Mbunge Zaytun Swai: Waziri Atueleze Sekta ya Utalii Itafikishaje Watalii Milioni 5 Hadi Kufikia 2025 Sawa na Ilani ya CCM

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,902
944

MHE. ZAYTUN SWAI: WAZIRI AJE ATUELEZE SEKTA YA UTALII ITAFIKISHAJE WATALII MILIONI 5 HADI KUFIKIA 2025 SAWA ILANI YA CCM

"Naipongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maono yake chanya ya kuweza kurudisha Tume ya Mipango na kuunda Wizara ya Mipango na Uwekezaji kwaajili ya kushughulikia Mipango mahususi ya Taifa letu" - Mhe. Zaytun Swai, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha

"Kuwepo kwa Tume ya Mipango na Wizara ya Mipango na Uwekezaji ni dhahiri kutatua changamoto zilizokuwepo awali ambapo tuliona kila Wizara ya kisekta ina panga Mipango yake kwani lilisababisha gharama kubwa ya utekelezaji wa miradi na ufanisi hafifu wa utekelezaji wa miradi" - Mhe. Zaytun Swai, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha

"Kwa miradi inayofanana, Wizara za kisekta ziweze kushirikiana na Wizara ya Fedha ili kutoa fedha kwenye fungu moja ili kutekeleza mradi mmoja wenye tija kwa Taifa letu" - Mhe. Zaytun Swai, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha

"Tunategemea kuona kwenye mpango mikakati ya Serikali katika kutekeleza malengo kama ilivyo kwenye Ilani ya CCM 2020-2025. Sekta ya Utalii mpaka 2025 tunategemea idadi ya Watalii ifikie million 5" - Mhe. Zaytun Swai, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha

"Mpango unaokuja wa Maendeleo ya Taifa, Waziri wa Maliasili na Utalii aje atuainishie ili tujue tutawezaje kufikia watalii Milioni 5 mpaka kufikia mwaka 2025 kutoka idadi ya sasa tuliyonayo ya watalii Milioni 1.4 wanaotembelea nchini" - Mhe. Zaytun Swai, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha

"Sekta ya Utalii ina changamoto ya Miundombinu, idadi ndogo ya vyumba vya kulaza wageni, maduka ya kubadilisha fedha, Ada na tozo ambazo ni kubwa kwa watalii wetu. Waziri atuambie mpango unaokuja utawezaje kutatua changamoto ili tuweze kufikia malengo yaliyopo kwenye Ilani ya Chama Cha Mapinduzi" - Mhe. Zaytun Swai, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha

"Kwa kuzingatia malengo ya mpango wa Taifa wa kujenga Uchumi shindani na viwanda ni lazima kama Taifa tuweze kuongeza tija kwenye sekta za uzalishaji kama Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Madini na Misitu" - Mhe. Zaytun Swai, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha

"Kupanga ni kuchagua, lakini siyo kuchagua tu ila kuchagua mambo yaliyo bora zaidi na yenye tija. Waziri asituletee orodha ya miradi isiyotekelezeka lakini atuletee miradi michache yenye tija inayotekelezeka" - Mhe. Zaytun Swai, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-11-07 at 10.29.01.jpeg
    WhatsApp Image 2023-11-07 at 10.29.01.jpeg
    41.6 KB · Views: 2
Back
Top Bottom