Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,682
- 1,234
MHE. JACQUELINE KAINJA AHOJI ZAHANATI KUFUNGULIWA BILA VIFAA TIBA MKOA WA TABORA
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tabora, Mhe. Jacqueline Kainja Andrew katika kipindi cha maswali na majibu Bungeni ameuliza maswali Wizara ya TAMISEMI yaliyojibiwa na Naibu Waziri TAMISEMI.
"Je, Serikali ina mpango gani kuhakikisha Zahanati kabla haujazinduliwa inawekewa vifaa tiba" - Mhe. Jacqueline Kainja, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tabora
"Katika mwaka wa fedha 2022-2023 Serikali imetoa Shilingi Bilioni 15.15 kwaajili ya ununuzi wa vifaa tiba kwenye Zahanati ambazo zimekamilika ambapo tayari Serikali imetoa Shilingi Bilioni 12.90" - Mhe. Deogratius Ndejembi, Naibu Waziri TAMISEMI
"Katika mwaka wa fedha 2023-2024 Serikali imetenga fedha Shilingi Bilioni 18.4 kwaajili ya ununuzi wa vifaa tiba kwenye Zahanati zote zinazoendelea kukamilishwa na itaendelea kutenga fedha kwaajili ya Zahanati zinazoendelea kukamilishwa kwa kadiri fedha zinapopatikana" - Mhe. Deogratius Ndejembi, Naibu Waziri TAMISEMI
"Kwanini Serikali inapotenga fedha za majengo ya Zahanati na Vituo vya Afya isitenge sambamba na fedha za vifaa tiba? Mara nyingi majengo yanafunguliwa wakati vifaa tiba hakuna" - Mhe. Jacqueline Kainja, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tabora
"Nini tamko la Serikali kwamba kuna fedha zimetengwa kwa ajili ya vifaa tiba katika Mkoa wa Tabora kwa Zahanati ambazo hazina vifaa tiba na tayari wananchi wanachangishwa Fedha za mabenchi kama Zahanati ya Goweko, Kalangire Wilaya ya Uyui, Wilaya ya Igunga, Kagongo Kata ya Itunduru na Ibuta Kata ya Mbutu" - Mhe. Jacqueline Kainja, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tabora
"Imekuwa ni kipaumbele cha Serikali kujenga miundombinu kwanza ili huduma za Msingi ziweze kuanza kutolewa ndipo Serikali inatenga fedha kwaajili ya ununuzi wa vifaa tiba na kuvipeleka kwenye Zahanati" - Mhe. Deogratius Ndejembi, Naibu Waziri TAMISEMI
"Serikali imeweka kipaumbele katika kuhakikisha vifaa tiba vinakuwa katika Zahanati zote, Vituo vya Afya vyote na katika Hospitali za Wilaya kote nchini katika kuhakikisha Afya za Watanzania zinaboreka. Serikali imetenga Shilingi Bilioni 112 mwaka wa fedha 2023-2024" - Mhe. Deogratius Ndejembi, Naibu Waziri TAMISEMI