Mbunge Mhe. Msongozi - Atoa Misaada ya Cherehani 60, Mbegu za Soya, Majiko ya Gesi 106 na Vifaa Tiba Ruvuma

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,895
940

MHE. JACQUELINE MSONGOZI - ATOA MISAADA YA CHEREHANI NA VIFAA TIBA VITUO VYA AFYA MKOA WA RUVUMA

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma na Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe. Jacqueline Ngonyani Msongozi amefanya ziara ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono kwa vitendo Kauli mbiu ya KAZI IENDELEE ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Akiwa na dhamira ya kuwainua kiuchumi wanawake aliwakabidhi Mbegu za Soya ambazo ni Tani 7 zenye thamani ya Milioni 35 ili wanawake wa Wilaya ya Songea wajishughulishe na kilimo cha mazao ya biashara.

Aidha, Mhe. Msongozi aliwakabidhi Majiko 106 ya gesi wanawake 106 wa Wilaya ya Mbinga yenye thamani ya Shilingi Milioni 10 kwa lengo la kusaidia kwa vitendo sera ya kuhifadhi na kutunza mazingira.

Mhe. Msongozi amechangia Vifaa Tiba katika kituo cha Afya cha Ipalama, Vifaa hivyo ni Vitanda Vitatu vya wagonjwa, Magodoro matatu, Kitanda kimoja cha kujifungulia wanawake, na Gloves 200.

Mhe. Msongozi amekabidhi mradi wa ushonaji kwa wanawake na kuwapa Cherehani 60. Amefanya hivyo kwa Wilaya zote za Mkoa wa Ruvuma.

Katika hatua nyingine, Mhe. Msongozi amempatia mmoja wa walemavu wa miguu baiskeli ya kutembelea katika Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma.

Mwisho, Mhe. Msongozi alishiriki ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali Mkoa wa Njombe na kukagua Miradi ya Maendeleo ikiwemo ujenzi wa Barabara ya kiwango cha lami Njombe-Makete, Ujenzi Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Njombe, Ujenzi Miradi ya Maji-Howadi na Ujenzi wa kiwanda cha Mipira ya Gloves cha Idofi kilichopo katika Halmashauri ya Mji wa Makambako Mkoani Njombe.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-03-26 at 09.50.45(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-03-26 at 09.50.45(1).jpeg
    58.5 KB · Views: 6
  • WhatsApp Image 2023-03-26 at 09.51.28(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-03-26 at 09.51.28(1).jpeg
    64.4 KB · Views: 6
  • WhatsApp Image 2023-03-26 at 09.51.23.jpeg
    WhatsApp Image 2023-03-26 at 09.51.23.jpeg
    55 KB · Views: 6
  • WhatsApp Image 2023-03-26 at 09.51.26(2).jpeg
    WhatsApp Image 2023-03-26 at 09.51.26(2).jpeg
    71 KB · Views: 6
  • WhatsApp Image 2023-03-26 at 09.51.27(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-03-26 at 09.51.27(1).jpeg
    103 KB · Views: 6
Back
Top Bottom