Mbunge Ester Midimu Atoa Baiskeli 400 na Majiko ya Gesi 400 kwa Viongozi UWT Mkoa wa Simiyu

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Simiyu Ester Midimu ametoa Baiskeli zaidi ya 400 na majiko ya Gesi zaidi ya 400 kwa viongozi wa Kata kupitia Umoja wa Wanawake (UWT) wa mkoa huo ili kuwawezesha kufanya kazi za Chama Cha Mapinduzi na kutunza mazingira.

Mbunge huyo amesema wanawake hao wamekuwa sehemu ya uhamasishaji kwa wapiga kura, kutafuta kura za Chama cha Mapinduzi, kuhamasisha daftari la wapiga kura na kwamba jiografia ya mkoa wa Simiyu siyo rafiki, hivyo ameamua kuwapatia baiskeli ili ziweze kuwasadia kutafuta kura za Dk. Samia.

Midimu ameyasema hayo jana kwenye kikao cha Baraza la UWT lililofanyika katika ukumbi wa CCM mjini Bariadi ambapo amesema pamoja na kuwapatia usafiri pia ametoa majiko ya gesi kwa kila mmoja ili kuwaondolea adha ya kutafuta kuni na mkaa.

Amesema katika uwezeshaji wanawake kiuchumi, ametoa zaidi ya shilingi mil. 45 ili kuwezesha vikundi vya wanawake ili wajikwamue kiuchumi kwa kuongeza mitaji katika biashara zao na waweze kujiongezea vipato.

‘’Natoa baiskeli 450 na majiko 450 yenye thamani ya shilingi Mil. 230 kwa wakina mama kupitia Umoja wa wanawake, tuendelee kumuunga mkono Dk. Samia Suluhu Hassan ambaye tangu aingie madarakani amejenga hospitali tatu ndani ya mkoa wa Simiyu wilaya za Busega, Itilima na Bariadi’’ amesema Ester.

Mbunge huyo amewataka wanawake kuendelea kuhamasisha wanawake wenzao ili wajitokeze kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa (2024) na uchaguzi mkuu utakaofanyika mwakani 2025 huku akiwasisitiza kuchagua viongozi wanaotokana na CCM.

Awali Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) Mkoa wa Simiyu Mariam Manyangu amewataka wanawake hao kuwa mstari wa mbele kukipigania Chama Cha Mapinduzi ili kiendelee kuwa madarakani.

Amewataka kufanya kazi kwa bidii katika ngazi za vijiji na kata kutafuta wanachama wapya ili kuongeza kura za Dk. Samia Suluhu Hassan na kwamba Umoja wa Wanawake wamejipanga kumchukulia fomu ya kugombea Urais Dk. Samia ikifika 2025.

WhatsApp Image 2024-01-16 at 16.01.47(2).jpeg
WhatsApp Image 2024-01-16 at 16.01.47(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-01-16 at 16.01.47.jpeg
WhatsApp Image 2024-01-16 at 16.01.46(2).jpeg
WhatsApp Image 2024-01-16 at 16.01.46(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-01-16 at 16.01.46.jpeg
WhatsApp Image 2024-01-16 at 16.01.45(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-01-16 at 16.01.45.jpeg
 
Yes give them Fish, Huwezi sikia, kaja na miradi ya kundoa umasikini, maje akiondoa umasikini atakosa watu wa kumuabudu, hizo ndio njia pekee za CCM kujihakikishia kuwepo Madarakani, lazima watu wapewe samaki, na sio kufundishwa jinsi ya kubua samaki.
 
Back
Top Bottom