Mbunge Ntate Katika Mkutano wa Utekelezaji Ilani ya CCM Mtaa wa Maganga, Temeke.

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,902
944

MBUNGE JANEJELLY NTATE KATIKA MKUTANO WA USOMAJI WA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM MTAA WA MAGANGA, TEMEKE

Mbunge wa Viti Maalum, Mwakilishi wa Wafanyakazi Nchini anayetokea Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Janejelly James Ntate leo tarehe 07 Oktoba, 2023 ameshiriki katika Mkutano wa kusoma taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020-2025 katika Mtaa wa Maganga, Temeke.

Mkutano huo ulihudhuriwa na mgeni rasmi ambaye ni Mwenyekiti wa Wilaya CCM, Bi. zena Mgaya aliyepongeza juhudi za Mwenyekiti wa Mtaa wa Maganga kwa kufanya kazi kwa bidii kutekeleza Ilani ya Chama bila kuyumbishwa na maneno na changamoto za kifedha.

Taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020-2025 katika Mtaa wa Maganga, Temeke ilisomwa na Ndugu Jafari Ibrahim Shoo ambapo baada ya kuisoma, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Temeke, Bi. Zena Mgaya aliikabdihi taarifa kwa Mbunge wa Viti Maalum, Mwakilishi wa Wafanyakazi Nchini, Mhe. Janejelly James Ntate

Mhe. Janejelly James Ntate amepongeza uongozi wa CCM Wilaya ya Temeke kwa kuonyesha uwazi katika taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020-2025 na kuahidi kuendelea kuwaunga mkono katika shughuli zote za Chama Cha Mapinduzi na Serikali ndani ya Wilaya ya Temeke.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-10-07 at 14.33.33.jpeg
    WhatsApp Image 2023-10-07 at 14.33.33.jpeg
    87.5 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-10-07 at 14.33.34.jpeg
    WhatsApp Image 2023-10-07 at 14.33.34.jpeg
    75 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-10-07 at 14.33.34(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-10-07 at 14.33.34(1).jpeg
    89.1 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-10-07 at 14.33.35.jpeg
    WhatsApp Image 2023-10-07 at 14.33.35.jpeg
    56.4 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-10-07 at 14.33.35(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-10-07 at 14.33.35(1).jpeg
    91.3 KB · Views: 3
Back
Top Bottom