Mbunge Samizi atimiza ahadi ya kuchangia saruji ujenzi wa zahanati na shule ili kumuunga mkono Rais Samia

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
328
414
MBUNGE SAMIZI ATIMIZA AHADI YA KUCHANGIA SARUJI UJENZI WA ZAHANATI NA SHULE ILI KUMUUNGA MKONO RAIS SAMIA.

Dkt. Florence George Samizi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Muhambwe mkoani Kigoma Jana Jumamosi Aprili 29, 2023 ametimiza ahadi yake ya kuchangia shughuli za maendeleo kwa kuchangia mifuko ya saruji kwenye ujenzi wa zahanati na shule ya msingi.

Ahadi ni deni ukiahidi timiza, wiki chache nyuma Dkt. Samizi alikua na mikutano ya hadhara vijiji viwili vya Nyakilenda na Karundo ambapo pamoja na mambo mengine aliahidi kuchangia ujenzi wa zahanati na shule.

Leo Mbunge Samizi amewakilishwa na msaidizi wake Bi. Dorice Nsekela ambapo ameweza kutoa mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa shule ya msingi Karundo iliyoko kijiji cha Kichananga na mifuko mingine 50 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya Nyakilenda iliyoko kata ya Mkabuye ambapo haya yalikuwa moja kati ya kero alizokutana nazo sana Jimboni na kuombwa.

Dkt. Samizi ametimiza ahadi hiyo katika lengo lilelile la kuunga mkono kazi kubwa ya kupeleka maendeleo kwa wananchi inayofanywa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Amiri jeshi Mkuu Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

#KaziInaendeleaMuhambwe

FB_IMG_1682866956259.jpg

FB_IMG_1682866958640.jpg

FB_IMG_1682866961086.jpg
 
Back
Top Bottom