Mch. Mhe. Dr. Getrude Lwakatare achunguzwe!

Mch. Mhe. Dr. Getrude Lwakatare achunguzwe!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
34,250
Reaction score
44,579
Uchunguzi uliofanywa na waandishi wetu katika kanisa hilo, unaonyesha kuwa kati ya watu hao Misukule nane waliopatikana katika misitu hiyo baada ya waliowachukua kimazingira kumrudia Mungu, watano wameshachukuliwa na ndugu zao ambapo watatu bado wanaendelea kutunzwa na kusali katika kanisa hilo, hali iliyowafanya baadhi ya waunimi kusema kuwa ndugu zao watakuwa wamewasusa.

Baadhi ya waumini waliozungumza na waandishi wetu kwa sharti la kutoandikwa majina yao gazetini kwa kuwa si wasemaji wa kanisa, walidai kuwa wanaamini kwamba vijana hao watatu ambao ndugu zao hawajajitokeza licha ya habari zao kutangazwa katika vyombo mbalimbali vya habari, inawafanya waamini kuwa jamaa zao bado wana imani kuwa wamekwisha fariki dunia.

Hata hivyo, uchunguzi unaonesha kuwa baadhi ya waumini walikuwa na mawazo tofauti kwa kusema kwamba uwenda ndugu zao hawajapata taarifa kuhusiana na vijana wao kwa kuwa wengi walipoteza kumbukumbu na endapo wangepatiwa taarifa wangeweza kujitokeza.

Akizungumza na mwandishi wetu kwa njia ya simu jana, Mchungaji Lwakatare alikiri kuendelea kuwa na misukule hao katika kanisa lake.

Hata kama ndugu zao watawasusa nitaendelea kuwalea na baadaye wakiwa na akili safi nitawapa ajira, alisema mchungaji huyo.

Akifafanua zaidi, Mchungaji Lwakatare alisema kuwa watu hao wengi wao awali walikuwa wamepoteza kumbukumbu kabisa lakini sasa wana afadhali kwa kuwa wanaanza kuelewa mambo.

Hivi karibuni gazeti hili na vyombo vingine vya habari viliripoti kukamatwa kwa misukule katika Kanisa la Mikocheni B Assemblies of God na kusababisha wasomaji wetu wengi kutaka kujua kinachoendelea, hivyo kuanzisha uchunguzi kujua kama bado wapo au la.

My Take:
Kanisa la huyu mama naamini linaeneza one of the most elaborated scheme of deception a.k.a a hoax! Inanikumbusha kisa cha Mchungaji Gilbert Deya wa Uingereza (raia wa Kenya) ambaye alikuwa amedai yeye na mke wake kuwa wanauwezo wa kuombea wa kina mama na wakapata mimba na kuzaa watoto hata kama kina mama hao walishapita uwezo wao wa kuzaa n.k

Ingawa mwanzoni mambo hayo yaliweza kuonekana ni miujiza, utaalamu wa kisayansi ulionesha kuwa mke wa mchungaji huyo na washirika wao kule Kenya walikuwa wananunua watoto wadogo na kuwapa kina mama wengine na kwa kufanya hivyo kufanya biashara ya watoto lakini wakati huo huo kulifanya kanisa la Mchungaji huyo kukua zaidi na kuwa na ujiko usio kifani kutokana na kazi ya "Mchungaji huyo".

Mwishoni, sheria ikakutana naye, mke wake akaswekwa jela na yeye mwenyewe mchungaji kutakiwa kurudishwa Kenya kukabiliana na mashtaka ya usafirishaji haramu wa watoto.

Naamini, kama kuna mtu ana ujasiri wa kuchunguza hii "misukule" na kanisa hilo kutaonekana pasipo shaka jinsi gani this hoax was propagated and carried out na hivyo kumpa mama Lwakatare ujiko na kumuongezea sadaka.

Natoa hoja, kanisa lake na yeye mwenyewe achunguzwe pamoja na hao "misukule" kwani anachezea imani za watu na hasa hofu yao ya mambo ya kishirikina.

Kwa vile tuna utaalamu wa DNA, basi misukule hao na "familia" zao na hata makaburi wanayodaiwa kuzikwa yachunguzwe ili wananchi wetu wasitekwe na ulaghai wa kidini unaoendeshwa kwa jina la dini.

Endapo uchunguzi wa kisayansi utaonesha kuwa kweli hawa watu walikufa, wakazikwa na baadaye kukutwa porini wakiwa wamechukuliwa misukule nitamwomba radhi; Lakini nasimamia kusema this is a HOAX inayofanywa na Mbunge Mchungaji!
 
Mwanakijiji,

Mimi naamini kwa YESU YOTE yanawezekana!

Isimuhukumu huyu mama. Ina maana waumini wote hapo kanisani hawayaoni hayo yote?

