Mbunge Ndaisaba aishauri Serikali kuhusu makato ya kodi kwa wawekezaji Madini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944
"Badala ya kutuletea Kodi ya Mapato ya 2% tuwekeeni ya Asilimia 1 mtujaribu kwanza wachimbaji wa madini tuone kama inatekelezeka hii 1% kwanza mkileta asilimia mbili watu wataona ni kubwa na matokeo yake watu wataanza kupitisha madini kwenye njia za panya" - Mhe. Ndaisaba Ruhoro, Mbunge wa Ngara.

"Wapi mliona tuna introduce kodi kwa mara ya kwanza 2% yote ambayo jumla inakuwa 10.3%? kwenye eneo hili niombe iwe asilimia Moja pekee tuijaribu kwanza kwa mwaka wa kwanza mwakani ikienda vizuri ongezeni hiyo nyingine iwe 2% eneo hili lifanyiwe kazi" - Mhe. Ndaisaba Ruhoro, Mbunge wa Ngara.

"Tunamuomba Rais Dkt. Samia aridhie kwa yale maeneo mengine ambayo yako kwenye hifadhi ambayo hayatumiki tuyaondoe TANAPA yaingie TFS ili Watanzania wachimbe madini wawezekufaidika kwenye nchi yao" - Mhe. Ndaisaba Ruhoro, Mbunge wa Ngara.

"Wafanyabiashara wa Ngara hawana njaa tunalima mara mbili kwa mwaka mazao tuliyovuna msimu wa kwanza bado yako majumbani mnatuchelewesha kufanya biashara kama njaa zipo katikati ya nchi njooni mnunue kwetu tuwape mazao" - Mhe. Ndaisaba Ruhoro, Mbunge wa Ngara.

"Makampuni yaliyokidhi vigezo yaruhusuni yaweze kuanzabiashara na sisi ni Taifa huru haiwezekani mtu akatoka nchi jirani anaingia kwa wakulima na kuanza kukusanya mazao na kuyatoa nje ya nchi bila kulipa Kodi Haiwezekani" - Mhe. Ndaisaba Ruhoro, Mbunge wa Ngara.

"Tanzania ni miongoni mwa mataifa ambayo yamekuwa na jeshi la zimamoto ambalo halina vifaa kwaajili ya kuzimia moto, yamewahi kutokea majanga ya moto Watanzania wakakimbia na kukaa uwanjani wakishuhudia Mali zao zikiteketea" - Mhe. Ndaisaba Ruhoro, Mbunge wa Ngara.

"Jambo la kuazima helikopta ya kuzimia moto katika nchi ndogo lilituumiza, lilitufedhehesha Kwasababu kama Taifa tuliona Kuna haja ya kufanya uwekezaji mkubwa kwa kuliwezesha jeshi letu la zimamoto ili liweze kupambana na majanga haya yanayotokea nchini " - Mhe. Ndaisaba Ruhoro, Mbunge wa Ngara.

"Hakuna mwekezaji wa aina yeyote atakubali kuleta fedha zake kuwekeza kwenye nchi ambayo miundombinu yake ikipata moto itaungua na kuisha Kwasababu hakuna vifaa vya kuzima moto huo" - Mhe. Ndaisaba Ruhoro, Mbunge wa Ngara.

maxresdefaultsaqw.jpg
 
Back
Top Bottom