Mbunge Kapufi akabidhi zaidi ya Shilingi Milioni 2 Ujenzi wa Nyumba ya Katibu wa CCM Wilaya ya Mpanda

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,662
837

Mbunge Kapufi akabidhi zaidi ya Shilingi Milioni 2 Ujenzi wa Nyumba ya Katibu wa CCM Wilaya ya Mpanda.

MBUNGE wa Jimbo la Mpanda Mjini Sebastian Kapufi amekabidhi zaidi ya Milioni 2 kwa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake (UWT) Wilaya ya Mpanda kwa ajili ya kukamilisha Ujenzi wa nyumba ya Katibu wa Jumuiya hiyo.

Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini Sebastian Kapufi amekabidhi zaidi ya Milioni 2 kwa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake (UWT) Wilaya ya Mpanda kwa ajili ya kukamilisha Ujenzi wa nyumba ya Katibu wa Jumuiya hiyo

Akikabidhi fedha hizo Mbunge Kapufi kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Mpanda Sadick Kadulo kwa niaba ya Mwenyekiti wa UWT katika ofisi za Chama Wilaya ya Mpanda ameipongeza Jumuiya hiyo kwa hatua waliyofikia katika ujenzi wa nyumba ya Katibu na kusema hataishia hapo yupo pamoja na Jumuiya hiyo hadi ujenzi utakapo kamilika.

Nae Katibu wa CCM Wilaya ya Mpanda Sadick Kadulo amemshukuru Mbunge Kapufi kwa kuendelea kukijenga chama kwa kujitolea katika shughuli za Maendeleo ndani ya chama hicho na kumwomba asichoke kwani amekuwa mzalendo katika kukijenga chama.

Kadulo pia amesisitiza ushirikiano baina ya Viongozi wachama na Jumuiya zake ili kuendelea kukijenga chama ili kukiletea Maendeleo katika Jumuiya zake zote.

Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Mpanda Tausi Ramadhani amemshukuru Mbunge Kapufi kwa kutimiza ahadi aliyoitoa katika Jumuiya hiyo ya wanawake na kumwomba asiwachoke kwani bado wanahitaji mchango wake katika kukiimarisha Chama na Jumuiya hiyo kwa ujumla.

Nao baadhi ya Viongozi wa Chama na Jumuiya wamempongeza Mbunge Kapufi kwa kuwa mzalendo katika chama na Jumuiya zake kwa mchango wake katika shughuli za Maendeleo ndani ya chama hicho.
 

Attachments

 • KAPUFI 1.jpg
  KAPUFI 1.jpg
  16.3 KB · Views: 4
 • KAPUFI 3.jpg
  KAPUFI 3.jpg
  17 KB · Views: 4
 • KAPUFI 2.jpg
  KAPUFI 2.jpg
  20.6 KB · Views: 4
Hakuna mbunge kimeo Kama kapufi

Hupenda sifa hivyo hivyo kutangazwa tangazwa na vyombo habari Wala huwa shida za wapiga kura wake mbunge sifa sif a ukipigia simu hapokei utadhani mnadaiana .

Hana lolote mpanda mjini Wala hatuna mbunge wakutesemea bungeni huko hata katika kuchangia mijadala ovyo hakuna anachokifanya huko.

Tutakunana 2025
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom