Linapokuja swala la fedha, sadaka, na kujitengenezea empire ya biashara tusichukulie jambo lolote kwa urahisi. Tumeyaona hapa US ya kina Jimmy Swaggart, na kina Poppoff; Tumeyaona ya kina Deya kama nilivyotolea mfano. Itakuwa ni makosa makubwa kwa akili zetu tukisema ati kwa vile mtu anasema "anatenda miujiza" basi tukubali tu na tusihoji.
Tutakuwa tunafanya makosa makubwa kabisa tukikubali madai ya kidini kwa vile ni ya kidini bila kuangalia athari zake.
a. Kama kuna kikundi cha watu (bila Rev. Lwakatare kujua) wameamua kuigiza, kujificha vichakani na wengine kwenda kudai kuwa wameona misukule wakiwa na lengo la kujipatia maisha ya bure nani atajua?
b. Kama mama Lwakatare mwenyewe katika haja ya kuongeza waumini, sadaka na ujiko kwa shughuli zake za biashara ameamua kufanya hoax hii akijua kwamba Watanzania wataamini bila kuhoji, na kwa kweli watu wanaanza kuamini kutoa sadaka zaidi na kupeleka watoto wao kwenye shule za mama huyo kwa sababu hiyo, je haionekani hii ni kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu?
c. Kama watu hawa kweli walikuwa ni misukule na sasa wanaishi; sayansi itafaidika katika kufahamu kilichozikwa ni nini basi na kwa vile aliyechukua misukule amejitangaza wazi basi atakuwa msaada wa kuonesha jinsi/madawa aliyotumia kufanya hivyo. Yawezekana yakawa na application nyingine kubwa sana kama vile kwenye mambo ya upasuaji n.k Je tusichunguze mambo haya ili kujiridhisha?
d. Kama watu hawa siyo waliokufa (yaani miili bado iko kaburini) hawa misule ni kina nani? Yawezekana ni watu waliokuwa wanahsikiliwa kinyume cha sheria na kutumikishwa kama watumwa?