Mbunge Zaytun Swai: Rais Samia ni Mhifadhi na mtunza Mazingira namba moja nchini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
942
"Tumekuja katika Gereza la Wilaya ya Karatu katika siku ya kumbukizi ya kuzaliwa ya Rais wetu Mpendwa Mama Samia Suluhu Hassan. Nimekuja na akina mama wa Wilaya ya Karatu kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Karatu" - Mhe. Zaytun Seif Swai, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha

"Tunamtakia Rais Samia Suluhu Hassan heri katika siku yake ya kuzaliwa. Tunamuomba mwenyezi Mungu aendelee kumjalia Busara nyingi, aendelee kumpa Upendo katika kututumikia watanzania" - Mhe. Zaytun Seif Swai, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha

"Katika kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa Rais Samia Suluhu Hassan, tumekuja hapa kupanda miti 100 kwaajili ya kivuli kuwasaidia Ndugu zetu (Wafungwa) wanaoishi Gereza la Wilaya ya Karatu na kuendelea kutunza mazingira" - Mhe. Zaytun Seif Swai, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha

"Tumefanya hivyo kwaajili ya kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni muhifadhi namba moja ni mtunza mazingira namba moja. Ametuletea maendeleo mengi watanzania hususani wana Arusha tunajivunia kuwa na Rais Samia Suluhu Hassan" - Mhe. Zaytun Seif Swai, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha

"Nilisikia wafungwa wanawake walikuwa na changamoto ya kukosa maji safi na salama kwa ukosefu wa tanki. Mimi na UWT Wilaya ya Karatu kwa pamoja tumekuja kuwaletea tanki la maji ili wafungwa wapate maji safi na salama" - Mhe. Zaytun Seif Swai, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha

"Tumesikia changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo wafungwa katika Gereza la Karatu, tumezichua na kuzitatua papo kwa papo na zingine tumeahidi kuzifanyia kazi" - Mhe. Zaytun Seif Swai, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha

WhatsApp Image 2024-01-28 at 13.13.18(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-01-28 at 13.13.18.jpeg
WhatsApp Image 2024-01-28 at 13.13.17(2).jpeg
WhatsApp Image 2024-01-28 at 13.13.17(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-01-28 at 13.13.16.jpeg
 
Back
Top Bottom