FP
 
Kazi kweli kweli ukistaajabu ya wasabato masalia utayaona ya mama Lwakatare...
 
Complicated? Sidhani. Hapa ni ujuha wa waumini; na utapeli wa mchungaji. Hakuna la ziada.

Beyond explanations. Isijekuwa wamewaokota watu wenye maradhi ya akili kusikojulikana, wakawapeleka msituni. Hii bwana ni biashara na biashara lazima utangaze vinginevyo huta uza kitu. Strategic Church Management ya Mch, Mh,Dr. Lwakatare
 
Mwanakijiji,

Mimi naamini kwa YESU YOTE yanawezekana!

Isimuhukumu huyu mama. Ina maana waumini wote hapo kanisani hawayaoni hayo yote?

FP

Kuna wakati fulani Yesu alimponya mtu mmoja mwenye ukoma; akamwambia "nenda kwa makuhani ukajioneshe". Lengo lilikuwa ni kuthibitisha kuwa ameponga kweli na haikuwa hoax.

Wakati mwingine alimponya mtu mmoja aliyezaliwa kipofu. Wakuu wa Makuhani waliposikia habari hiyo hawakuamini na wakawaita wazazi wa huyo jamaa na kuuliza habari zake. Wale wazazi wakasema "yeye ni mtu mzima muulizeni mwenyewe". Yule bwana alipoitwa akawaambia kuwa "mimi sijui kama huyo aliyeniponya ni mtakatifu au la, ninachojua ni kuwa nilikuwa kipofu na sasa naona".

Katika mifano hiyo miwili utaona kuwa kwenye mambo ya miujiza kufanya uchunguzi siyo kukana miujiza bali kuondoa uwezekano wa uongo. Ninaamini miujiza lakini miujiza yote inafanywa kwa kutumia vitu vya asili. So, kuhoji suala la misukule si kukana uwezo wa Mungu kutenda miujiza bali kuthibitisha nguvu hizo na kuzikiri lakini wakati huo huo kuondoa uwezekano wa roho ya mwanadamu kujikweza na kujiinua na kujisamamisha mahali pa Mungu!
 
Mwanakijiji,

Mimi naamini kwa YESU YOTE yanawezekana!

Isimuhukumu huyu mama. Ina maana waumini wote hapo kanisani hawayaoni hayo yote?

FP

Kumbuka ndugu yangu watu siku hizi wanatumia kila njia kufanikisha wanachotaka. siku zote sijawahi kumkubali huyu mama hasa baada ya kuanza kutoa vioja na jamii nzima kumtegea sikio zaidi na kuuliza "yule mama mwenye shule za st. mary's" "aaah yule mama mwenye radio eenh" wengine wakisema "aliyewatoa misukule ni yule mama mbunge" na title zake nyingine nyngi. wakati watu wanaongelea misukule anayoijua yeye (am not conviced) kumbe mnamtangaza na kutangaza biashara zake bila watu kujijua!

umaarufu gharama ati, maana hata imani ya dini yake yenyewe inasema wazi kuwa sku za mwisho watakuwa manabii wengi wa uongo (sijasema yeye mmoja wapo) hivyo wananchi hasa wenye kutaka kuondolewa matatizo yetu kwa urahisi na haraka tuwe makini!
 
..... Dini Biashara, ndio maana inafanya matangazo na mamilioni ya pesa kulipia vipindi vya TV, na kutoa mabango mitaani, kwa namna hiyo unategemea asile mingo? tena katika hali ya sasa ya wachungaji kibao wanaoponya DHAMBI (ya ngono, ulevi na nyinginezo)

mimi wala sishangai kwa huyu mama. hivi ile kashfa ya kuwa anajihusisha na madawa ya kulevya ilithibitishwa au? kwa anayejua nitafurah akinifahamisha
 
Waandishi wetu wa habari wa Tanzania wako wapi? Hakuna journalist investigation jamani? Sio lazima kila kitu polisi waachiwe, kwanza hawawezi hao. Waandishi makini (achana na hawa wa Shigongo) wanaweza kutusaidia kumuumbua huyu mama. Huu ni utapeli period!
 
With all due respect, mapema sana nilishasema kuwa huyu mama mimi ninamshitukia sana kwa sababu ninajua according to the dataz, kuwa anajirusha na Mkulu mmoja wa CCM,

Kwa hiyo haya mengine yote ni tisa, kumi Mungu hawezi chezewa na bina-adam hata siku moja, ndio maana yanaanza kujitokeza, ni aibu sana kwa wale tunaomuamini Mungu.
 
