwa zamani siku hizi tunaka kula na kunywa pamoja mwisho tukipendana unajua kinachfuata.Kiongozi nilichokiandika nimekipata kutoka kwa mchaga mtu mzima na nimefuatilia kwa wengine wawili watatu wote wanasema hivyo. Kuhusu hiyo ndoa ya wazazi wako, chunguza vizuri utasikia kuna tambiko walifanya kuzuia laana hiyo. Tena kama ni wa miaka 30 iliyopita lazima walifanya tambiko la ukweli haswa maana miaka hiyo imani hiyo ilikuwa na nguvu labda kuliko leo.