Mbunge Zaytun Swai Agawa Majiko ya Gesi na Vyerehani Ili Kuwainua Wanawake Kiuchumi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945

MBUNGE ZAYTUN SWAI AGAWA MAJIKO NA VYEREHANI ILI KUWAWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha, Mh. Zaytun Swai kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) amegawa majiko ya gesi 10 na vyerahani 5 kwaajili ya kuwawezesha kiuchumi wanawake wa vijijini katika Kata ya Kimyaki Halmashauri ya Arusha wilayani Arumeru.

Akizungumka wakati wa hafla ya kukabidhi majiko hayo, Mhe. Zaytun Swai amesema ameamua kugawa majiko na cherahani hivyo ili kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita katika adhma ya kumkomboa na kumsaidia mwanamke kiuchumi hususani mwanamke anayeishi kijijini kwa kuhakikisha anapata mahitaji muhimu ikiwemo huduma za afya, elimu, nishati bora, maji pamoja na mitaji ya kibiashara.

"Mimi kama mwakilishi wa wanawake Bungeni kutoka Mkoa wa Arusha jukumu langu kubwa ni kuhakikisha nawasemea wanawake ili muweze kunufaika na fursa za kiuwekezaji zilizopo ikiwa ni pamoja na kujiunga katika vikundi vya ujasilimali vilevile kupata mikopo ya riba nafuu itakayowasaidia kuwainua kiuchumi na kuzisaidia familia zenu kwani wanawake ndiyo nguzo kuu ya familia" - Mhe. Zaytun Swai, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha.

Sambamba na hilo Mhe. Zaytun Swai pia amechangia matofali 500 kwaajili ya ujenzi wa bweni la Shule ya Sekondari Kimyaki ambayo inaupungufu wa mabweni kwa wanafunzi wa kike, kitu ambacho kinapelekea wengine kukatisha masomo kutokana na umbali wa kuja shuleni pamoja na vishawishi mbalimbali.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi maalum Dkt. Doroth Gwajima katika kuhitimisha sherehe za maadhimisho ya mwanamke anayeishi kijijini, amempongeza mbunge Zaituin Swai kwa moyo wa kizalendo wa kuwajali wanawake hususani waishio katika mazingira magumu.

Vilevile Mwenyekiti wa Halmashauri ya Arusha, Dkt. Ujung’u Salekwa amempongeza na kumshukuru Mh.Swai kwa mchango wake huo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika kuhakikisha kwamba, akina mama na watoto wa kike wanaweza kujisimamia.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-10-22 at 14.22.01.jpeg
    WhatsApp Image 2023-10-22 at 14.22.01.jpeg
    88 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-10-22 at 14.22.03.jpeg
    WhatsApp Image 2023-10-22 at 14.22.03.jpeg
    74 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-10-22 at 14.22.03(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-10-22 at 14.22.03(1).jpeg
    60.2 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-10-22 at 14.22.04(3).jpeg
    WhatsApp Image 2023-10-22 at 14.22.04(3).jpeg
    85.3 KB · Views: 3
Back
Top Bottom