Waandishi wetu wa habari wa Tanzania wako wapi? Hakuna journalist investigation jamani? Sio lazima kila kitu polisi waachiwe, kwanza hawawezi hao. Waandishi makini (achana na hawa wa Shigongo) wanaweza kutusaidia kumuumbua huyu mama. Huu ni utapeli period![/QUOTE

Mkuu Nurujamii,Mimi kama wewe siamini kabisa hayo yanayotokea kwa Mama Mchungaji Lwakatare.Lakini niamini.... ni kweli watu wengi wanamuona Mama ni kama Muokozi/mkombozi wao kwa kuwarudisha hao ndugu zao (Misukule).Tusichukue nafasi hii kumlaumu sana Mama,nafikiri ni kazi ya serikali kwa kupitia vyombo vyake mbalimbali kupata Ukweli na uhakika wa Jambo hili,vinginevyo tutakuwa tunajenga jamii inayoamini Imani za Uchawi.

Hivi karibuni kumezuka mambo mengi yanayohusishwa na ushirikiana,lakini inaonekana serikali inayafumbia macho..Kumbuka mauaji ya Albinos,Unga unga wa Mheshimiwa Chenge Bungeni,Yule kijana aliyekutwa na Kichwa cha Mtoto kwenye mfuko wa Rambo....Najua kuna mengi yanayoendelea huko mitaani lakini hatuyajui.

Ili kujenga Taifa lenye maendeleo ya kweli ni vyema kukomesha mambo haya ya imani za kichawi...Haingii akilini kwenye karne hii ya mwendokasi wa maendeleo ya Teknolojia sie bado tupo kwenye stone age.Serikali ni vyema ichukue hatua madhubuti kuchunguza na kutoa Tamko kuhusu suala hili zito..
 
..........kanisa katoliki kinaamini kuwa miujiza yote ni lazima ichunguzwe kabla ya kutangazwa kikanisa......!!!..kwa utaratibu huo kwenye kanisa katoliki mtumishi au muumini yeyote akifanya miujiza hatakiwi kuanza kujitangaza hadi ...uchunguzi na maombi ufanyike kubaini kama uponyaji au miujiza umetokaana na jina la bwana yesu au tofauti!!!..na ikiweza kudhibitika kuwa mtu ana nguvu hizo basi huwekwa kwenye kundi la watakatifu....

makanisa mengi yanaibuka siku hizi ie mtume na nabii mwingira,askofu mkuu kakobe na wengine.......wanafanya kazi nzuri ..lakini kinachonitia hofu ni kuwa wengi kati ya hawa..hawapendi MASWALI KWENYE MIUJIZA WANAYOTENDA ...WALA HAWATAKI UCHUNGUZI....!!!

LAKINI BADO NAAMINI umuhimui wa nadharia ya kanisa katoliki na makanisa mengine ya asili kama orthodox ,lutheran etc .....kwenye "kusikiliza kwa makini sauti"...kwani hata shetani anaweza kuiga sauti ya Mungu!!
 
Uchunguzi uliofanywa na waandishi wetu katika kanisa hilo, unaonyesha kuwa kati ya watu hao Misukule nane waliopatikana katika misitu hiyo baada ya waliowachukua kimazingira kumrudia Mungu, watano wameshachukuliwa na ndugu zao ambapo watatu bado wanaendelea kutunzwa na kusali katika kanisa hilo, hali iliyowafanya baadhi ya waunimi kusema kuwa ndugu zao watakuwa wamewasusa.

Baadhi ya waumini waliozungumza na waandishi wetu kwa sharti la kutoandikwa majina yao gazetini kwa kuwa si wasemaji wa kanisa, walidai kuwa wanaamini kwamba vijana hao watatu ambao ndugu zao hawajajitokeza licha ya habari zao kutangazwa katika vyombo mbalimbali vya habari, inawafanya waamini kuwa jamaa zao bado wana imani kuwa wamekwisha fariki dunia.
1217917692_mfuhai2eweb.gif

Hata hivyo, uchunguzi unaonesha kuwa baadhi ya waumini walikuwa na mawazo tofauti kwa kusema kwamba uwenda ndugu zao hawajapata taarifa kuhusiana na vijana wao kwa kuwa wengi walipoteza kumbukumbu na endapo wangepatiwa taarifa wangeweza kujitokeza.

Akizungumza na mwandishi wetu kwa njia ya simu jana, Mchungaji Lwakatare alikiri kuendelea kuwa na misukule hao katika kanisa lake.

“Hata kama ndugu zao watawasusa nitaendelea kuwalea na baadaye wakiwa na akili safi nitawapa ajira,” alisema mchungaji huyo.
1217917692_msukuleweb.gif

Akifafanua zaidi, Mchungaji Lwakatare alisema kuwa watu hao wengi wao awali walikuwa wamepoteza kumbukumbu kabisa lakini sasa wana afadhali kwa kuwa wanaanza kuelewa mambo.

