Mbunge Martha Mariki Aitaka Wizara ya Mambo ya Ndani Kuboresha Makazi ya Polisi na Magereza

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
944

MARTHA FESTO MARIKI AITAKA WIZARA YA MAMBO YA NDANI KUBORESHA MAKAZI YA POLISI NA MAGEREZA

"Katika Mkoa wa Katavi katika Jeshi la Zimamoto tuna takribani zaidi ya miaka 12 hatuna gari la uhakika la Zimamoto. Mkoa unakua, Serikali imewekeza ikiwepo Bandari. Mkoa unapokea wafanyabiashara wengi kutokana na Biashara ya Kilimo " - Mhe. Martha Festo Mariki, Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Katavi

"Mkoa wa Katavi, Gari tulilokuwanalo lilipata ajali tokea mwaka 2012 likaenda kupatiwa matengenezo, lakini mpaka leo gari halijaweza kurudi katika Mkoa wa Katavi. Gari tunalolitegemeq ni dogo lipo Airport. Ikitokea ajali ya moto na ndege inatua gari litaweza kuzima moto?" - Martha Festo Mariki, Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Katavi

"Nikuombe Mheshimiwa Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi Mkoa wa Katavi una uhitaji wa gari la Zimamoto na ukizingatia Mkoa wa Katavi unakua" - Martha Festo Mariki, Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Katavi

"Jeshi la Magereza, katika Mkoa wa Katavi kumekuwa na msongamano mkubwa sana wa wafungwa na mahabusu ukizingatia Geraza la Wilaya ya Mpanda Mjini ambalo linachukua karibu wafungwa wote katika Mkoa" - Martha Festo Mariki, Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Katavi

"Gereza linaweza kupokea Wafungwa 100 lakini mpaka sasa lina wafungwa takribani 400 ambao wamesongamana. Tujiulize, ukitokea mlipuko wa Magonjwa nini kitatokea?" - Martha Festo Mariki, Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Katavi

"Naiomba Wizara, Mkoa wa Katavi tumeshaleta maombi yetu, tumeshatenga eneo lipo Mpimbwe katika Kata ya Usevya eneo kubwa la kutosha kwaajili ya kujenga Magereza. Tunaomba tujengewe Gereza ili kuondoa msongamano" - Martha Festo Mariki, Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Katavi

"Shirika la Uzalishaji la Magereza (SHIMA) hapo mwanzo lilikuwa halifanyi vizuri lakini tunalipongeza. Ila tunataka lije na mkakati. Mkoa wa Katavi na Rukwa tuna mashamba makubwa sana yanayomilikiwa na Magereza lakini SHIMA limeshindwa kutumia rasilimali kulima Chakula cha kutosha ili kuipunguzia Serikali mzigo wa kuwahudumia wafungwa ambao wamekuwa na upungufu mkubwa wa chakula" - Martha Festo Mariki, Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Katavi

"Naiomba Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi iweze kuisimamia SHIMA liweze kufanya Kilimo ikiwezekana Kilimo cha umwagiliaji ili kuendana na wakati. Wakitumia Kilimo ipasavyo hawatakuwa na upungufu wa Chakula." - Martha Festo Mariki, Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Katavi

"Ni aibu kubwa kwa Taifa lenye maeneo makubwa sana kushindwa kutumia Ardhi kulima chakula cha kutosha na matokeo yake kuipa Serikali mzigo wa kuwahudumia wafungwa Magerezani. Wanayo nguvu kazi wafungwa, waweze kuitumia waweze kupata chakula cha kutosha" - Martha Festo Mariki, Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Katavi

"Tunaomba Shirika la SHIMA ikiwezekana lifuge liweze kupata Mifugo ambayo itasidia akina Mama ambao wapo Magereza waliofungwa na watoto wadogo. Wale watoto hawana hatia, wale watoto wadogo wataweza kupata Maziwa. Wizara lisukume SHIMA liweze kufanya kazi vizuri" - Martha Festo Mariki, Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Katavi

"Makazi ya Askari Polisi na Askari Magereza; Makazi yao yanasikitisha. Tuwape heshima maaskari hawa. Kama wanatulinda kwanini tusiweze kuboresha mazingira yao. Tuwape vifaa vya kufanyia kazi. Tuwape magari na tuwabadirishie unifomu zao mara kwa mara ili waweze kuwa Nadhifa" - Martha Festo Mariki, Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Katavi

"Ukiangalia nyumba za Maaskari unaweza kulia machozi. Watu hawa ni muhimu sana kwa Taifa letu, wanatulinda, wanasababisha tunakuwa na amani. Kwanini tusiwalinde watu hawa ili wawe na Mazingira mazuri katika kazi zao!" - Martha Festo Mariki, Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Katavi

"Polisi Jamii; Polisi Jamii wamefanya kazi nzuri kwenye kila Kata wakituhusisha UWT, lakini ili waweze kufanya kazi vizuri ni vyema tukajipanga na kujenga vituo vya Polisi kila Kata na kuwapelekea vitendea kazi. Hawana vitendea kazi, watafanyaje kazi!" - Martha Festo Mariki, Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Katavi

"Ukizingatia uhalifu mkubwa unafanyika kwenye Kata zetu, tukiwaboreshea mazingira wakaweza kufanya kazi vizuri tutaweza kukomesha uhalifu kuanzia ngazi za Kata, Wilaya na ngazi ya Mkoa" - Mhe. Martha Festo Mariki, Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Katavi

"Maeneo mengi wananchi hawana uelewa na Masuala ya Ukatili lakini kupitia Polisi Jamii tukitenga fedha kwaajili ya Elimu hususani Vijijini wananchi wengi watakwenda kupata uelewa ni wapi wakashitaki kuliko kuficha Mambo yanayofanya uhalifu kwenye maeneo yetu kama ulawiti na ubakaji" - Martha Festo Mariki, Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Katavi.

 
Back
Top Bottom