NAIBU Waziri TAMISEMI, Mhe Dkt. Festo Dugange - Tsh. Bilioni 8 Zimepelekwa katika Mkoa wa Njombe kwa ajili ya Ununuzi wa Vifaa Tiba

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
944
NAIBU Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Dkt.Festo Dugange amesema ndani ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan zaidi ya Sh. Bilioni 8 zimepelekwa katika Mkoa wa Njombe kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba.

Mhe. Dugange ameyasema hayo akiwa katika ziara ya Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango mkoani Njombe alipokuwa akizungumza wafanyakazi wa kiwanda cha mbao cha TAN WAT kilichopo wilayani Njombe.

"Mhe Makamu wa Rais kipekee sana nimshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo ndani ya miaka miwili amefanikiwa kuboresha sekta ya afya katika Mkoa huu wa Njombe. Kiasi cha Sh Bilioni 8 kimeletwa kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba na dawa.

" Miaka miwili ya Rais Dkt Samia amejenga Hospitali za Wilaya katika Wilaya ya Wanging'ombe, Njombe Vijijini, Mji wa Makambako huku akipeleka Sh Milioni 900 kwa Wilaya ya Ludewa na Makete kila moja kwa ajili ya ukarabati wa Hospitali," amesema Dkt. Dugange.

Amesema Mkoa wa Njombe ulikuwa una upungufu wa vituo vya afya lakini ndani ya miaka miwili vimejengwa vituo vya afya 17 pamoja na Zahanati 34 ndani ya Mkoa huo.

F9YZhkjW4AAkcBu.jpg
F9YZhkmWwAAwjsQ.jpg
F9YZhknXAAEXGT9.jpg
F9YZhkkX0AAPcnz.jpg
F9a_R7VWoAASUdP.jpg
 
Back
Top Bottom