Mbunge Samizi achangia ujenzi wa msikiti wa ghorofa Kibondo, Waumini wamtaja Rais Samia

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
328
414
Mbunge wa Jimbo la Muhambwe mkoani Kigoma Mhe. Dkt. Florence George Samizi leo tarehe 07/04/2023 amemtuma Katibu wake Bi. Dorice Nsekela kumwakilisha kwenye msikiti wa Ijumaa na wa wilaya ya Kibondo ambapo alifanikisha kutoa ahadi aliyoahidi ya kuchangia seruji mifuko 50.

Pia, Mbunge wa Njombe Mhe. Neema Mgaya amemuunga mkono Mbunge Dr Samizi kwa kuchangia seruji mifuko 25 na hivyo kufanya jumla ya mifuko 75 iliyochangiwa kwa ajili ya ujenzi wa msikiti huo utakaogharimu milioni 325 ukiwa na ghorofa 1.

Shekhe Mkuu wa msikiti huo na waumini wamemshukuru sana Mbunge Dkt. Samizi pamoja na Mhe. Mgaya kwa kuwaunga mkono ujenzi huo.

Sambamba na hilo, waumini hao wamemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kama ikimpendaza wanayo heshima ya kumuomba chochote atakachojaaliwa ili aweze kuwaunga mkono kwenye ujenzi huo wa msikiti.

Pia wamewakaribisha Watanzania wote wenye mapenzi mema kuwaunga mkono kwenye ujenzi wa msikiti huo.

IMG-20230407-WA0042.jpg
IMG-20230407-WA0043.jpg
IMG-20230407-WA0044.jpg
IMG-20230407-WA0045.jpg
 
Back
Top Bottom