Mbunge Mzeru atoa milioni 10 kuchangia ujenzi wa Nyumba ya Katibu UWT Wilaya ya Morogoro

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Morogoro Mhe. Norah Mzeru Agosti 11, 2023 amekabidhi kiasi cha fedha cha Shilingi Milioni 10 kwa ajili ya Ujenzi wa nyumba ya Katibu wa UWT Wilaya ya Morogoro Mjini ikiwa ni sehemu ya ahadi aliyoahidi ya kuchangia ujenzi wa nyumba hiyo.

Akikabidhi fedha hizo kwa uongozi wa UWT mbele ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Morogoro Fikiri Juma Mhe. Mzeru ameomba usimamizi mzuri ufanyike katika ujenzi wa nyumba hiyo.

Mara baada ya makabidhiano hayo Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro Fikiri Juma amewashauri Uongozi wa UWT uunde kamati ya ujenzi na mchakato wa ujenzi uanze mapema.

Akishukuru mara baada ya kukabidhiwa Fedha hizo Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Morogoro Mjini Victoria Saduka amesema kuwa fedha walizopewa na Mbunge huyo zitaenda kufanyiwa kile kilichokusudiwa huku akiahidi kusimamia vyema ujenzi huo mpaka kukamilika kwake

WhatsApp Image 2023-08-11 at 21.02.25.jpeg
WhatsApp Image 2023-08-11 at 21.02.25(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-08-11 at 21.02.31.jpeg
WhatsApp Image 2023-08-11 at 21.02.35.jpeg
WhatsApp Image 2023-08-11 at 21.02.31(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-08-11 at 21.02.32.jpeg
WhatsApp Image 2023-08-11 at 21.02.28.jpeg
.
 
Back
Top Bottom