Mbunge Janejelly Ntate ametembelea kituo cha kulelea watoto yatima cha Swadiq development orphanage Tanzania

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,902
945

MBUNGE JANEJELLY NTATE NTATE ATEMBELEA KITUO CHA WATOTO YATIMA CHA SWADIQ ORPHANAGE DEVELOPMENT TANZANIA

Mbunge wa Viti Maalum, Mwakilishi wa Wafanyakazi Nchini anayetokea Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Janejelly James Ntate leo tarehe 26 Machi, 2023 ametembelea Kituo cha kulelea watoto yatima cha SWADIQ DEVELOPMENT ORPHANAGE TANZANIA kilichopo maeneo ya Royal Village Dodoma.

Mhe. Ntate aliwapelekea watoto hao mahitaji muhimu ya Chakula na Malazi kwa ajili ya kutumia kwa kipindi hiki cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Mhe. Ntate ameongea na Bi Mwajuma Issa Jory ambaye ni mlezi wa kituo na kumpongeza kwa kazi ya kitume anayoifanya na kumsisitiza kuwalea watoto katika maadili mazuri hasa kipindi hiki ambacho mmomonyoko wa maadili umekuwa ni mkubwa hasa suala la ushoga na ndoa za jinsia moja.

Mhe. Ntate ameongea na watoto na kuwasisitiza kumshika sana Mungu kwani ndiye muweza wa yote, pia waipende na washike sqna elimu.

Mhe. Ntate aliwaeleza watoto hao jinsi Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan alivyoamua elimu iwe bure kuanzia Shuke za Msingi hadi kidato cha sita, lakini pia ipo mikopo ya elimu ya juu ambapo wakifaulu vizuri watosoma.

Mhe. Ntate aliwaliomba wasijisikie vibaya kwa kuondokewa na Wazazi wao kwani Mungu amewapa mzazi Mama Samia Suluhu Hassan ambaye anahakikisha huduma za kijamii zinapatikana, pia Mungu amewapa Mama Mwajuma hivyo wasiogope.

Katika picha, inaonyesha Mhe. Ntate amevaa mtandio wa kijani akiwa kwenye picha ya pamoja na watoto yatima aliokwenda kuwaona na kuwasalimia kituoni hapo.

WhatsApp Image 2023-03-26 at 13.51.44.jpeg
WhatsApp Image 2023-03-26 at 15.06.28(1).jpeg
 
Back
Top Bottom