Mbunge Janejelly Ntate Aendesha Semina ya Utekelezaji wa Maono ya Mama Samia kwa Akina Mama wa Mkoa wa Dar

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941

MHE. JANEJELLY NTATE AENDESHA SEMINA YA UTEKELEZAJI WA MAONO YA MAMA SAMIA KWA WAKINA MAMA WA MKOA WA DAR ES SALAAM

Mbunge wa Viti Maalum (Anayewakilisha Wafanyakazi Nchini) Anayetokea Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Janejelly James Ntate leo tarehe 22 Disemba, 2023 Msimbazi Centre, Ukumbi wa Maranta ameendesha Semina ya viongozi wote wa UWT Mkoa wa Dar es Salaam.

Semina hiyo imehusisha viongozi wote wa UWT Mkoa wa Dar es Salaam wakiwemo Kamati ya Utekelezaji UWT Mkoa, Wajumbe wa Halmashauri UWT Wilaya, Wenyeviti UWT Wilaya, Makatibu UWT Wilaya, Makatibu UWT Kata, Wenyeviti UWT Kata, Madiwani wa Kata na Madiwani wa Viti Maalum.

Katika Semina hiyo, mgeni rasmi alikuwa ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Ndugu Abbas Zuberi Mtemvu ambaye katika hotuba yake amesifu utendaji kazi wa Mbunge JANEJELLY NTATE kwani amekuwa Mbunge ambaye amewashika sana mkono Wanawake na Wafanyakazi Nchini.

Mbunge JANEJELLY James Ntate amesema tangu achaguliwe kuwa Mbunge amekutana na Makundi mbalimbali na kuwapa semina za fursa, kusikiliza changamoto na kuzisemea Bungeni, kuelezea utekelezaji wa Ilani ya CCM.

Mhe. Ntate amesema kuwa lengo la semina ya Viongozi wa UWT Mkoa wa Dar es Salaam ni ili kuwakutanisha wanawake hao na Waelimishaji wa masuala ya Kifedha kutoka Tanzania Commercial Benki ili kuzidi kujengeana uwezo.

Aidha, Mhe Ntate amesema lengo pia ni kutakiana heri ya Krismasi na Mwaka mpya ambapo amegawa zawadi mbalimbali kwa makundi ikiwemo kuwapatia TV zaidi ya 300 kwa kila Kiongozi wa UWT Mkoa wa Dar es Salaam ili kuweza kufuatilia taarifa mbalimbali zianzoendelea Nchini.

Mhe. Janejelly James Ntate ameahidi na amesema pia kuwa anapanga kufika na kufanya ziara Kata kwa Kata katika Kata zote za Mkoa wa Dar es Salaam kwani si vyema kuingia kwenye kata zao bila kuwambia mapema juu ya ujio wao.
 

Attachments

  • mahojiano.jpg
    mahojiano.jpg
    1.8 MB · Views: 1
  • elimu.jpg
    elimu.jpg
    3.3 MB · Views: 1
  • mwenykt uwt.jpg
    mwenykt uwt.jpg
    2.8 MB · Views: 1
  • zawadi 2.jpg
    zawadi 2.jpg
    2.6 MB · Views: 2
  • zawadi.jpg
    zawadi.jpg
    2.4 MB · Views: 1
AACHE KUMSINGIZIA MAMA SAMIA UONGO. MAMA SAMIA ANA MAONO GANI MPAKA SASA? HUYU MBUNGE AKAMATWE NA AFUNGULIWE MASHTAKA.
 
Kampeni zimeanza rasmi kila mtu anabuni tu aiiteje mradi akutane na wajumbe wake wa UWT. Anyway,tusio na fedha za kuwakusanya tuwafundishe kuhusu maono ya Mama,fursa na Ilani tutaendelea kutoa maoni JF.
 
Back
Top Bottom