SAGAI GALGANO
JF-Expert Member
- Nov 13, 2009
- 43,707
- 60,767
January Makamba pia hana nyumba Bumbuli
mbona balozi wa nchi ana makazi nje ya nchi yake na anatoa huduma na kupeleka maendeleo nchini mwake? it works like that
Na inakuwaje mbunge wa sehemu fulani apewe ukuu wa mkoa mahala pengine...........??? Au hata huyo waziri mkuumfano mbunge wa tarime kapanga na makazi yake yako dar es salaam je inakuaje muda wake wote ameishi dar alafu apate ubunge tarime, ni kitu gani huwa kinatokea kwa wananchi wanao amua kumpa kura mtu ambaye wanajua kabisa akishapata uongozi anarudi kwenye makazi yake ambako amezoea na kwa shughuli zake zote
Mimi nafiriki mbunge anapaswa kupimwa kwa namna anavyotekeleza au atakavyotekeleza ahadi zake kwa wananchi na si kwa kuwa au kutokuwa na nyumba jimboni,kwani hili halitowasaidia wananchi mwisho wa siku!!!
....Sio contradiction yoyote kwa sababu sio kosa la mbunge kuwepo kwa simu moja ya kukoroga. Unaongelea "hewa" ...Awaachie wanaoweza kukaa huko na kuondoa hali umasikini kwa kufanya kazi bega kwa bega na waliomchagua.Kwanini asigombee jimbo lenye simu kila kona ili awasiliane vizuri na wizara? Kama angekuwa anaishi huko jimboni kwake lazima hayo matatizo yangemgusa pia na angetafuta solution right away.
...Ndiyo shida ya umasikini na ndg yake umbumbumbu..... maana hata priority hatuzijui na badala ya kuangalia mambo ya msingi tunaanza kuhangaikia mambo ya nani anaishi wapi ect. Kazi gani hizo za bega kwa bega au paja kwa paja ambazo unategemea hao masikini wazifanye ili kuleta hayo maendeleo ?
Binafsi hata kama mbunge anakaa nje ya inji, i dont care kama wajibu wake anautekeleza. I care about the end product- period na sio anaishi wapi ect.
Na kwa mfumo huu wa sasa ambapo mawaziri na baadhi ya watendaji wakubwa wanatokana na hao hao wabunge, unategemea waziri wa maji awe anaishi Mfaranyaki (au mkuu wa mkoa dodoma awe anaishi Masasi), wakati serikali kuu ipo DSM ?. Na utawezaje kulazimisha wengine waishi majimboni, na wengine no say kwa sababu ni mawaziri au wana dhamana flan ?
mbona balozi wa nchi ana makazi nje ya nchi yake na anatoa huduma na kupeleka maendeleo nchini mwake? it works like that
Wewe KIlembwe kweli!!! Tatizo lako unasahau kuwa wabunge wengi ni wa CHAMA chako hivyo unavyozungumzia wabunge wangapi basi ulitakiwa ujue kuwa Wabunge wengi wa chama chako hawana nia ya dhati ndio maana wengi wao hawana nyumba majimboni mwao! Kwa taarifa yako si dhambi mbunge kuwa na nyumba DAR au mbali na Jimbo lake! Ila Walau awe na nyumba Jimboni kwake na muda mwingi autumie jimboni kwake. Kwa taarifa yako zaidi ya 75% ya Wabunge wa CDM walioshinda majimbo yao wanakaa Sehemu husika ukilinganisha na chama chako!
HAWA NDIO WATANGANYIKA BONGO LA-LA-LA A LA AAAAAAAA!! YAANI MBUNGE WAO AKISHACHAGULIWA WATAMWONA TENA WAKATI WA UCHAGUZI AU WAKATI AMESIKIA KIONGOZI WA SERIKALI ANATEMBELEA JIMBONI MWAKE NDIO UTAMWONA ANAJISHEBEDUA KUWA KARIBUKARIBU! HII INATIA SHAKA KAMA KWELI WANANCHI WENGI WATANZANIA HUWA WANAJUA WANACHOKIFANYA WAKATI WA KIPIGA KURA!
>>> Mfano mtu kama huyu Mbunge wa Tarime sijui anaitwa '' Nyambari Nyagwine''....Anaishi Dar es saalaam ni lini atajua matatizo ya wana TARIME? .....Ndo maana sishangai kusoma habari zake kwenye gazeti la Mwananchi la leo 03/01/2011 Anakutana na wajumbe wa CCM kawe kuwauliza kwa nini Jimbo la KAWE Limechukuliwa na wapinzani (Chadema) !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! JE HAYA NDO WANA TARIME WALIYOMTUMA??????????????? Watu kama hawa 2015 waogopwe kama UKoma......
huyu mbunge wa tarime walichakachua kura lakini alikuwa atakiwi kwa wanatarime
bora hao wa tarime walizaliwa huko......mbona morogoro,singida , rukwa, tabora wanawahusudu waasia (akina rostamu)kwenye ubunge km vile ni wazawa kuliko hata watoto wao ambao serikali ya kikwete inawakamua kwa kuwasomesha kwa ghjarama kubwa lakini bado wanabaki kusujudia rangi................wana watoto wengi tu wanaoweza kuwasaidia na wanaojhua vema matatizo yao lakini wanajidharau wenyewe........waache hao wa tarime nk walienda kupata maarifa na wanarudi na jipya sudhani km kuna shida hapo.....ni sawa tu na mtz kwenda kutafuta maarifa ng'ambo baada ya miaka mingi anakuja tunampa uongozi sembuse dar-tarime?