Hivi karibuni gazeti hili na vyombo vingine vya habari viliripoti kukamatwa kwa misukule katika Kanisa la Mikocheni B Assemblies of God na kusababisha wasomaji wetu wengi kutaka kujua kinachoendelea, hivyo kuanzisha uchunguzi kujua kama bado wapo au la.
1219302231_jenifaweb00.jpg

My Take:
Kanisa la huyu mama naamini linaeneza one of the most elaborated scheme of deception a.k.a a hoax! Inanikumbusha kisa cha Mchungaji Gilbert Deya wa Uingereza (raia wa Kenya) ambaye alikuwa amedai yeye na mke wake kuwa wanauwezo wa kuombea wa kina mama na wakapata mimba na kuzaa watoto hata kama kina mama hao walishapita uwezo wao wa kuzaa n.k

Ingawa mwanzoni mambo hayo yaliweza kuonekana ni miujiza, utaalamu wa kisayansi ulionesha kuwa mke wa mchungaji huyo na washirika wao kule Kenya walikuwa wananunua watoto wadogo na kuwapa kina mama wengine na kwa kufanya hivyo kufanya biashara ya watoto lakini wakati huo huo kulifanya kanisa la Mchungaji huyo kukua zaidi na kuwa na ujiko usio kifani kutokana na kazi ya "Mchungaji huyo".

Mwishoni, sheria ikakutana naye, mke wake akaswekwa jela na yeye mwenyewe mchungaji kutakiwa kurudishwa Kenya kukabiliana na mashtaka ya usafirishaji haramu wa watoto.

Naamini, kama kuna mtu ana ujasiri wa kuchunguza hii "misukule" na kanisa hilo kutaonekana pasipo shaka jinsi gani this hoax was propagated and carried out na hivyo kumpa mama Lwakatare ujiko na kumuongezea sadaka.

Natoa hoja, kanisa lake na yeye mwenyewe achunguzwe pamoja na hao "misukule" kwani anachezea imani za watu na hasa hofu yao ya mambo ya kishirikina.

Kwa vile tuna utaalamu wa DNA, basi misukule hao na "familia" zao na hata makaburi wanayodaiwa kuzikwa yachunguzwe ili wananchi wetu wasitekwe na ulaghai wa kidini unaoendeshwa kwa jina la dini.

Endapo uchunguzi wa kisayansi utaonesha kuwa kweli hawa watu walikufa, wakazikwa na baadaye kukutwa porini wakiwa wamechukuliwa misukule nitamwomba radhi; Lakini nasimamia kusema this is a HOAX inayofanywa na Mbunge Mchungaji!

Clear as glass. I dont have none to add this is wht I was thinking since yule kijana Ramadhani aliyekamatwa na kichwa cha mtoto alipodondoka pale Kanisani. Mwanzo alisema ametokea mikoa ya kusini walikuwa wakisafiri kwa ungo yeye na bibi yake baada ya muda si akakamatwa na kichwa cha mtoto na kudai kuwa anakaa maeneo ya segerea na yeye na mama yake huwa wanakunywa damu za watu na huwa wanafanya ajali zitokee.

Missing point:

Kama huwa wanafanya ajali zitokee ndipo wanywe damu kanini walimchinja yule binti wa miaka mitatu? na makazi ya huyu kijana mbona yana utata kuanzia story ya mwanzo na story ya pili? Ninazidi kuchanganyikiwa zaidi na hili la misukule.
 
Jamani mweee!...
Uchawi upo na umeonekana toka enzi na enzi hivyo imani ya dini moja kati ya therapy ambazo zimewapa ponya watu wengi kiakili..
Binafsi huyu Mama hata kama ni zuga anachokifanya kinastahiri sifa kwa sababu hakuna kati yenu anayeweza kuwachukua watu hao na kuwapa hifadhi..
Kama binadamu hawa jamaa wanahitaji hifadhi na hakuna ushahidi wa kwamba wanakuwa abused isipokuwa kutendewa mema mbali na kuongozwa ktk imani ya dini...It's somekind of therapy kwao...
Iwe miujiza ya Mungu ama sababu ya kupata nafuu ni malezi mazuri ktk mazingira huru yote haya yanalenga kuwarudisha watu hawa katika uzima wa afya zaidi ya roho..
Kinachowaudhi wengi humu ni kufikiria tu kwamba lengo la Mama Lwakatare ni kueneza imani ya dini yake wakati sote humu tunaelewa wazi kwamba hawa jamaa ni vichaa kama sio wendawazimu... Sasa sijui hiyo dini ataweza vipi kuwafundisha wendawazimu wakaifuata...
My two cents kama wewe unaumwa sana kuona jinsi mama huyu anavyotumia nafsi yake basi volunteer kumchukua hata mmoja kati ya hao vijana..
 
Back
Top Bottom